Kanisa la Segerea latupiwa 'bomu' la mafuta, laungua; KKKT Kijitonyama kwaibuka hofu!

Kanisa la Segerea latupiwa 'bomu' la mafuta, laungua; KKKT Kijitonyama kwaibuka hofu!

Status
Not open for further replies.
Hii ni hatari kwa kweli,haya mambo sijui yataendelea hadi lini.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Habari ya ITV saa 2 usiku, Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania tawi la Tabata lilipatwa na majanga hayo jana jumamosi. Watu wasiojulikana walikuja na mafuta ya taa na kuwasha moto eneo la madhabahu na baadaye gari lililokuwa limeegeshwa nje. Hata hivyo jitihada za kuuzima zilifanikiwa na kuokoa kanisa na gari lisiteketee kwa moto. Hii ndiyo Tanzania tuliyonayo sasa.
 
Matukio ya mabomu kurushwa kanisani yanaendelea nchini, kufuatia kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Segerea, jijini Dar es Salaam kunusurika kuteketea kwa moto uliotokana na milipuko ya mabomu usiku wa kuamkia jana.

source:nipashe
 
Kuna kitu kimewekwa kwenye jenereta la kanisa na jengo la kitega uchumi la kkkt kijitonyama kilichosadikiwa ni bomu, bomu hilo lilikuwa limeunganishwa na kamba iliyopita ng'ambo ya pili lakini polisi wamewahi na kuja kulitegua na kuondoka nalo, polisi wamegoma kutoa maelezo kama kweli ni bomu au la.

Source mimi mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama Polisi hawajathibitisha mbona wewe waandika ni bomu mkuu?
 
Kwa sababu wamegoma kutoa maelezo na wananchi tumehisi hivyo. Ndio maana nimeandika bomu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Limeunganishwa na kamba,au waya?.isijekuwa umeona mtego wa panya mkuu.
 
Kuna kitu kimewekwa kwenye jenereta la kanisa na jengo la kitega uchumi la kkkt kijitonyama kilichosadikiwa ni bomu, bomu hilo lilikuwa limeunganishwa na kamba iliyopita ng'ambo ya pili lakini polisi wamewahi na kuja kulitegua na kuondoka nalo, polisi wamegoma kutoa maelezo kama kweli ni bomu au la.

Source mimi mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Sie tulidhani katoliki pekee ndio wasanii kumbe hata kkkt upo. Mbowe ameshatoa ule ushahidi wa Arusha
 
Limeunganishwa na ile kamba ya kushonea viatu ila tatizo limekuja hyo kamba ilikuwa imetupwa kupitia nyaya za umeme kwa juu na tena ilikotua ni kwenye jenereta la kanisa na jengo la kitega uchumi,halafu hicho kitu chenyewe kilikuwa na taa inawaka (dim light)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hofu imetanda kanisa la Kkkt usharika wa kijitonyama Dar es salaa... Hali ni tete kweli kweli..
Kimerushwa kitu kikiwa ndani ya box karibu na trasfoma ya umeme iliyoko kanisani hapo..
Polis wamefika na kuchukua boxi hilo na kuondoka nalo

waandishi wazuiwa kupiga picha!
 
ITV nao wamesema kuna kitu kimerushwa kanisani kkt,ilapolisi wamegoma kusema kama ni bomu au la.
 
Hofu imetanda kanisa la Kkkt usharika wa kijitonyama Dar es salaa... Hali ni tete kweli kweli..
Kimerushwa kitu kikiwa ndani ya box karibu na trasfoma ya umeme iliyoko kanisani hapo..
Polis wamefika na kuchukua boxi hilo na kuondoka nalo

waandishi wazuiwa kupiga picha!
Kimenuka tena..
 
Kwa sababu wamegoma kutoa maelezo na wananchi tumehisi hivyo. Ndio maana nimeandika bomu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Hadi sasa naona hakuna taarifa kamili inayoeleweka...anyways asante kwa taarifa.
 
[h=3]KUHUSU BOMU LILILOTENGWA JIONI HII KANISANI KIJITONYAMA,POLISI WAMECHUKUA HATUA HII[/h]
[h=5]Hofu kubwa imewapata waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Kijitonyama, baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kurushwa kanisa hapo. Polisi wafika kanisa hapo na kuondoka na kitu hicho.
HABARI HII NI TOFAUTI NA ILE YA JAMA
ITV[/h]
1005225_639157012775882_890374929_n.jpg
 
Hii amani tuliyonayo tusipoilinda sisi wenyewe hatutopata kamwe wa kututafutia tena
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom