Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Mkuu wanasema siku hizi hakuna Wafadhili.
 
We mtoa mada na wengine shauri yenu. Siku ya kifo chenu katekista atavuta kwanza fail lako la zaka kuchek kuwa ulikuwa unaipa michango vzur au la, kama liko vbaya padri hatokuja kukuzika! Utazikwa kama mbwaa!🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tukisema ukristo sio dini ya kweli muamini

Lets say waislamu wanaswali mara 5 kila siku je wangekua wanachangisha ivo wangekua matajiri kiasi gani?
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Dini ni Taasisi zilizoanzishwa ili kuwa exploit wana jumuiya
Unaenda kanisani unakuta kuna Sadaka karibia 10,ibada moja ,ukitoka hapo umekamuliwa hela yote 😄

Mtanyooka
 
Hapana siku hizi zipo mpaka katoliki.
Parking kwangu huku bunju wanaiita zaka ya kujipukutisha. Mtu mpaka unaogopa kwenda kusali haya sio mafundisho tuliyopewa, yanaibuka tu
Zamani tulikua tunawacheka walokole ila sasa wameyaleta na kwetu huku
Tunasali kanisa moja nini ndugu yangu, ila ya bunju imebtisha!
Zaka ya asilimia mia moja!!
Na majina yao Big may Big November.
 
Dini ni Taasisi zilizoanzishwa ili kuwa exploit wana jumuiya
Unaenda kanisani unakuta kuna Sadaka karibia 10,ibada moja ,ukitoka hapo umekamuliwa hela yote 😄

Mtanyooka
Dah halafu kuna kadi ya kumtmbulisha mkatoliki inaitwa kaakaa nayo kupata sh 3000,pia kuna ile mtoto anapopata kumunio eti analipa zaka 5000.je analipaje zaka mtoto wakati hatafuti hela anamapato gani?
 
We mtoa mada na wengine shauri yenu. Siku ya kifo chenu katekista atavuta kwanza fail lako la zaka kuchek kuwa ulikuwa unaipa michango vzur au la, kama liko vbaya padri hatokuja kukuzika! Utazikwa kama mbwaa!🤣🤣🤣🤣🤣
Sawa tu.kuzikwa ni kuzikwa tu.
 
Anaishi kifukara ila sio fukara.....ni kama ndani una msosi ila ukaamua kushinda njaa
Na njaa ikukubana sana ,unaenda ndani unastua tumbo kidogo! Sasa mwenzangu na mimi hata katonge huko ndani huna,ikibana utastua na nini!? Ufukara usikie tu kwa mwenzio na usiombe ukukute utashaa!!
 
🤣🤣🤣 kuna watu wanasema katekista na padre hawatakuja kuzika Kwa kuwa hutoi michango ,niulize tu Kwa miaka yako yote binadamu yupi aliachwa ndani,chumbani bila kuzikwa???Kuna mwingine anasema hautazikwa vizuri 🤣🤣🤣 nilipita makaburi ya kinondoni nikitafakariiiiiiiiiiii nikajisemea moyoni hivi katika hawa woooote Nani alizikwa vizuri!!!sikupata Jibu kifupi kuzikwa vizuri ,vibaya it doesn't matter
 
Michango ya kanisa ukitoa kwa moyo kadiri uwezavyo bila manung'uniko kuna baraka nyingi sana.
Ningeweza kutoa shuhuda nyingi hapa, ila si sawia kadiri ya desturi zetu wakatoliki.
Sadaka ya kweli ni ile inayouma, japo mtoaji hupaswi kulalama njia nzima
 
Na sadaka ya kweli hailazimishwi kwa kufokeana
 
Solution ni kuacha kutoaa hiyo michango tu, kwani umelazimishwa?

Kingine, mapadre waache na wakome kutoa vitisho vya kishamba kishamba Kwa waumini,

Matangazo ni mengi na marefu ambayo mengi ni useless,

Mahubiri yawe mafupi yenye kumjenga mtu kiimani na kiroho, sio kila mahubiri lazima waongelee kuhusu hela,

Tusikubali mambo ya kijinga kijinga kanisani, padre yupo kwàajili ya waumini, sio waumini kwàajili ya padre.

Kama hutaki kutoa huduma toka na upote parokiani kwetu,
umejileta wewe mwenyewe parokiani kwetu,ni wajibu wako kutupatia huduma.

Sisi Waumini kama tukipendezwa tunaweza tukachanga chochote kitu, lakini sio lazima.
 
Back
Top Bottom