Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

As i said before! Kanisa ni mali yetu waumini. Kwa hiyo ni sisi wenyewe ndiyo tutakao lijenga.

Kuhusu kutoa sadaka kwa kunyanyuka benchi moja baada ya jingine; kwa upande wangu sioni kama kuna shida! Tena Parokiani kwangu huwa wanasema kama huna hiyo sadaka, unaenda pia kule mbele na waumini wenzako kumshukuru Mungu ili wiki ijayo akupatie kipato cha kutoa kama wengine.
Hata usipokuwa wazi, utaenda kupinga wapi..?
Takukuru..?
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
This is a criminal offence, HUMAN TRAFFICKING
 
Parokia/Kigango cha wapi mkuu?
 
Mkuu misaada haijapungua sana ila hawz wandungu wanatamani hata V8 wakati wale mapadre wakizungu hawakuwa na matumizi ya anasa hivyo.
Vatican imefilisika ,,,,,katoliki ya ujerumani ndo yenye pesa kwa sasa na ndo hao wanaolazimisha mambo ya ushoga,,,....hawa wa huku wameachiwa majukumu mapema kabla hawajajipanga na wao wanaendekeza tena ubinafsi, kila padri anataka ndinga na kula goodlife kwa migongo ya waumini
 
Unaujua ufukara lakn kiongozi 😃 huyo anaigiza ufukara
Ni fukara kweli brother, 2004 niliwahi kumtembelea kwenye makazi yake pale nanenane Morogoro, ndani kwao hakuna hata sahani, chakula kinaliwa kwenye sufuria ya kupikia glass za maji hamna, vitanda na magodoro yao ni duni mno, hawana nguo ama kanzu ya pili, kanzu yake ine jaa viraka kila sehemu, ikichanika wanashona kwa sindano ya mkono.
Usafiri alio nao ni baiskeli ambayo pia ni duni mno, na hio baiskeli hupanda pale anapo wahi ibada kanisa kuu st Patrick, au kipindi redio ukweli.
Vinginevyo anatembea kwa miguu safari nyingi.
Redio ukweli ilikuwa yake kabla haijamilikiwa na jimbo.
So ni fukara kweli japo ana hudumia miradi yenye thamani kubwa.
 
Me catholics wanachonikwaza ni pale tunapochanga kwenye jumuia kujenga buildings for social welfares kama Dispensary, ukumbi or whatever alau ukishakamilika hawa wanajumuia wa chini kabisa huku, waliojinyima kujenga hivyo vitega uchumi, hawapati incentives yeyote kwenye matumizi ya vitu walivyojenga kwa gharama zao. Inaumiza sana maana hatuombi iwe for free lakini unaweza sema kwa mwaka kila mwana jumuia hai apewe angalau discount charges ya hata 15% kila mara anapoenda ku seek huduma ambayo alichangia kwenye uanzishaji wake.
Kwa sasa wanaenda kukopa benki baadae mnaambiwa waumini mrejeshe mkopo, kinachoumiza zaidi ni kuona maduka ya biashara yaliyoshamiri mjini yakiendeshwa na wadada wanaosadikika ni wake wa ma-fr.
 
Uje penda kuzungumzia mambo ya Parokia yako na Paroko wako na viongozi wako uliowachagua.

Kila mtu ana parokia yake na jimbo lake. Hivyo jambo likifanyika kwenye parokia au kigango chako usianze kulihusisha kanisa zima Katoliki.

Kila Jimbo, Parokia au kigango kila utaratibu wake na uongozi wake.

Na unao Uhuru kamili wa kutoa maoni, mapendekezo, ushauri lipi baya halifai au lipi jema liendelee kupitia jumuiya yako, mikutano ya Kigango au Parokia yako ambapo wajumbe wa mikutano hiyo wanatokana na jumuiya.

