Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia leo ambapo watu waliovamia wamevunja mlango na kuingia ndani kisha kuharibu vitu vitakatifu vikiwemo mavazi ya misa na kuvunja misalaba.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na upepelezi wa tukio hilo unaendelea.


=====
Askofu Flavian Kassala
Wapendwa, nawatangazia kuwa jimbo katoliki Geita tumepatwa mkasa mkubwa ambapo mtu mmoja amevamia kanisa kuu na kuvunja mlango mkuu na kisha kuanza kuharibu vitu vitakatifu, vikiwemo Tabernakulo na Ekaristi. Ni kufuru ya matakatifu.

Kavunja misalaba na mavazi ya misa. Nawaombeni mtumie vyombo vyenu vya habari ktk redio na television muupashe habari umma kuwa kitendo cha kudhalilisha imani yetu kimefanyika na tunakikemea na kukilaumu kwani kukaa kimya ni kama kuonesha hatuthamini imani yetu. Kwa wenye redio au tv, atakayehitaji "Audio" ya baba askofu, nitamtumia ili airushe na tuunganishe nguvu ya vyombo vya habari vya kanisa kukemea udhalimu dhidi ya imani katoliki.

Matukio ya uharibifu wa kanisa kuu la kiaskofu jimbo la Geita usiku wa kuamkia Jumapili trh 26 February 2023. Tukio limeripotiwa saa nane usiku. Uharibifu na kufuru zilizotokea ni kubwa sana. Mhusika amekamatwa. Mungu azidi kutulinda.
View attachment 2530803
Hii mbungi ingepigwa msikitini sipati picha n'titi wake
 
Wahuni wamevunja mguu wa Brian Deacon. Sijui wataliomba hivyo hivyo sanamu lake likiwa lina ulemavu au wataliunga gundi kwenye ibada zao.
 
Leta link wewe,umejipa kazi mwenyewe na sasa unabwata bwata nini tena [emoji2957][emoji2957]

Popo wenu keshawaruhusu wanaume kuolewa haya wakumbatie Mapadri wako

 
Popo wenu keshawaruhusu wanaume kuolewa haya wakumbatie Mapadri wako

Eheee endelea [emoji847][emoji847][emoji847]
 
Narudia tena kuandika hakuna mkristo wa dhehebu lolote anayeweza kuingia kwenye kanisa la wengine na kufanya uharibifu.

Kama kuna tofauti imetokea miongoni mwa viongozi kwa viongozi, viongozi kwa waumini au waumini kwa waumini hakuna mshirika atakayefikia uamuzi wa kwenda kuingia kanisani kufanya uharibifu huo. Hata kama ni vibaka, ni kibaka gani huyo asiye na hofu na Mungu?

Huyo kibaka au mwizi na jambazi amekulia wapi kiasi cha kukosa hata mafundisho ya watoto ya shule ya jumapili? Kwanza kanisa ni mahali patakatifu na ni nyumba ya kumuabudu Mungu.

Hata wavuta bangi na walevi wanaheshimu nyumba za kuabudia
Naunga mkono hoja, hao labda wametumwa na wamelipwa
 
Back
Top Bottom