Kanisa wanaposali Waumini wa Gwajima Lavunjwa

Ndugu zangu Watanzania,

Soma hapo 👉Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) lililopo Ubungo Kibo Jijini Dar es salaam ambalo kwa Wiki tatu limetumiwa na Waumini wa KKAM na Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima kufanya Ibada, limevunjwa na kubomolewa kabisa ambapo Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amefika katika eneo hilo asubuhi hii leo July 13,2025 na kujionea pakiwa pamevunjwa kabisa na hakuna Muumini yoyote huku Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi.

Itakumbukwa Jumapili iliyopita Jeshi la Polisi liliimairisha ulinzi pia katika eneo kubwa la Ubungo ikiwemo kuzingira Kanisa hilo wakati Waumini wakifanya Ibada hatua ambayo ilijiri baada ya Jeshi hilo kuta onyo kwa kundi la Watu ambao walikuwa wakitokea KKAM na mabango baada ya ibada wakidai haki yao ya kuabudu kufuatia kufungwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima hivyo kupelekea Waumini kutawanywa kwa mabomu kwa Wiki mbili mfululizo huku Waumini wengine wakikamatwa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la KKAM.

Waumini kwa Kanisa la Gwajima kwa zaidi ya Wiki mbili walijumuika na Waumini wa KKAM Usharika wa Ubungo Kibo ambalo ni Kanisa rafiki na lililo jirani na Kanisa lao lililofungwa ambapo kwenye Ibada ya ya Jumapili iliyopita miongoni mwa waliohudhuria ni Naibu Katibu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima Akofu Maximilian Machumu Kadutu maarufu Askofu Mwanamapinduzi ambaye aliwasihi Waumini kutobeba mabango wala kufanya vurugu huku akiwaomba Polisi kutorusha mabovu kauli ambayo ilizaa matunda na Ibada ikakamilika kukiwa na usalama Waumini wakarejea makwao bila kupigwa na Polisi.

Bado haijajulikana sababu ya Kanisa kuvunjwa na aliyevunja lakini Majirani wa eneo hilo wanasema limevunjwa juzi Ijumaa.. tunaendelea kufuatilia kujua wanapofanyia Ibada Waumini wa Gwajima na wa KKM na tutakujuza >> youtu.be/PhTgm6FGIbg?si…View attachment 3404279
Unapataje ujasiri wa kuongea habari mbofu mbofu tena ulizokuwa na maslahi nazo,za kuwaumiza waenzio Wadanganyika tena waumini wenzio?
 
Huyu Lucas mwashambwa sio jina lake halisi. Na wala sio mtu wa mbeya
Jina lake halisi ni Abubakar Karim na ni mzawa wa Unguja chakechake.

You know the rest.
Naona unajitekenya na kujichekesha Mwenyewe kama mlevi wa gongo
 
Hahaha nendeni kwa MWAMPOSA kanisa la mamaaA.

Mbona mna vichwa vigumu hivyo?
kosa kubwa wanaloamini ni ati wakristo wameshikwa masikio na mwamposa, akishikamana na mwamposa hata kama ataumiza wakristo, jamii itamwona kuwa anapenda wakristo; siasa za aina hii kwenye imani za watu huwa hazifanyi kazi, ni rahisi tu kung'amua mbona. kwa taarifa yake, waumini wa gwajima ni mara 20 zaidi ya waumini wa mwamposa. wakikusanyika nchi nzima waje hapo dar es salaam, hapatatosha. ni makanisa zaidi ya 2000 nchi nzima, mwamposa ana kanisa gani lingine nje ya hapo kawe? na hata mwamposa akienda mikoani, ule umati ndani yake kuna wakatoliki wengi mno, na walokole wengi mno, walutherani wengi mno, ni wale wanaotoka huko huko kwenye makanisa anayoumiza ambapo akiondoa mkoa ule wanarudi kwenye makanisa yao huko alikowazuia wasiabudu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Soma hapo 👉Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) lililopo Ubungo Kibo Jijini Dar es salaam ambalo kwa Wiki tatu limetumiwa na Waumini wa KKAM na Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima kufanya Ibada, limevunjwa na kubomolewa kabisa ambapo Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amefika katika eneo hilo asubuhi hii leo July 13,2025 na kujionea pakiwa pamevunjwa kabisa na hakuna Muumini yoyote huku Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi.

