Kanisa limepiga marufuku wanasiasa kusalimia kanisani, wamekosea sana

Ifike mahali Kanisa na Watumishi wa Mungu waheshimiwe.
 
Mambo ya kichanganya dini na siasa yameleta matatizo sana Ulaya.

The very birth of the nation state, after The Thirty Years War of 1618 - 1648, was the beginning of an exercise in restrain from mixing religion and politics.

Walioanza kuwa na haya mabunge, mahakama na serikali hizi za kisasa, waliona matatizo ya kuchanganya dini na siasa. Kuchanganya dini na siasa kumeleta vita nyingi sana za kidini from the Crusades to the recent American wars to some extent.

First amendment ya katiba ya US imetenganisha siasa na dini. Wamarekani wamekataza bunge lao kutunga sheria kuhusu kuanzisha dini au uhuru wa kuabudu kidini.

Separation of religion and state inasaidia kuifanya serikali isiingilie dini. Tungekuwa tunaiheshimu, huu uhuni anaofanyiwa Gwajima usingewezekana.

Inasaidia nchi kutokuwa na dini inayopendelewa na serikali, na kuweka religious pluralism.Inasaidia kuweka uhuru wa mtu binafsi kuchagua dini bila kuingiliwa na serikali. Inasaidia kufanya dini zisitumiwe na wanasiasa kwa manufaa yao ya kisiasa. Sasa hivi tuna ujinga mwingi sana wa wanasiasa kutumia dini kisiasa, tungekuwa tunaheshimu separation of religion and state, tungetambua michezo michafu hii.
 
Uko sahihi uncle kwa 100%. Dini, kabila, kanda na sasa jinsia ya mgombea vimegeuka kuwa kimbilio kwa watu waliofilisika kisaisa au wale wenye ajenda zaa nyuma za pazia. Nyerere alikuwa akipambana na ukabila na udini visiwe vigezo vya kupata uongozi lakini awamu ya tano tulirudi nyuma kwenye hilo kwa hatua nyingi sana nyuma. Hata wewe sema ukweli wako kutoka moyoni, yule Mpina aliweza vipi kuwa na sifa ya kuwa waziri wa nchi hii?
 
Nyerere alikuwa anasali St. Peters Oysterbay, si kila Jumapili, kila siku. Alivyokuwa Dar alikuwa anasali kila siku asubuhi.

Hakuna hata siku moja yuliyoona Nyerere kapanda mbele pale St. Peters kutoa neno.

Mkapa alivyokuwa rais alisali St. Immaculata Upanga.

Hakuna hata siku moja aliyopanda mbele kutoa neno kama rais.

Hawa marais wasomi walielewa Separation of Religion and State.
 
Utafiti wangu mdogo unanionyesha kuwa chanzo (genesis) ya wanasiasa kuhudhuria na kusimama mbele ya kanisa kusema neno ni kualikwa na wanakanisa wenyewe. Hapo awali Walifanya hivyo kwa maslahi ya kanisa, hasa walipokuwa wanataka kitu kutoka kwa wanasiasa (serikali). Hii ilitumika kama leverage ya kupata kitu kutoka kwa wafanya maamuzi kwenye jambo lao kama vile kutwaa ardhi, kupata misamaha ya kodi, kubadilisha sera, kubadilisha maamuzi, kupata michango, nk. Kifupi ilikuwa njia ya kuwavuta/kuwasogeza/kuwaingiza kingi wafanya maamuzi wawe karibu yao kwa manufaa yao.

Hasa pale ambapo mtawala sio wa dini yao au dhehebu lao watafanya kila namna mfanyamaamuzi huyo awe karibu yao. Hata kama mwanasiasa huyo ni muislamu ataandaliwa mazingira ya kumvuta karibu kanisani kama vile kusimika viongozi, kufungua kanisa, kuadhimisha jubelee, nk ilimradi tu waweze kukutana nae karibu wamuombe jambo lenye manufaa kwa kanisa lao.

Juzi umeona Mwamposa alimwalika Rais aende akafungue mahema yao, lakini kama utaangalia vizuri sababu kuu ya kumwalika pale ilikuwa awape eneo la Tanganyika packers liwe eneo lao la kudumu. Huu ni upuzi kabisa kudai eneo la umma wenye dini na wasio na dini liwe lako.
 
