Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Wenzako huwa wanahama,kama unaona kuna fursa ya kuiweka nafsi yako rehani tafuta pa kujishikisha kama ni kwa nabii mtume sijui malkia ni wewe au hama ng’ambo ya pili huko upate na fursa ya kuongeza wake.
 
Uje penda kuzungumzia mambo ya Parokia yako na Paroko wako na viongozi wako uliowachagua.

Kila mtu ana parokia yake na jimbo lake. Hivyo jambo likifanyika kwenye parokia au kigango chako usianze kulihusisha kanisa zima Katoliki.

Kila Jimbo, Parokia au kigango kila utaratibu wake na uongozi wake.

Na unao Uhuru kamili wa kutoa maoni, mapendekezo, ushauri lipi baya halifai au lipi jema liendelee kupitia jumuiya yako, mikutano ya Kigango au Parokia yako ambapo wajumbe wa mikutano hiyo wanatokana na jumuiya.

Ila kama huwa husali jumuiya au kushiriki masuala yote ya kanisa unavizia matukio tuu, ubatizo, kipaimara, komunyo au ndoa na misiba hakika wacha mnyooshwee kisawa sawa.
Haya mambo usizungumze tu kama muumini wa Mwamposa au nabii wanaoota kama uyoga siku hizi.

Katoliki ni moja, kanisa la kimapokeo. Ukisema ni Parokia yake n.k unakuwa unamaanisha?
- Ina maana kwenye umri ulionao umekuwa kwenye Parokia moja tu?

Umeshasikia kuwa Chota baraka kwa kuchangia Radio Tumaini, Radio Maria etc?
  • Mipango ya ujenzi wa Kanisa Gezaulole, kuna haja ya kuwakamua waumini? Sadaka, zaka, miradi ya shule, kumbi na hospitali za Jimbo kama la DSM inafanya kazi gani?
  • Unajua Parokiani huko, watu wanakamuliwa kuanzia ngazi ya Familia, Jumuiya, Kanda hadi Parokia, kisha wanaanza tena kwenye vyama vya kitume, na ukiangalia michango ni ile ile ila majina tofauti?
  • Unazungumzia viongozi waliochaguliwa? Fikiria sasa hao viongozi ndo wawe mfano wa wewe, unadhani nini kitabadilika?

Unayafahamu maisha ya kifahari wanayoishi hawa watawa wetu walioapa kutoa maisha yao sadaka?

Katoliki inachochora kwenye mipesa!
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamuwa waumini michango hadi wanachukia dini.Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto,halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda.Michango ya ujenzi inautaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Changia Kanisa lako Comrade. Kanisa litajengwa na sisi wenyewe.
 
Sie wengine tumeishia kwenda kusali tu , mengine mbele kwa mbele,,,ukisema ujifanye muumini mzuri unaanza kukaangwa tokea kwenye jumuiya
Nimehesabu bahasha nilizonazo toka mwaka jana zinafika 15. Hio ni michango ambayo sijailipia. Hii dini hapana kama ni huko kuogopwa kutengwa tu basi wanitenge nikifa.
 
Nimehesabu bahasha nilizonazo toka mwaka jana zinafika 15. Hio ni michango ambayo sijailipia. Hii dini hapana kama ni huko kuogopwa kutengwa tu basi wanitenge nikifa.
Hahah kikubwa maisha yako unaishi vipi na wanaokuzunguka baas ,ukitaka mengi utaishia kuishi kwa woga tu,,,,mie nishakubaliana na hali tutengwe tu
 
Hizi dini biashara tu sikuhz,

Zamani watumishi wa Mungu walikua wanaishi kifukara lkn sikuhizi nao wanataka kwenda na trends za maisha ndo maana michango juu
Wapo ndugu yangu kuna huyu padre mwitaliano anaye hudumu Morogoro anaishi kifukara kwa uhalisia japo milioni milioni hizi kwake ni kama mia
Screenshot_20240602-185751_Google Go.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20240602-185751_Google Go.jpg
    Screenshot_20240602-185751_Google Go.jpg
    291.4 KB · Views: 8
Wapo ndugu yangu kuna huyu padre mwitaliano anaye hudumu Morogoro anaishi kifukara kwa uhalisia japo milioni milioni hizi kwake ni kama mia View attachment 3006791
Usanii tu huyo si ndo yule mwenye ile shule wanamuita faza pekupeku,,,,,,anaishije kifukara wakati ana shirika linamuhudumia,,,,mafukara wapo ila sio hawa
 
Back
Top Bottom