Kanisa Katoliki latoa waraka mpya unaiotwa 'Dignitas Infinita' likipinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba

Kanisa Katoliki latoa waraka mpya unaiotwa 'Dignitas Infinita' likipinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba

kwa hiyo Vatican wanataka kusema ushoga na usagaji ni mpango wa Mungu
 
Siku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba.

Katika waraka huo wenye Point 66, umevavaduliwa kama ifuatavyo

USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.

KUTOA MIMBA
Point ya 47 inasisitiza kanisa linakataa utoaji mimba, na kwamba ni kinyume cha mapenzi ya MUNGU, na kwa sababu mtoto yeye hana makosa na hawezi kujitetea. Utoaji mimba ni kosa katika miiko ya kanisa

KUPANDIKIZA MIMBA (SURROGACY)
Point ya 48, 49, na 50 Kanisa linakemea kitendo cha kubeba mwanamke kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine au kupandikiza mimba, likisisitiza Mtoto anatakiwa kubebwa katika mfuko wa uzazi wa mama yake na si mtu mwingine.

VITA
Point ya 38 na 39 kanisa linahimiza kuepuka vita, na kupinga vikali vitendo vyote vinavyochochea vita au ubaguzi kwa namna yeyote.

WAHAMIAJI HARAMU (IMMIGRANTS)
Point ya 40 kanisa linasisitiza wahamiaji haramu wasitengwe au kufanyiwa uvunjifu wa utu wao, Kanisa linataka wahamiaji haramu watendewe mema kama watu wengine kwa sababu hawakutaka kuwa katika hali hiyo, hivyo jamii ziwapokee, ziwasaidie na si kuwabagua.

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU (HUMAN TRAFFICKING)
Point ya 41 na 42 kanisa linasema litaendelea kupambana na vitendo vya kusafirisha binadamu kwa ajili ya kuuza viungo vyao vya mwili, kwa ajili ya kazi za kitumwa, kwa ajili ta kazi za umalaya, kwa ajili ya kuwatumikisha kingono mabinti na vijana wadogo, kwa ajili ya vitendo vya kigaidi na kazi zote za namna hiyo.

UKATILI WA KIJINSIA
Point ya 43 kanisa linapinga ukatili wa aina yoyote wa kijinsia

UKATILI WA WANAWAKE
Point ya 44, 45 na 46 Kanisa linapinga ukatili wa wanawake ikiwemo rushwa ya ngono, kitendo cha kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe kuwafurahisha wanaume, vipigo, kuwashurutisha kutoa mimba, bila kusahau kuwafanyia ndoa za mitaala (wake wengi), vitendo hivyo vyote vinapingwa na kanisa

KUSITISHA MAISHA YA MGONJWA, AU KUSAIDIA MTU KUJITOA UHAI
Point ya 51 na 52 kanisa linakataza kitendo cha kukatisha maisha ya mgonjwa kwa namna yoyote au kumsaidia mtu kujitoa uhai. Kanisa linaimiza hata kama mtu ni mahututi kiasi gani au hawezi kupona basi ni vyema tumfariji mpaka pale umauti wake utakapomfika na si kutoa uhai wake kwa namna yoyote hata kama ni kwa ridhaa yake.

UBAGUZI WA WALEMAVU
Point ya 53 na 54 Kanisa linapinga vitendo vya ubaguzi na kuwatenga walemavu.

VURUGU MITANDAONI YA KIDIGITALI
Point ya 61 na 62 kanisa linakumbusha kutumia mitandao katika njia nzuri, na sio kutumia kuumiza wengine. Kanisa linasema kazi ya Teknolojia ya kidigitali ni kumsaidia binadamu na si kumdhuru.

SOMA WARAKA WOTE HAPA CHINI: Declaration of the Dicastery for the Doctrine of the Faith “Dignitas Infinita” on Human Dignity
Sawa.
 
Sisi tunashikilia kauli yake ya kwanza ndio sahihi . Tunahitaji maelezo kwanini mwanzo alisema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe?
 
jambo usilolijua n sawa na usku wa giza
Acheni propaganda ni sawa na useme TISS ni mashetani kisa ni taasisi ya kisiri!!

Jesuites ni order kabisa na ipo kama tu Benedictine, Francisca etc na haina connection yoyote na ushetani.
 
Sisi tunashikilia kauli yake ya kwanza ndio sahihi . Tunahitaji maelezo kwanini mwanzo alisema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe?
Kubarikiwa means kuombewa baraka ibadani na alisema uwe muuaji, mzinzi, shoga n.k haikunyimi haki ya kuombewa. Ni sawa na Yesu alivyosema kahaba sio tu asiadhibiwe ila yeye alijichanganya naye!!

