Mkuu,naomba unifafanulie hapa nielewe,sijui shida kizungu au vip?
Unamanisha nini?
Mambo yetu ya uongozi, nchi, mahakama, bunge, serikali, demokrasia, etc, tumeiga.
Na kuiga si lazima liwe jambo baya. Hatuhitaji kuanza upya kila kitu, hususan kama kimefanyika vizuri kwingine.
Na huko tulikoiga ambapo walianza haya mambo zamani kabla yetu, walipitia matatizo mengi sana, matatizo ambayo kwa sababu wao waliyapitia, sisi tunaweza kujifunza tu kutoka kwao tusiyapitie kama wao.
Mtu mjanja mara zote hujifunza kutokana na matatizo na historia ya wengine ili yeye asiyapitie, apate somo moja kwa moja.
Wale ambao tumejifunza kwao waliuana sana, walichinjana sana, walipigana vita sana, kwa sababu ya kuchanganya dini na siasa.
Mpaka wazungu wengine wakakimbia Ulaya wakaenda kuanzisha makazi Marekani kwa sababu walibaguliwa kidini Ulaya. Walikuwa wanataka kuishi kwa uhuru wao.
Mpaka Ulaya wakapigana kitu kinaitwa "The Thirty Years War" kwa Kiswahili "Vita Vya Miaka Thelathini" ya mwaka 1618 mpaka 1648. Sababu moja kubwa ya vita hizi ilikuwa ni kuchanganya siasa na dini.
Baada ya "The Thirty Years War" walikubaliana kimkataba kutopigana vita, kila mtu akae kwake, na wajitawale kiserikali, na watweganishe dini na siasa. Hapa ndipo dhana ya nchi kama tunavyoijua leo ikaanza, kwenye mkataba ulioitwa "The Peace of Westphalia" wa mwaka 1648. Takriban miaka 377 iliyopita wenzetu walijifunza kwamba kuchanganya dini na siasa kunatengeneza sumu mbaya inayosababisha vita kubwa sana. Wakatenganisha dini na siasa.
Sasa na sisi kimsingi tumejifunza hilo. Ndiyo maana tuna katiba inayosema nchi yetu haina dini. Lakini dini ina nguvu sana tunashindwa kutekeleza Separation of State and Religion. Ni viongozi wanafalsafa tu kama Nyerere waliosoma, kuelewa na ku internalize hii historia ndio waliweza kujizuia wao wenyewe kusimama makanisani kutoa hotuba za kisiasa.
Juzi Samia kaenda kufungua kanisa la Mwamposa, kuna Babu wa Kizanzibari alikuwa analia anasema Samia kaombewa na Mwamposa kwa jina la Yesu kaondolewa kwenye Uislamu kawa Mkristo.
Hata kabla ya hapo Samia alivyokuwa anagawa sana hela makanisani, Wazanzibari kwenye misikiti walikuwa wanamsema anawapendelea sana Wakristo anawapa hela sana Wakristo, Waislamu hawamuoni. Tayari rais kujiingiza makanisani inaleta mgawanyiko kwa wananchi.
Wasio na dini naowanaona vibaya pesa zao za kodi zinatumika kwenye nyumba za dini.
Ndiyo maana wenzetu waliona matatizo haya mapema wakaweka hii Separation of State and Religion.
Nyerere alikuwa anasali pale St. Peters Oysterbay kila siku akiwa Dar. Si kila Jumapili, kila siku. Lakini hakwenda mbele pale kusema neno hata siku moja. Ilikuwa mwiko. Mkapa naye vilevile alikiwa anasali St. Immaculata hapa Upanga karibu na Selander Bridge. Hakuenda mbele kutoa neno hata siku moja.
Huu ujinga kwa Wakristo umeanza na Magufuli tu. I am not sure about Mwinyi and Kikwete.