Ahsante sana mkuu
 
Wakipewa kusalimia wanaongea sana mambo ya siasa na kuanza kuwapangia maombi Gani waombe, yaani mwanasiasa anakuja kanisani kuwaambia Kanisa muombe sana amani...🙇, kupangiwa na wanasiasa Kanisa halitaki....mara utasikia muombee rais mara liombee taifa
...Kanisa halipangiwi na linajua Cha kuomba
 
Kuombea taifa na watawala ni agizo ambalo limo ndani ya biblia zenu. Bila amani hata kazi ya Mungu hawezi kufanyika. Huwezi kwenda kuhubiri mahali ambako kunarindima mabomu.
 
Every opinion on a subjective matter has value, but it doesn’t alter the underlying reality.
 
Kuombea taifa na watawala ni agizo ambalo limo ndani ya biblia zenu. Bila amani hata kazi ya Mungu hawezi kufanyika. Huwezi kwenda kuhubiri mahali ambako kunarindima mabomu.
Sasa mwanasiasa hawezi kuja Makanisani kutuambia, sisi tunaongozwa na roho Cha kufanya 🤣....automatically mwanasiasa ni mtu mwenye dhambi yaani maisha yake yote asilimia kubwa anaishi maisha ya dhambi anatakiwa akienda Makanisani awaombe wamuongoze sala ya toba tu na sio kuwapangia Cha kufanya 😄😄
 
ile sadaka mnayokusanya inatoka wapi? serikali lazima itengeneze mazingira ya watu kuwa na kipato, kazi hiyo inahitaji amani na utulivu na mipango madhubuti ya kutengeneza ajira na fursa. Kuombea taifa, watawala na amani sio hiari ni agizo kutoka kwa Mungu.
 
Sadaka inatoka kwa binadamu kwenda kwa Mungu wake, na hii inatolewa kwa Imani, anatoa akiwa anaelewa anatoa kwasababu Gani, wanasiasa sio wa kuwachekea Makanisani😀🤣
 
Halijapiga vita wapinzani lakini

Limepiga vita ccm tu
 

Kila mtu apambane na hali yake. Ila altare ya Bwana Yesu, haitaki kunajisiwa


View: https://www.youtube.com/watch?v=EtUQxJmZ5rY&list=RDEtUQxJmZ5rY&start_radio=1
 
Sadaka inatoka kwa binadamu kwenda kwa Mungu wake, na hii inatolewa kwa Imani, anatoa akiwa anaelewa anatoa kwasababu Gani, wanasiasa sio wa kuwachekea Makanisani😀🤣
Mungu hahitaji sadaka, ana Kila kitu. Wala hatambui pesa mlizojitengenezea.
 
Nimefurahi maana wanaingiza kampeni na siasa Tena chafu.... hawa Mapadre Wana akili nyingi WENGI ni PhD Og, si kama ile ilompoteza Ben sanane,



Wakitaka ujumbe ufikie waumini wawaambie makasisi wao watawaambia KONDOO wao😅😅😅😅...
Maana mwisho wa siku kanisa litsunganisha kwenye UTEKAJI
 
Sadaka sio pesa, elewa kwanza hapa
Hungu hajui pesa zenu Wala hana meno Wala mdomo, haendi chooni kwakuwa hali chakula, hivyo Padre ndiye mwenye meno ya Mungu anakula pesa, matoleo, sadaka, fungu la kumi, michango, nk. Wanakusanya hata misibani, kwenye sherehe, kwa wagonjwa, kwa maskini na kwa matajiri. Wajinga ndio wanaoangamizwa kwa kukosa maarifa. Amkeni amkeni amkeni bhana.

Kama watu wote ni watoto wa Mungu basi Kila mtu anapaswa kumjua baba yake yeye mwenyewe Bure kabisa. Haiwezekani nyumbani mtoto mmoja awahadithie watoto wenzake habari za baba yao ambae wanaishi nae humohumo nyumbani. Yaani dada Yako akwambie baba hanywi Pepsi, hali mlenda na ni mkali sana wakati Kila mtu anamfahamu, anamsikia tangu utotoni. Mnaibiwa, baba yetu sote kwanini wewe umjue zaidi kuliko sisi kama sio ujinga wa watoto wengine. Mtoto mmoja Kila jumapili anawaambia watoto wenzake baba kasema, baba kaagiza, baba amekasirika, baba anataka pesa, mbuzi, nk wakati wote tulikuwa nae muda wote, yeye ameambiwa muda Gani wakati wote tulilala, tulikuwa chooni, tulikuwa tunaoga, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…