Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Ni wapi huo waraka umezungumzia habari za ushoga ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Too lateSiku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba.
Katika waraka huo wenye Point 66, umevavaduliwa kama ifuatavyo
USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.
Andiko gani linasema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe kanisani?Ile statement ipo biblical kaka, hakuna mwenye dhambi hata mmoja anaye paswa kufungiwa mlango na kanisa, kilichomleta Yesu duniani sio kwa yoyote aliye mwema ila kwa wote walio na dhambi ambao dhamiri zao zinawadai kufanya toba na marejeo kw Mungu muumba wao.
Kama walipata uongozi wa Mungu kubariki wapenzi wa jinsia mojaHakuna shaka papa na uongozi wa vatikani ulipata msaada na mwongozo wa ki Mungu kabla ya kutoa kauli ile.
Paul alishauri tu wanaojiweza wakae bila kuoa/ kuolewaKwani mapadre na watawa wa kike wanapungukiwa kipi hasa wasipokuwa na wenza wao ?
Mafundisho ya mtume Paulo umesoma ?
Wanaochagua upadre wanajiwezaPaul alishauri tu wanaojiweza wakae bila kuoa/ kuolewa
Wakishindwa wawe na mke/mme mmoja
Safi sana Nimependa Alivyofanya Hapa sasa kajidafisha na atakufa akiwa Shujaa
Ndio maana nikasema alitoa ushauri tu.Wanaochagua upadre wanajiweza
Ushujaa gani mkuu?Safi sana Nimependa Alivyofanya Hapa sasa kajidafisha na atakufa akiwa Shujaa
kabadili gia angani, angeweza kuligawa kanisa katolikiHataki? Kwa nini alisema wabarikiwe?
Unaamini tamko lake lilivuviwa na Roho mtakatifu kama wanavyodai wengine?kabadili gia angani, angeweza kuligawa kanisa katoliki
Tafsiri ya Shujaa sio Yule anayejificha kwenye mapambano lah..Ushujaa gani mkuu?
Sahihi.Tafsiri ya Shujaa sio Yule anayejificha kwenye mapambano lah..
Shujaa ni yule anayeingia kwenye mapambano hata kama mwanzoni aliona kaharibu, bhasi bado hurudi hadharani na kusema nilikosea huo hauitwi unafiki Unaitwa ushujaa...
Ila ukiona mtu hata baada ya kukosea anaendelea kushikiria Msimamo wa Kijinga mchunguze sana huyo Mtu anaunafiki na majuto moyoni mwake..
Ndugu yangu si wewe wa la si mimi au mingoni mwetu wengi ambao tunaifahamu Biblia kwa asili yake kiukamilifu.Andiko gani linasema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe kanisani?
Nakubali hakuna mwenye dhambi anapaswa kufungiwa mlango, na natambua Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi.
1.Lakini kuna tofauti hapo, Yesu alimfata Zakayo mtoza ushuru (alikuwa mwenye dhambi maana aliwadhurumu watu mali zao), akampa injili hatimae Zakayo akaacha dhambi (akaacha kudhurumu na akarudisha mali za aliowadhurumu mara 4 zaidi)
2.Yesu alipoletewa mwanamke aliefumaniwa akifanya uzinzi (dhambi), alimsamehe na kumwagiza asitende dhambi tena.
Swali langu kwako, Papa aliposema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe je kuwabariki kungewafanya waache dhambi zao (kufanya mapenzi ya jinsia moja) au wakibarikiwa maana yake aendelee kufanya dhambi (kuendeleza mapenzi ya jinsia moja)?
Kama walipata uongozi wa Mungu kubariki wapenzi wa jinsia moja
1. Kwanini watu wa sodoma na gomora walichomwa?
2. Kwa nini kauli imebadilika sasa, je Mungu amegundua alikosea kuruhusu jambo alilolikataza mwenyewe?
USHOGA NA KUBADILI JINSIASwali langu kwako, Papa aliposema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe je kuwabariki kungewafanya waache dhambi zao (kufanya mapenzi ya jinsia moja) au wakibarikiwa maana yake aendelee kufanya dhambi (kuendeleza mapenzi ya jinsia moja)?
With due respect.Ndugu yangu si wewe wa la si mimi au mingoni mwetu wengi ambao tunaifahamu Biblia kwa asili yake kiukamilifu.
Hatuna kingi katika ufahamu kuzidi wanazuoni au wanateolojia na wanafalsafa waliopo pale Vatican.
Msimamo wa kanisa kwa leo haujitimishi leo tu bali kesho na kesho kutwa na mtondogoo.
Swali langu halijibiwi na huo waraka.USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.
👆
Huo ndio msimamamo wa kanisi kuhusu hilo ulilouliza!
Naam naweza kuwa siijui Biblia ndugu yangu, maana Biblia ni kama kioo, kila anaekitazama anajiona yeye, ndio maana kila leo anatokea huyu anatafsiri hivi na yule anatafsiri vile!With due respect.
Naifahamu biblia nje ndani. I'm a theologian for 20 yrs now
Wewe umesema agizo liko biblically, nimetaka andiko unasema si mimi wala wewe tuanoijua bilbia. Nakuhakikishia wewe ndie hujui Biblia.
Mimi sijawahi fungwa na dini, nimesoma kuhusu ukristo, uislam, butha, uyahudi nk.
Nakuhakikishia tena hujui Biblia, usipotoshe watu kwa maneno matupu.
Ukisoma vitabu vyote 72 kwenye biblia yako, hakuna sehemu Mungu wala nabii wala mtume kasema WAPENZI WA JINSIA MOJA WABARIKIWE.Naam naweza kuwa siijui Biblia ndugu yangu, maana Biblia ni kama kioo, kila anaekitazama anajiona yeye, ndio maana kila leo anatokea huyu anatafsiri hivi na yule anatafsiri vile!
Hebu tupe darasa kidogo mkuu kuhusu Biblia ufanuvyo wewe sio sawa na wengine tulivyo jaliwa kufahamu.