Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

So, what😳😳😳😳😳
 
Pietro wa italy ndio atachaguliwa (mtazamo wangu)


Ila ningependa papa atoke ulaya mashariki kule ukrsto upo moyon
Hasa kutoka poland hungary na malita
Huyu Pietro Parolin aweza kabisa kuchaguliwa kwani alikuwa akishika nafasi pale papa francis alipoanza kuugua.

Ila huyu ni jasusi mbobezi na alikuwa mshauri mkuu wa papa Francis.

Ni mwanadiplomasia na mtawala mzuri.

Italy wangependa kadinali Matteo Zuppi achaguliwe na ambae alikuwa karibu sana na Papa Francis.

Huyu aitwa kadinali wa mtaani Street Cardinal kwa mtindo wake kuwa kujichanganya na watu wa aina zote kuanzia kanisani hadi mitaani.

Na umri wa miaka 69.

Kwanini huenda Kadinali Matteo Zuppi akachaguliwa kuwa Papa?

1. Ni mpenda amani na amekuwa akishiriki kutatua migogoro mbalimbali khasa barani Afrika nchini Burundi, Kolombia na Kosovo. Hivyo ni msuluhishi mzuri.

2. Aliteuliwa kuwa kadinali mwaka 2019 baada ya kuwa askofu wa Rome na Bologna baada ya kuonyesha umahiri katika shughuli za kikanisa, kupigania haki ndani ya jamii na kipaji cha uongozi.

Hata hivyo kadinali Matteo ana upinzani mkali kutoka kwa kadinali Jose Tolentino de Mandonca kutoka Ureno. Huyu kazaliwa Ureno lakini kakulia Angola na baba yake alikuwa ni mvuvi.

Kadinali Mendonca alijiunga na seminari akiwa na umri wa miaka 11 na alikuja kupata uparoko mwaka 1990. Ana shahada ya udaktari wa theolojia na amefundisha sana katika vyuo vikuu vya theolojia nchini Ureno na Marekani.

Mwaka 2019 aliteuliwa kuwa kadinali na Papa Francis.

Sifa zake huyu ni pamoja na kuunganisha madaraja ya watu mbalimbali ndani ya kanisa katoliki, na kuwa tayari kusikiliza ktuoak kwa watu mbalimbali bila kujali watu hao watoka katika nchi ipi.

Makadinali kutoka Afrika wana nafasi yoyote?

1. Kadinali Fridolin Ambongo Besungu mwenye umri wa miaka 65 ni kadinali kutoka Kinshasa nchini Kongo DRC. Ni mjumbe pekee kutoka barani Afrika alie katika baraza la makadinali. Hili baraza liliundwa na Papa Francis ili kusaidia kumshauri masuala ya uongozi na kufanya mabadiliko ndani ya kanisa.

Nafasi ya kadinali Besungu kuwa papa ni ndogo sana kutokana na kauli zake nyingi za kuwazodoa mabeberu kwamba wanakomba mali za Afrika huko Congo DRC na kauli zingine tata.

2. Kadinali Robert Sarah mweye umri wa miaka 79 atokea nchini Guinea. Lakini nafasi ya kadinali Sarah kuwa papa ni ndogo sana kutokana na umri wake ambapo mwaka huu atatimiza umri wa miaka 80.

3. Kadinali Peter Turkson kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 76 ambae pia umri wake utakuwa tatizo

Wapo makadinali wengineo kama kadinali Mario Grech kutoka Malta ambae ana umri wa miaka 68, kadinali Luis Antonio Tagle kutoka Ufilipino mwenye umri wa miaka 67, kadinali Jean Marc Avelin mwenye umri wa miaka 66 anetokea Ufaransa.
 
Zuppi yuko vizuri
Ila mchuano mkali ni kati ya Asia na Ulaya.

