Kanisa la Waadventist Wasabato limchukulie hatua za kidhamu mshiriki wao Mafwele

Kanisa la Waadventist Wasabato limchukulie hatua za kidhamu mshiriki wao Mafwele

kwa taarifa yako, Yesu aliwahubiria, ila hakuambatana nao, aliwaponya na kuwasamehe dhambi, ila hakuwajumuisha kwenye thenashara. Hata zakayo alimwendea na kumpelekea habari njema tu, ila hakuungana naye kwenye maisha yake ya uthurumati. wafuasi wa shetani na wafuasi walioamua kumfuata Mungu haviwezi kukaa pamoja hata siku moja. na Biblia ndivyo inavyosema.
iskariote hakuwa miongoni mwa thenashara?.
 
Kwa ushahidi upi walionao kama kanisa hadi wamchukulie hatua?

Lady jaydee alionekana hadharani akiimba miziki ya kidunia ushahidi wa wazi
Surat Al-Imran (3:19), ambapo Mwenyezi Mungu anasema:"Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu..

."Hii inaonyesha kuwa, kwa mujibu wa Qur'an, Uislamu ni dini ya haki inayokubalika mbele ya Mwenyezi Mungu, ikiwa na maana ya kujisalimisha kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Uislamu unatokana na neno la Kiarabu "Islam", linalomaanisha "kujisalimisha" au "kujitoa kwa Mwenyezi Mungu".
 
Ni wazi kuwa huyu ndugu Mafwele ni mshiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato.

Kwakuwa mwongozo wao wa kanisa unasema kuwa kuvunja moja ya amri 10 za Mungu ni kosa linaloweza pelekea adhabu dhidi yako, basi naomba kanisa limhoji ndugu Mafwele na ashike Biblia mbele ya baraza la kanisa aape kama kweli hahusiki na tuhuma zinazotajwa dhidi yake.

Ikiwa anahusika basi kanisa limwondoe katika kitabu cha ushirika kama mwongozo unavyosema na kumpa muda wa kujirekebisha na akijirekebisha abatizwe tena na kuwa kiumbe kipya.

Aidha waumini wake wengine ndugu Lengai Ole Sabaya, Boniphace Jacob, Cyprian Musiba, Mzee Wassira, Dr. Ryoba na wengine wachukuliwe hatua kwa usawa kama alivyo chukuliwa hatua Lady Jaydee kipindi alivyo amua kujihusisha na muziki wa kidunia.

Kanisa la Waadventista Wasabato limepiga marufuku waumini wake kujihusisha na mambo ya siasa, watajwa hapo juu na wengine ambao sijawataja wamehusika mojakwamoja katika siasa.
Mbona wewe uajihusisha. Unaelewa siasa ni maisha ya kujitawala, usipotaka kama huna wadhifa serikalini basi jua utapngiwa maisha yako na hao wanasiasa
 
Penye kusema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Maana itaendana kweli na ile kauli aliyosisitiza na kutuasa Yesu mwenyewe inayosema:
Lk 13:24; Yn 10:7,9Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache..???
Mkuu; mbona hayo ni mambo (Mafundisho mawili tofauti) japokuwa yana chimbuko sawa? Habari za mlango mwembamba na njia nyembamba ref. Mathayo 7: 13-14: Lakini Sauti ya wengi ref. Math. 18: 20 na ni kwa wale wanaoliita Jina lake ........... Ila vyote ni kutoka kwenye kitabu cha Biblia; La kwanza likionesha kazi ya kuupata ufalme wa mbingu na ugumu uliopo, na la pili likionesha umuhimu wa maombi au sala za pamoja (Jumuiya) na uwezo wa sala au maombi ya namna hiyo.
 
Hizi chuki ni mbaya. Kwamba hao uliowaita wa sabato ndio waovu kuliko waumini wa madhehebu mengine. Ni mwongozo upi wa kanisa la wasdventista wa sabato unaokataza muumini mmoja mmoja kuwa mwanasiasa? Ninachokujukisha ni kwamba kanisa linachokataza ni kanisa lenyewe kama taasisi kujihusisha na masuala ya kisiasa. Huhawahi kusikia kanisa kujifungamanisha na siasa. Mifano ya madhara ya kanisa kujifangamanisha na siasa yamelikumba kanisa la rc ambapo limejikuta kuhusishwa na mauaji katika vipindi na mahali duniani mfano Rwanda, ulaya, Canada nk.
 
Nanukuu: "Kwa ushahidi upi walionao kama kanisa hadi wamchukulie hatua?"
Kumbuka Sauti ya wengi ni sauti ya Muumba wetu i.e. Mungu.
Lakini pia zingatia kwamba Mungu ndiye aonaye sirini. Mungu anajua yote - Hahitaji ushahidi. Kwa kuwa huyo ndg. aliyetajwa ni mtu muumini katika Imani yao; basi akishika kitabu kitakatifu, yani Bibilia, na kuapa mbele ya kanisa, kama mtoa mada alivyosema "kanisa limhoji ndugu Mafwele na ashike Biblia mbele ya baraza la kanisa aape kama kweli hahusiki na tuhuma zinazotajwa dhidi yake" , itakuwa bora kwake na ndipo atajua kwamba Mungu hadhihakiwi (Biblia;

Gal 6:7-9 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna ...) 🙏

Usimshirikishe Mungu kwenye mambo yakufikirika mkuu
 
Ni wazi kuwa huyu ndugu Mafwele ni mshiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato.

Kwakuwa mwongozo wao wa kanisa unasema kuwa kuvunja moja ya amri 10 za Mungu ni kosa linaloweza pelekea adhabu dhidi yako, basi naomba kanisa limhoji ndugu Mafwele na ashike Biblia mbele ya baraza la kanisa aape kama kweli hahusiki na tuhuma zinazotajwa dhidi yake.

Ikiwa anahusika basi kanisa limwondoe katika kitabu cha ushirika kama mwongozo unavyosema na kumpa muda wa kujirekebisha na akijirekebisha abatizwe tena na kuwa kiumbe kipya.

Aidha waumini wake wengine ndugu Lengai Ole Sabaya, Boniphace Jacob, Cyprian Musiba, Mzee Wassira, Dr. Ryoba na wengine wachukuliwe hatua kwa usawa kama alivyo chukuliwa hatua Lady Jaydee kipindi alivyo amua kujihusisha na muziki wa kidunia.

Kanisa la Waadventista Wasabato limepiga marufuku waumini wake kujihusisha na mambo ya siasa, watajwa hapo juu na wengine ambao sijawataja wamehusika mojakwamoja katika siasa.
Ndio maana dini hazina maana kwenye ulimwengu huu. Sababu zimekuwa kichaka.
Mungu ni mmoja, dini nyingi za nini?
 
Usimshirikishe Mungu kwenye mambo yakufikirika mkuu
Mimi Nimenukuu Neno lake. Labda iwe wewe huamini katika yaliyomo kwenye kitabu kiitwacho Biblia.
Ni kweli mambo yanayozungumziwa ni ya kufikirika i.e. hakuna mtu mwenye ushahidi kamili.
 
Back
Top Bottom