Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Kufuatia kufungwa kwa kanisa la Glory of Christ (Ufufuo na Uzima), viongozi wa kanisa hilo sasa wamesema wamepata hifadhi katika Kanisa Katoliki kigango cha Bikira Maria Kimara Dar es Salaam.
Akizungumza leo Julai 27 katika ibada iliyofanyika katika ukumbi wa Kilato uliopo Kimara Stop Over, kiongozi wa kanisa hilo, Askofu Baraka Tenge, amesema baada ya usumbufu wa kupata sehemu ya kuabudu sasa wamepata hifadhi hiyo.
Awali baada ya kanisa hilo kifungwa Juni 2, 2025 waumini hao walikiwa wakikusanyika pembeni ya kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini walifukuzwa na polisi.
Baadaye walitafuta hifadhi katika Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM), ambapo pia walifukuzwa na sasa kanisa hilo limevunjwa.
Kisha waumini hao walihamia katika Ukumbi wa Tanzanite uliopo Kimara.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando alisema waumini hao wamemaliza semina hivyo waondoke.
Katika ibada ya leo Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Vernon Fernandes alishiriki na alihubiri.