Ni fukara kweli brother, 2004 niliwahi kumtembelea kwenye makazi yake pale nanenane Morogoro, ndani kwao hakuna hata sahani, chakula kinaliwa kwenye sufuria ya kupikia glass za maji hamna, vitanda na magodoro yao ni duni mno, hawana nguo ama kanzu ya pili, kanzu yake ine jaa viraka kila sehemu, ikichanika wanashona kwa sindano ya mkono.
Usafiri alio nao ni baiskeli ambayo pia ni duni mno, na hio baiskeli hupanda pale anapo wahi ibada kanisa kuu st Patrick, au kipindi redio ukweli.
Vinginevyo anatembea kwa miguu safari nyingi.
Redio ukweli ilikuwa yake kabla haijamilikiwa na jimbo.
So ni fukara kweli japo ana hudumia miradi yenye thamani kubwa.