Kanisa Katoliki latoa waraka mpya unaiotwa 'Dignitas Infinita' likipinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba

Mashoga wanabarikiwa kwa maana gani?
Jibu hapo kama una akili.
Hilo swali muilize papa wako ndie alisema wabarikiwe.
Hakuna shoga anapaswa kubarikiwa. Anatakiwa atubu, aache ushoga Ndipo anaweza barikiwa.
 
Nimependa busara na hekima ya majibu yako. Kiukweli ukiona mtu anasema anaijua biblia inatakiwa uwe naye makini, huenda anamaanisha kukariri mistari ndio kujua biblia maana hata shetani anajua biblia na vitabu vya dini zote ulimwenguni.

Yesu alipokuja duniani alikubalika na wale wa kawaida ila alikataliwa na wanaojua torati ambayo ni kama biblia kwa sasa.

Kikubwa sio kujua biblia, unaweza usijue hata mstari mmoja ila je, unaishi ndani ya neno au umekariri? Hilo ndio la muhimu.

Maana hata mbinguni katika hukumu hatutaulizwa mistari ya biblia bali matendo yetu.
Nilitegemea ukosoe majibu yangu kwa hoja, badala yke unaleta mipasho tu.
Mbona muuliza swali alinielewa nilichosema?
 
Hivi ni kwa nini wahamiaji haramu Mfano hawa wanaokamatwa wakiwa wanakwenda au wanapita tuu nchini kwetu kwenda kujitafutia maisha mahali pengine na wala sio nchini mwetu kwa nini tusiwaache kwa sababu sisi haituhusu na wala haituathiri chochote kupita kwao hapa tuache jukumu hili huko wanakokwenda wakaelewana
 
Siku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba.

Katika waraka huo wenye Point 66, umevavaduliwa kama ifuatavyo

USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.

KUTOA MIMBA
Point ya 47 inasisitiza kanisa linakataa utoaji mimba, na kwamba ni kinyume cha mapenzi ya MUNGU, na kwa sababu mtoto yeye hana makosa na hawezi kujitetea. Utoaji mimba ni kosa katika miiko ya kanisa

KUPANDIKIZA MIMBA (SURROGACY)
Point ya 48, 49, na 50 Kanisa linakemea kitendo cha kubeba mwanamke kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine au kupandikiza mimba, likisisitiza Mtoto anatakiwa kubebwa katika mfuko wa uzazi wa mama yake na si mtu mwingine.

VITA
Point ya 38 na 39 kanisa linahimiza kuepuka vita, na kupinga vikali vitendo vyote vinavyochochea vita au ubaguzi kwa namna yeyote.

WAHAMIAJI HARAMU (IMMIGRANTS)
Point ya 40 kanisa linasisitiza wahamiaji haramu wasitengwe au kufanyiwa uvunjifu wa utu wao, Kanisa linataka wahamiaji haramu watendewe mema kama watu wengine kwa sababu hawakutaka kuwa katika hali hiyo, hivyo jamii ziwapokee, ziwasaidie na si kuwabagua.

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU (HUMAN TRAFFICKING)
Point ya 41 na 42 kanisa linasema litaendelea kupambana na vitendo vya kusafirisha binadamu kwa ajili ya kuuza viungo vyao vya mwili, kwa ajili ya kazi za kitumwa, kwa ajili ta kazi za umalaya, kwa ajili ya kuwatumikisha kingono mabinti na vijana wadogo, kwa ajili ya vitendo vya kigaidi na kazi zote za namna hiyo.

UKATILI WA KIJINSIA
Point ya 43 kanisa linapinga ukatili wa aina yoyote wa kijinsia

UKATILI WA WANAWAKE
Point ya 44, 45 na 46 Kanisa linapinga ukatili wa wanawake ikiwemo rushwa ya ngono, kitendo cha kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe kuwafurahisha wanaume, vipigo, kuwashurutisha kutoa mimba, bila kusahau kuwafanyia ndoa za mitaala (wake wengi), vitendo hivyo vyote vinapingwa na kanisa

KUSITISHA MAISHA YA MGONJWA, AU KUSAIDIA MTU KUJITOA UHAI
Point ya 51 na 52 kanisa linakataza kitendo cha kukatisha maisha ya mgonjwa kwa namna yoyote au kumsaidia mtu kujitoa uhai. Kanisa linaimiza hata kama mtu ni mahututi kiasi gani au hawezi kupona basi ni vyema tumfariji mpaka pale umauti wake utakapomfika na si kutoa uhai wake kwa namna yoyote hata kama ni kwa ridhaa yake.

UBAGUZI WA WALEMAVU
Point ya 53 na 54 Kanisa linapinga vitendo vya ubaguzi na kuwatenga walemavu.

