Siasa za Tanzania ziishie Tanzania zisivuke mipaka. Chuki za serikali kwa Chadema zisiliingize Kanisa. Kanisa ni kubwa kuliko chama chochote cha siasa nchini, kiwe CCM au CHADEMA kimuundo, kiuchumi, kiuwezo, idadi ya wanachama. Lipo dunia nzima.
Ili Kanisa lijiendeshe duniani kiufasaha limeundwa na mashirika mengi mojawapo ni Shirika la 'Jesuit'.
JESUIT ni shirika la kijasusi la Kanisa Katoliki ni idara ya ulinzi na usalama ya kanisa Katoliki ni Polisi na 'TISS' ya Kanisa.
Hili shirika lipo hadi Tanzania. Linaundwa na makada wasomi kwenye fani zote, wapo madaktari, mainjinia, polisi, walimu, wanajeshi, wahasibu ina pia viongozi wakuu kwenye serikali nyingi duniani, lina watu wake kwenye idara nyeti za serikali, ina shule zake, vyuo vikuu vyake, na hospitali zake.
Uwezo wa shirika hili ni mkubwa kiasi kwamba linaweza kumuweka au kumuondoa kiongozi yeyote wa serikali hata Rais.
Usalama wa Makardinali, Mapadri, Maaskofu, Maparoko upo chini ya shirika hili na lina ripoti moja kwa moja Vatican. Padri au Askofu yeyote akidhuliwa Jesuits wa eneo hilo wanakuwa answerable.
Usalama wa Padri Kitima upo chini ya shirika hili, kumshambulia Padri Kitima ni kulishambulia Kanisa sio sawa na kumshambulia Kibao wa Chadema.
Hadi sasa taarifa za kushambuliwa kwake zipo Vatican zinafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa, uzuri wa shirika hili huwa halikurupuki, halina papara hufanya kazi kwa usiri mkubwa, ripoti zake zinapotoka hutoka na matokeo chanya kwa Kanisa lakini zinaweza ziwe hasi kwa waliohusika.
Ex Jusuit.
Naomba Mods msiunganishe uzi huu una maudhui tofauti ya kuelimisha jamii.