Asia nao wana hao makadinali Tagke na kadinali Lazarro You Heung kutoka Korea Kusini ambae nae aliteuliw ana papa Francis kuwa kadinali mwaka 2022, na ongea kitaliano kiufasaha.

Huyu ametembea sana barani Afrika, Asia na Ulaya akitangaza neno la Mungu.

Akiwa na umri wa miaka 73 itakuwa kikwazo kwake lakini kutokana na rekodi yake kusimamia viongozi wa kanisa na pia kuonyesha kutotamani sana madaraka, vyaweza kuwafikirisha makadinali kumpigia kura.
 
Kila laheri kwa hao Makardinali
 
EBO mm nikadhani moshi mweusi Manake tumepata PAPA mweusi kwamala ya Kwanza kumbe nyeusi manake akuna kitu ndani yani O !!!

afu Nyeupe ndio kuna kitu ndani awa Jamaaa langi nyeusi Sijui imewakwanza nini !!!!!

Sisi weusi tunakandamizwa kisaikolojia !!!

mbaya zaid Wazee wetu Walinogewa na Vibeskuti iyouyo walivolishwa na Wazungu !!!!6g

zipo adi nyimbo za Kibaguzi lkn mtu Mweusi nayeye anaimba !!!

nyimbo kama ilivo bila kutafakari maudhui yake!!!!!! Tutafika tukiwa tupo hooooooii
 
Zoezi la kumchagua Papa limeingia siku ya pili leo baada ya process ya jana kushindwa kumchagua papa mpya ambaye anapaswa kupata angalau 2/3 ya kura zote 133. Zoezi la jana usiku lilichukua muda mrefu zaidi na ilivyotarajiwa, hali iliyolazimu zoezi kusitishwa hadi leo asubuhi, baada kushindwa kupata mshindi.

Siku ya pili imeendelea leo bila majibu. Hata hivyo, muda mfupi kabla ya saa sita mchana muda wa Vatican, au saa saba kamili saa za Tanzania moshi mwingine mweusi umeonekana, ikiashiria kuwa zoezi bado limeshindwa kumpata kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki.

Tetesi zinasema cardinals walipiga round ya 2 na ya 3 bila majibu leo asubuhi. Hivyo kama maelezo ni sahihi awamu inayofuata ni round ya 4.

Kwa sasa cardinals wameelezwa kuelekea kupata lunch, ambapo zoezi litaendelea tena baadaye. Makadinari wametengwa na yanayoendelea duniani ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano, ikiwemo simu zao za mkononi.

Kwa Mkatoliki popote ulipo huu ni muda wa kuendelea kuwaombea makadinari, kama tunavyojua vita kali ambayo kanisa linapitia hivi sasa. Jipe hata dakika chache usali hata ile sala ya "Baba Yetu" aliyotufundisha Kristo mwenyewe ili kanisa limshinde shetani.
 

Attachments

  • Screenshot_20250508-125712_YouTube.jpg
    266.8 KB · Views: 19
Maandiko kwenye Biblia yanaonyesha viongozi hawakuchaguliwa bali waliitwa na bwana kwa nyakati tofauti. Hii ya Vatican naona haina tofauti na michakato ya nafasi za kisiasa au ile ya katibu mkuu wa UN.
Hili jambo linanishangaza?
Hata hivyo hili kanisa Sanaa nyingi
 
Naona mpaka sasa hakuna jipya kuhusu papa mpya

Wale mnaofwatilia najua Jana ikitokea Moshi mweusi mns ajapatokana

Vipi na Leo Moshi mweusi unaendeleaaaaaaaaaa
 
Kwa mara ya pili Moshi weusi umeonekana Tena ktk kura ya kupata pope mpya
Ikimaanisha Pope hajaaptikana Leo tena
 

Attachments

  • IMG_20250508_163013_776.jpg
    346.5 KB · Views: 21
  • IMG_20250508_163012_365.jpg
    358.1 KB · Views: 25
  • IMG_20250508_162819_579.jpg
    402.3 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…