VURUGU MITANDAONI YA KIDIGITALI
Point ya 61 na 62 kanisa linakumbusha kutumia mitandao katika njia nzuri, na sio kutumia kuumiza wengine. Kanisa linasema kazi ya Teknolojia ya kidigitali ni kumsaidia binadamu na si kumdhuru.

SOMA WARAKA WOTE HAPA CHINI: Declaration of the Dicastery for the Doctrine of the Faith “Dignitas Infinita” on Human Dignity
da!! ukioga uani wakati tanesco wamezima umeme,alaf ghafla umeme ukarudi!!!! inakuaje hapo kwa mfano!!!
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Nilitegemea ukosoe majibu yangu kwa hoja, badala yke unaleta mipasho tu.
Mbona muuliza swali alinielewa nilichosema?
Sio mipasho ni hoja na pia ni ukweli mshirika wa kanisa katoliki ambaye ni biden ni mfuasi wa ushoga, kama kanisa mnapaswa kumkanya arudi kundini.

Na pia marekani ni wachochezi katika vita hilo liko wazi kila mtu anajua. Nchi nyingi zimeharibiwa kwa vita kwa uchochezi wa marekani na kiongozi wenu wa kanisa katoliki amekuwa kimya muda wote wala hakemei.

Hii ni hoja na ukweli tosha, wewe ndio unataka kuingiza mipasho.

Huu waraka ni mzuri na unapaswa utekelezwe kwa vitendo hiyo ndio maana yangu. Kwa sasa vitendo kwenye hivyo vipengele viwili nilivyoonesha ni sifuri.
 
Ulinikosoa kuwa nimekaririshwa tu Biblia siijui, nikataka unikosoe kwa hoja.

Kitu ambacho hukijui kunihusu ni kwamba sijawahi na wala sitakuja kuwa muumini wa Roman catholic.

Huyo niliemkosoa ukani-quote ni kwa vile alitetea maamuzi ya papa kuruhusu mashoga kubarikiwa. Na akadai tamko liko kibiblia ndio maana nikataka anipe andiko. Akajibu mimi na yeye hatujui Biblia, nikamjibu yeye ndie hajui ila mimi naijua vizuri ndio maana nikadiriki kumwambia hakuna hilo andiko.

Post zilizofata alikubali kwamba kweli hakuna andiko.
 
Pumbavu pekee ndie hujibu hoja kwa kuwatukana wenzake wapumbavu ili kuficha upumbavu wake.

Catholic haijawahi upambania ukristo.
Serikali ya Kirumi ilikubali dini ili kuhudumia mahitaji yao. Badala ya dini kuwa kitu kinachofanywa na makuhani , serikali ya Roma iliigeuza kuwa njia ya kudhibiti watu, kuleta umoja wa kitaifa, kutia uhasama wa haki kwa askari, kuhalalisha ongezeko la kodi na kadhalika. Ili kufanya hivyo, walihitaji dini ambayo inaweza kuvutia mtu yeyote na walifanya hivyo kwa kuanzisha catholic.

Kwa kifupi.
Warumi walikuwa wanaitawala Israeli kipindi cha Yesu, na ukristo ulikuwepo na makanisa yalikuwepo. Walishiriki kutaka kumuua kipindi anazaliwa kupitia kwa Herode kwa hofu ya kupoteza utawala wao. Kipindi Yesu anauwawa ni warumi walimuua kwa sheria zao sio za wa Israel. Sheria ya kirumi ilikuwa kutundikwa mtini, na ya kiyahudi ni kupigwa mawe. Baada ya kifo cha Yesu waliendelea kuwasakama wanafunzi wake na kuwatesa na kuwaua. Pamoja na yote hayo bado ukristo ulizidi kusambaa, kipindi hicho warumi wana mipango ya kutawala dunia, wakaona hawa wanaomwamini Yesu ni kikwazo katika utawala wao, kibaya zaidi wanaongezeka. Ndipo wakaja na wazo la kuanzisha kanisa ili waweze kuwa control, wakaiba machapisho ya kale ya kiyahudi na kupeleka kwao, wakayatumia kuandaa Biblia. Wao ndio walichagua vitabu wanavyovitaka na kuacha wasivyovitaka.

Tamaa za kidunia ni za catholic ndio maana wanakubali kubariki mashoga ili wasikose sadaka za washirika.
Basi babaako aliupambania ukristo.
 
Siku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba.

Katika waraka huo wenye Point 66, umevavaduliwa kama ifuatavyo

USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.

KUTOA MIMBA
Point ya 47 inasisitiza kanisa linakataa utoaji mimba, na kwamba ni kinyume cha mapenzi ya MUNGU, na kwa sababu mtoto yeye hana makosa na hawezi kujitetea. Utoaji mimba ni kosa katika miiko ya kanisa

KUPANDIKIZA MIMBA (SURROGACY)
Point ya 48, 49, na 50 Kanisa linakemea kitendo cha kubeba mwanamke kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine au kupandikiza mimba, likisisitiza Mtoto anatakiwa kubebwa katika mfuko wa uzazi wa mama yake na si mtu mwingine.

