Kanisa Katoliki lasitisha huduma za kufungisha ndoa na ubatizo hadi pale ugonjwa wa COVID-19 utakapodhibitiwa

Kanisa Katoliki lasitisha huduma za kufungisha ndoa na ubatizo hadi pale ugonjwa wa COVID-19 utakapodhibitiwa

Kwa nini kanisa linaacha kuchapa kazi?
Rais wa TEC baba Askofu Nyaisonga ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Mbeya amesema katika kupambana na maambukizi ya Covid 19 wanasitisha Huduma za sakramenti ya ubatizo na ile ya Ndoa.

Baba askofu amesema Huduma hizo zitarejea tena kama kawaida pale ugonjwa huo utakapokuwa umedhibitiwa.
Baba askofu amesema hayo wakati wa ibada za Pasaka jijini Mbeya.

Source ITV habari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mbeya tu siyo majimbo yote. Kila Askofu ana eneo lake la kiutawala.
Tamko halijatolewa na TEC, ni yeye Kama yeye. Nimeona hii habari ITV jana Saa2 usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa TEC baba Askofu Nyaisonga ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Mbeya amesema katika kupambana na maambukizi ya Covid 19 wanasitisha Huduma za sakramenti ya ubatizo na ile ya Ndoa.

Baba askofu amesema Huduma hizo zitarejea tena kama kawaida pale ugonjwa huo utakapokuwa umedhibitiwa.
Baba askofu amesema hayo wakati wa ibada za Pasaka jijini Mbeya.

Source ITV habari!
Ibada za ndoa na Misa za kawaida zipi zenye watu wengi?
 
Fanya kurekebisha mkuu...Isomeke
"Amezuia SHAMRASHAMRA za ubatizo na ndoa"
sawa kabisa
lkn jana tumemaliza shamrashamra kwa muumini mmoja hapo Dodoma baada ya kubatiza
na zilienda safi na kwa amani kabisa
 
Halafu tusisali sio?
Sali ukiwa nyumbani au popote siyo lazima uende kanisani. Baba 'mtakatifu' mwenyewe amesalisha misa bila waumini kutokana na ugonjwa kwanini na hawa wa kwetu walioipokea dini hiyo wasifute misa? Kama issue ni sadaka watoe namba za Mpesa, tigo, airtel, halotel na ezy pesa tutatuma na ya kutolea
 
kwa hiyo tuliokuwa mbioni kufunga ndoa tupotezee tuendelee na haka katendo ka ndoa!!!! au hakueleweka uzuri?
 
Back
Top Bottom