Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Hilo ni kanisa lenu mkuu heri ungetaja kigango na parokia ipi
Mengi tu sahv yapo hivyo,,,ni machache kwa sasa ambayo yamebaki kama zamani,,,,,,,kwa sasa matangazo ya michango na harambee ni kama part ya misa,unaweza ukakaa nusu saa nzima ni makelele ya michango tuu na jamaa wanakua wakali kama wao ndo sir God kashuka duniani kudai chake
 
Waumini wanakamuliwa kweli kweli, ni kuwa makini sana makanisa yanafanya biashara siku hizi, wanaangalia fedha tu, ni kero kubwa sana, kikubwa ni wewe jpili toa sadaka yako 500 au usitoe hakuna kesi wala kushtakiwa
 
Usanii tu huyo si ndo yule mwenye ile shule wanamuita faza pekupeku,,,,,,anaishije kifukara wakati ana shirika linamuhudumia,,,,mafukara wapo ila sio hawa
Ndio mmiliki wa shule ya sekondari ya Alfa.
Ukweli anaishi kifukara na pengine ni moja wapo wa mapadre wachache wanao ishi viapo na nadhiri zao kikamilifu.
Padre wa kanisa katoliki anaweka nadhiri na kiapo cha Ufukara, useja na utii.
Wengi wa mapadre ufukara hawajaweza kuwa waaminifu kwa hilo.
 
Anaishi kifukara ila sio fukara.....ni kama ndani una msosi ila ukaamua kushinda njaa
 
Tunaomba usi-generalize tafadhali! Kanisa Katoliki linajielewa! Kwa akina Mwamposa mkiagizwa kuku mweupe mnapeleka bila kuhoji! Wacha hizo mkuu! Sasa unataka nani aje akujengee Parokia yako?
 
Umegundua ukristu ni biashara, kinachokupeleka huko ni nini. Tumieni tu imani zenu za asili. Zina nguvu kuliko hizi imani za Kiyahudi.
 
Niliacha kwenda church kimkakati
 
Moja wapo ya ujinga mkubwa tumefanya ni kuwapa mitaji hawa wahuni, sasa wamekuwa wafanyabiashara na dini inatumika kuendelea kukusanya pesa za kufanyia biashara.

Watanzania tuamke, katoriki walipofikia hawahitaji kupewa pesa ya aina yoyote, hizo sadaka mkawape wenye uhitaji.

Mitaji mikubwa tuliyowapa iliyozaa biashara kubwa inatosha kabisa kuendesha mambo ya kidini. Mtakuwa wapumbavu sana kama mtaendelea kuwarundikia pesa hawa wafanyabiashara ya dini
 
Nimecheka kama mazuri, pole muamini wa Bwana
 
Nimehesabu bahasha nilizonazo toka mwaka jana zinafika 15. Hio ni michango ambayo sijaitoa kabisa.
Kuna mchango eti wa mashindano kati ya UWAKA (chama cha wanaume); WAWATA (chama cha wanawake); VIWAWA (chama cha vijana) na UTOTO MTAKATIFU (chama cha watoto) nani atamzidi mwenzake wakati hawa wote wanatoka familia moja au nyumba moja. Ni kama KIKOKOTOO cha aina fulani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…