Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamuwa waumini michango hadi wanachukia dini.Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto,halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda.Michango ya ujenzi inautaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Kwani msipotoa wanawanyima pumzi ?
Acheni kujiendekeza.
 
Kuna mchango eti wa mashindano kati ya UWAKA (chama cha wanaume); WAWATA (chama cha wanawake); VIWAWA (chama cha vijana) na UTOTO MTAKATIFU (chama cha watoto) nani atamzidi mwenzake wakati hawa wote wanatoka familia moja au nyumba moja. Ni kama KIKOKOTOO cha aina fulani hivi.
Jamaa mi naona wanazingua tu af kwenye jumuiya ya juzi wakawa kama wamenichunia hivi😁
 
Ndio mmiliki wa shule ya sekondari ya Alfa.
Ukweli anaishi kifukara na pengine ni moja wapo wa mapadre wachache wanao ishi viapo na nadhiri zao kikamilifu.
Padre wa kanisa katoliki anaweka nadhiri na kiapo cha Ufukara, useja na utii.
Wengi wa mapadre ufukara hawajaweza kuwa waaminifu kwa hilo.
Unaujua ufukara lakn kiongozi 😃 huyo anaigiza ufukara
 
Sie wengine tumeishia kwenda kusali tu , mengine mbele kwa mbele,,,ukisema ujifanye muumini mzuri unaanza kukaangwa tokea kwenye jumuiya
Fikiria siku za Kazi ni Siku 6, siku moja Ukalime kwenye Jumuia, siku ya pili ukalime kanisani, Siku nyingine ni siku ya Mafungo au Ibada ya Mtakatifu Petro.

Una baki na siku tatu, nyingine ukajitolee kwenye hizi shule za Kata za ccm.

Umaskini hauwezi kuisha.
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamuwa waumini michango hadi wanachukia dini.Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto,halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda.Michango ya ujenzi inautaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Kwani mnalazimishwa kwenda huko makanisani?

Mtu ukisema sitaki kwenda, watakulazimisha uende?
 
Kuna mchango eti wa mashindano kati ya UWAKA (chama cha wanaume); WAWATA (chama cha wanawake); VIWAWA (chama cha vijana) na UTOTO MTAKATIFU (chama cha watoto) nani atamzidi mwenzake wakati hawa wote wanatoka familia moja au nyumba moja. Ni kama KIKOKOTOO cha aina fulani hivi.
Huu ni wizi wa kutumia akili
 
Hapa umegeuka kuwa mpotoshaji wa wazi kwa kusema eti huu ni wizi wa kutumia akili. Hiyo ni njia tu ya kuwahamasisha waumini kuchangia.
Na uzuri hiyo michango huwa tunachanga kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa! Na mchanganuo wa matumizi yake siku zote ni wa wazi.
Hili suala miaka ya karibuni limewachosha waumini wengi, ndo maana imefika hatua hata waumini wengine kutopenda kwenda kanisani wala jumuiya,.
Siku hizi kama mtu huna sadaka huwezi kwenda kanisani, maana wananyanyua bench moja baada ya nyingine.
 
As i said before! Kanisa ni mali yetu waumini. Kwa hiyo ni sisi wenyewe ndiyo tutakao lijenga.

Kuhusu kutoa sadaka kwa kunyanyuka benchi moja baada ya jingine; kwa upande wangu sioni kama kuna shida! Tena Parokiani kwangu huwa wanasema kama huna hiyo sadaka, unaenda pia kule mbele na waumini wenzako kumshukuru Mungu ili wiki ijayo akupatie kipato cha kutoa kama wengine.
 
Nilichoona wengi wanafuata mkumbo,.kujionyesha Kwa watu
Watu wengi wanaishi kwa kuangalia macho ya watu, kuangalia jamii inawaonaje, si kwa kuangalia wao wenyewe wanataka kuishi vipi?

Matokeo yake unafiki mwingi.

Unatoa kwa kulazimishwa huku roho inakuuma, bora hata tuliojiamulia tusiende kanisani kabisa, hatutaki unafiki.
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Pigaaaa hao maamae , na juzi nikaona video moja padili mmoja ananyandua kademu uganda huku kajirekodi duh yaani mnachangia hela zenu watu wanaend kunyandulia, hatari sana
 
Sadaka sikuizi imekua ni kama lazima maan unatajwa jina au unanyanyuliw kwa aibu n unatoa au kuahid ila walioweng awazitimiz ahadi zao kwa kuwa aiufungaman na moyo wake
KKKT jumapili ya kawaida kuna sadaka ya shukrn ya wiki ,ahadi na jengo (kadi),shukrani ya neno (baada ya maubili) na kazi za jimbo na mission . Izi nne ni lazima ziwepo hapo bado zaka mala vijana wanatak kwend kushoot video wanaitaji mchango ukifanya masiala 10 linakatika pale pale
 
Back
Top Bottom