Meaning maombi ni kwa wenye dhambi sio watakatifu!! Ni ajabu kanisa kufukuza wenye dhambi ilihali wanapaswa kuwaombea ili wabadilike.
 
Tujaribu kuacha mihemko kwa kuipambania taasisi [Roman Catholic]tusiyoijua vizuri,tuijadili taasisi na uongozi wake bila kuwaingiza waumini wa dhehebu la Catholic.
Ufunio wa Yohana 2;13/16;10 na 17;18 imenyoosha maelezo kuwa Vatican ndipo kilipo kiti cha enzi cha Shetani [hatuwezi kuyapinga maandiko]Imeelezewa humu harakati za Rumi kutaka kutawala dunia zilianza zaman [tangu kuzaliwa kwa Yesu Kristo]na zinaendelea hadi sasa.Shetani ndiye anayeratibu mipango na mikakati yote akiitumia Roman Catholic chini ya upapa[papa wote wanalijua hilo kuwa wao ni mawakala wa Ibilisi.Machafuko yote yanayoendelea duniani mf.vita,ugaidi,mmong'onyoko wa maadili[ushoga,usagaji,usawa wa kijinsia 50/50 n.k.]magonjwa ya mlipuko mf.corona,ebola,mafua ya nguruwe,mafua ya ndege n.k. ,mauaji mbalimbali yaliyotokea na yanayoendelea mf.ya kimbari Rwanda,DRC Congo n.k.,mifumuko ya bei kwenye mataifa mbalimbali pamoja na umasikini wa makusudi n mengine mengi,yote hayo yanaratibiwa na taasisi hii ya Roman Catholic chini ya mawakala wao waliopo kwenye kila taifa ulimwenguni , na sasa wana kauli mbiu yao ya MABADILIKO YA TABIA NCHI ambayo imebeba ajenda za kuhitimisha mpango wao hadi kufikia mwaka 2030[Google UN agenda 2021-2030 Goals]. Mikakati yote imelenga jambo/kusudi moja tu ambalo ni ibada kwa Shetani.
Tujizoeshe kuwa wadadisi wa kujua ukweli kwa kusoma vitabu [Biblia n.k]ili tuelimishane kwa hoja,na sio kwa mihemko na matusi.
 
Kubarikiwa means kuombewa baraka ibadani na alisema uwe muuaji, mzinzi, shoga n.k haikunyimi haki ya kuombewa. Ni sawa na Yesu alivyosema kahaba sio tu asiadhibiwe ila yeye alijichanganya naye!!

Meaning maombi ni kwa wenye dhambi sio watakatifu!! Ni ajabu kanisa kufukuza wenye dhambi ilihali wanapaswa kuwaombea ili wabadilike.
Kwahiyo wanaume wawili wakienda kanisani wanataka baraka za kuishi pamoja padre au askofu anaruhusiwa kuwabariki wakaishi pamoja?
 
Kwahiyo wanaume wawili wakienda kanisani wanataka baraka za kuishi pamoja padre au askofu anaruhusiwa kuwabariki wakaishi pamoja?
Wapi walisema wabariki NDOA? Kubarikiwa ni ile kuombewa na kiongozi wa dini kwa ajili ya shughuli zako n.k.

Ni sawa na wezi mbona wanasali kanisani? Je kuna siku kanisa limewahi kataa kuombea mtu kisa ni mwizi? Ingekua hivyo why Yesu aliandamana na zakayo na yule kahaba?

Maombi ni ya wenye dhambi wakiwemo wezi, ndoa za jinsia moja pia wazinzi kama wewe!!
 
Wapi walisema wabariki NDOA? Kubarikiwa ni ile kuombewa na kiongozi wa dini kwa ajili ya shughuli zako n.k.

Ni sawa na wezi mbona wanasali kanisani? Je kuna siku kanisa limewahi kataa kuombea mtu kisa ni mwizi? Ingekua hivyo why Yesu aliandamana na zakayo na yule kahaba?

Maombi ni ya wenye dhambi wakiwemo wezi, ndoa za jinsia moja pia wazinzi kama wewe!!
Acha kuleta maneno mengi nimekuuliza wanaume wawili wenye mahusiano ya kingono wakienda kwa padre kuomba wabarikiwe watakataliwa?
 
Ile statement ipo biblical kaka, hakuna mwenye dhambi hata mmoja anaye paswa kufungiwa mlango na kanisa, kilichomleta Yesu duniani sio kwa yoyote aliye mwema ila kwa wote walio na dhambi ambao dhamiri zao zinawadai kufanya toba na marejeo kw Mungu muumba wao.
😂 Na baada ya KIFO cha Yesu hakuna mwenye dhambi tena maana dhambi zote alizichukua pale Msalabana, namaanisha hakuna binadamu mwenye dhambi baada ya KIFO cha Yesu

Daniel 9 : 22-25
 
Back
Top Bottom