VITA
Point ya 38 na 39 kanisa linahimiza kuepuka vita, na kupinga vikali vitendo vyote vinavyochochea vita au ubaguzi kwa namna yeyote.

WAHAMIAJI HARAMU (IMMIGRANTS)
Point ya 40 kanisa linasisitiza wahamiaji haramu wasitengwe au kufanyiwa uvunjifu wa utu wao, Kanisa linataka wahamiaji haramu watendewe mema kama watu wengine kwa sababu hawakutaka kuwa katika hali hiyo, hivyo jamii ziwapokee, ziwasaidie na si kuwabagua.

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU (HUMAN TRAFFICKING)
Point ya 41 na 42 kanisa linasema litaendelea kupambana na vitendo vya kusafirisha binadamu kwa ajili ya kuuza viungo vyao vya mwili, kwa ajili ya kazi za kitumwa, kwa ajili ta kazi za umalaya, kwa ajili ya kuwatumikisha kingono mabinti na vijana wadogo, kwa ajili ya vitendo vya kigaidi na kazi zote za namna hiyo.

UKATILI WA KIJINSIA
Point ya 43 kanisa linapinga ukatili wa aina yoyote wa kijinsia

UKATILI WA WANAWAKE
Point ya 44, 45 na 46 Kanisa linapinga ukatili wa wanawake ikiwemo rushwa ya ngono, kitendo cha kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe kuwafurahisha wanaume, vipigo, kuwashurutisha kutoa mimba, bila kusahau kuwafanyia ndoa za mitaala (wake wengi), vitendo hivyo vyote vinapingwa na kanisa

KUSITISHA MAISHA YA MGONJWA, AU KUSAIDIA MTU KUJITOA UHAI
Point ya 51 na 52 kanisa linakataza kitendo cha kukatisha maisha ya mgonjwa kwa namna yoyote au kumsaidia mtu kujitoa uhai. Kanisa linaimiza hata kama mtu ni mahututi kiasi gani au hawezi kupona basi ni vyema tumfariji mpaka pale umauti wake utakapomfika na si kutoa uhai wake kwa namna yoyote hata kama ni kwa ridhaa yake.

UBAGUZI WA WALEMAVU
Point ya 53 na 54 Kanisa linapinga vitendo vya ubaguzi na kuwatenga walemavu.

VURUGU MITANDAONI YA KIDIGITALI
Point ya 61 na 62 kanisa linakumbusha kutumia mitandao katika njia nzuri, na sio kutumia kuumiza wengine. Kanisa linasema kazi ya Teknolojia ya kidigitali ni kumsaidia binadamu na si kumdhuru.

SOMA WARAKA WOTE HAPA CHINI: Declaration of the Dicastery for the Doctrine of the Faith “Dignitas Infinita” on Human Dignity
Kwenye kupandikiza mimba umepotosha sasa sijui kwa maslahi ya nani. Ungesema linakataza kupandikiza mimba kw niaba lakin wewe umeonyesha kana kwamba kanisa linapinga kupandikiza mimba kwa ujumla wake hata kama ni kwa wana ndoa ambao wanafanya kwa ajili yao wenyewe na sio kwa kubeba mimba kwa niamba ya mtu mwingine.

Sent from my itel S13 using JamiiForums mobile app
 
1 .Chanzo cha taarifa yako ni media ipi? 2.Muda utakwambia uchafu wote wa vatican..........narudia tena it's just a matter of time. Hivi kwanini maraisi kibao lazma waende vatican? including Watanzania?

Tena wanaenda officially? kuna nini huko vatikani ......vijundi vyote vya kishetani vimeasisiwa vatican i.e JESUITS ILUMINANT FREEMASONS etc.

NB hayo yote uliyoyataja yanapigiwa chapuo na vatikan n swala la muda tuu ...sema wakatoliki wengi sanamu zimewalumbaza ata hamuwezi kung'amua lipi ni lip.

Allah akbar

View attachment 2958227
Mkuu acha kusikiliza masheikh wa buguruni na huko kijiwe samli ndio wanawapa hizo pumba kupitia cds zao huko uswahilini..
Pia acha kuwasilikiza wachungaji wa kisabato ambao wapo depressed itakusaidia.
 
JESUITS ILUMINANT FREEMASONS etc.
Ushetani wao ni upi? Tofautisha secret societies na ushetani. Chambo kuwa siri haikifanyi kiwe cha kishetani. Hao Illuminati ilikua armed/intelligence Wing ya kanisa na ilishakua disbanded miaka zaidi ya 300 sasa. Hao jesuites mbona ni order tu kama Constantine n.k. wala haimaanishi ni shetani.
 
jambo usilolijua n sawa na usku wa giza
 
Back
Top Bottom