Ila kama huwa husali jumuiya au kushiriki masuala yote ya kanisa unavizia matukio tuu, ubatizo, kipaimara, komunyo au ndoa na misiba hakika wacha mnyooshwee kisawa sawa.
Hizi unaandika nadharia tu na wewe, huna uhalisia, kuna baadhi ya mambo yakiishapitishwa na paroka na baraza la walei..wewe huku kwenye jumuiya ni kutekeleza tu huwezi kupinga.Hakuna hiyo demokrasia kwenye kanisa katoliki..michango mingi kwa ngazi ya chini huwa ni taarifa tu..nyie mnatekeleza..sio kuanza kuhoji
 
Ukweli usemwe,Kanisa la sasa kwa asilimia kubwa limepoteza mwelekeo.
Kipaumbele cha kanisa& watumishi waliowengi kimekuwa pesa,na siyo kuutafuta ufalme wa Mungu.
Miongozo ya uendeshaji taasisi
haifuatwi tena.
Pesa inahubiriwa sana,kuliko Injili
yenyewe.
Nguvu za Mungu,hazipo tena kwa waliowengi.
 
catholic imeshaingia rasmi kwenye mfumo wa haya makanisa ya mfukoni (hawa wanaojiita makanisa ya kiroho) labda kwa sababu waumini wengi wa catholic wamekuwa wakichepukia kwenye hayo makanisa ya mifukoni.

ni kama inashindana nao. yaani wamejisahau kama wale wenzao wapo kibiashara na kimaslahi zaidi.

kuna mambo mengi wanaiga kutoka huko hata haya ya mambo ya michango lukuki ya kila uchao wameyatoa huko na ukikuta kamati tendaji ni oyaoya ndo waumini mtakoma.

Zamani michango mikubwa ilikuwa michache sana na sanasana ni zaka na sadaka tu lakini saivi kuna mchango lukuki tena mingine isiyo na kichwa na wala miguu. Jamaa wanabuni mradi tu hata haueleweki wakijua waumini watachangia tu.

Wanachojua ni kutafuta jina la mradi tu hata km ni simba na yanga na kuweka kisonjo pale mbele wanajua watu watatoa pesa tu.

kanisa lina miradi kibao tena inayojiendesha kibiashara na kupata faida lakini unakuta hela za kutoka kwenye miradi hazirudi kuwa mbegu kwa miradi mipya. badala yake mradi mpya lazima uchangiwe na waumini na ndo shida iko apo.
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Kumbe bado unaenda kanisani
 
Wapo ndugu yangu kuna huyu padre mwitaliano anaye hudumu Morogoro anaishi kifukara kwa uhalisia japo milioni milioni hizi kwake ni kama mia View attachment 3006791
Huyu si kama mpoto tu. Anatembea peku lakini anausafiri.
Kikubwa ni kuwa gharama za kuendesha kanisa zimeongezeka. Na siyo Katoriki tu. Makanisa mengi hasa yakiwa ktk ujenzi michango utatamani ukimbie. Lakini baada ya miaka kadhaa Hali inakuwa sawa. Sema shida ya katoriki ni kikusanya michango kipindi Cha huduma za kikanisa kama ndoa, kumunio, kipaimara ubatizo na mazishi yaaji unakuta kuna shida fulani ya pesa na wao wanapiga hapo hapo
 
Ha
catholic imeshaingia rasmi kwenye mfumo wa haya makanisa ya mfukoni (hawa wanaojiita makanisa ya kiroho) labda kwa sababu waumini wengi wa catholic wamekuwa wakichepukia kwenye hayo makanisa ya mifukoni.

ni kama inashindana nao. yaani wamejisahau kama wale wenzao wapo kibiashara na kimaslahi zaidi.

kuna mambo mengi wanaiga kutoka huko hata haya ya mambo ya michango lukuki ya kila uchao wameyatoa huko na ukikuta kamati tendaji ni oyaoya ndo waumini mtakoma.

Zamani michango mikubwa ilikuwa michache sana na sanasana ni zaka na sadaka tu lakini saivi kuna mchango lukuki tena mingine isiyo na kichwa na wala miguu. Jamaa wanabuni mradi tu hata haueleweki wakijua waumini watachangia tu.

Wanachojua ni kutafuta jina la mradi tu hata km ni simba na yanga na kuweka kisonjo pale mbele wanajua watu watatoa pesa tu.

kanisa lina miradi kibao tena inayojiendesha kibiashara na kupata faida lakini unakuta hela za kutoka kwenye miradi hazirudi kuwa mbegu kwa miradi mipya. badala yake mradi mpya lazima uchangiwe na waumini na ndo shida iko apo.
Hayo makanisa ya kiroho hayambani muumini kikubwa ni zaka. Ila katoriki wanakubana hata ktk shughuli nyingine za kijamii
 
Back
Top Bottom