Itakumbukwa Jumapili iliyopita Jeshi la Polisi liliimairisha ulinzi pia katika eneo kubwa la Ubungo ikiwemo kuzingira Kanisa hilo wakati Waumini wakifanya Ibada hatua ambayo ilijiri baada ya Jeshi hilo kuta onyo kwa kundi la Watu ambao walikuwa wakitokea KKAM na mabango baada ya ibada wakidai haki yao ya kuabudu kufuatia kufungwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima hivyo kupelekea Waumini kutawanywa kwa mabomu kwa Wiki mbili mfululizo huku Waumini wengine wakikamatwa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la KKAM.

Waumini kwa Kanisa la Gwajima kwa zaidi ya Wiki mbili walijumuika na Waumini wa KKAM Usharika wa Ubungo Kibo ambalo ni Kanisa rafiki na lililo jirani na Kanisa lao lililofungwa ambapo kwenye Ibada ya ya Jumapili iliyopita miongoni mwa waliohudhuria ni Naibu Katibu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima Akofu Maximilian Machumu Kadutu maarufu Askofu Mwanamapinduzi ambaye aliwasihi Waumini kutobeba mabango wala kufanya vurugu huku akiwaomba Polisi kutorusha mabovu kauli ambayo ilizaa matunda na Ibada ikakamilika kukiwa na usalama Waumini wakarejea makwao bila kupigwa na Polisi.

Bado haijajulikana sababu ya Kanisa kuvunjwa na aliyevunja lakini Majirani wa eneo hilo wanasema limevunjwa juzi Ijumaa.. tunaendelea kufuatilia kujua wanapofanyia Ibada Waumini wa Gwajima na wa KKM na tutakujuza >> youtu.be/PhTgm6FGIbg?si…View attachment 3404279
Na miaka ya mbeleni tutalipishwa fidia ya kivunja hilo kanisa mahakamani.
Kweli usimpe mwanamke mamlaka makubwa
 
kosa kubwa wanaloamini ni ati wakristo wameshikwa masikio na mwamposa, akishikamana na mwamposa hata kama ataumiza wakristo, jamii itamwona kuwa anapenda wakristo. kwa taarifa yake, waumini wa gwajima ni mara 20 zaidi ya waumini wa mwamposa. wakikusanyika nchi nzima waje hapo dar es salaam, hapatatosha. ni makanisa zaidi ya 2000 nchi nzima, mwamposa ana kanisa gani lingine nje ya hapo kawe? na hata mwamposa akienda mikoani, ule umati ndani yake kuna wakatoliki wengi mno, na walokole wengi mno, walutherani wengi mno, ni wale wanaotoka huko huko kwenye makanisa anayoumiza ambapo akiondoa mkoa ule wanarudi kwenye makanisa yao huko alikowazuia wasiabudu.
Shida kuna KKKT yule malasusa hapana mkuu
 
sasa kuna siku Mungu atashusha wokovu na utukufu kwa wale wanaotafuta haki, na hawa wanaounga mkono uovu wataaibika pamoja na wauvu. Mungu ni Mungu wa haki, haki yakaa ndani yake, unapomwonea mtu, unapomuua mtu n.k Mungu akiwa mbinguni huwa anaangalia wapi haki inavunjwa, wapi kuna machozi ya haki, na akishuka kutetea wahanga huwa anaacha alama ambayo hata vizazi vijavyo vitajifunza kutokana na namna ulivyoadhibiwa. ndio maana kwetu sisi tuliookoka huwa tunasema kuwa, afadhali hata uadhibiwe na mwanadamu kuliko kuadhibiwa na Mungu, hakuna anayeweza kustahimili adhabu ya Mungu. uzito wake hautastahimili.
 
Amina na sisi tuna sema maombi ya wenye haki huwa ni adhabu ya Mungu iliyo kali juu ya watesi wale.
 
Mungu huwa anajibu maombi, maelfu na maelfu toka makanisa 2000 ya ufufuo na uzima ambao hawana hatia yeyote, wamenyimwa haki ya kumwabudu Mungu. upo sahihi, sisi hatutumii nguvu ya bunduki, hatuna uwezo kupambana na Mungu anatuzuia kupambana kimwili, hatutafanya hivyo, ila tutamwomba Mungu kwa sababu jambo hili linaliumiza kanisa zima la Tanzania kuona wakristo wenzio wanazuiwa kuabudu, kwa sababu tunajua leo kwangu kesho kwako. wakristo wengi hasa mwamposa na mabula na mitume wa uongo wanashangilia bila kujua kesho inaweza kuwa kwao. tuendelee kumwomba Mungu katikati ya maumivu makali ya kuzuiwa kuabudu.

ZABURI 50:15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
 
Back
Top Bottom