Kanisa wanaposali Waumini wa Gwajima Lavunjwa

Kanisa wanaposali Waumini wa Gwajima Lavunjwa

Mungu huwa anajibu maombi, maelfu na maelfu toka makanisa 2000 ya ufufuo na uzima ambao hawana hatia yeyote, wamenyimwa haki ya kumwabudu Mungu. upo sahihi, sisi hatutumii nguvu ya bunduki, hatuna uwezo kupambana na Mungu anatuzuia kupambana kimwili, hatutafanya hivyo, ila tutamwomba Mungu kwa sababu jambo hili linaliumiza kanisa zima la Tanzania kuona wakristo wenzio wanazuiwa kuabudu, kwa sababu tunajua leo kwangu kesho kwako. wakristo wengi hasa mwamposa na mabula na mitume wa uongo wanashangilia bila kujua kesho inaweza kuwa kwao. tuendelee kumwomba Mungu katikati ya maumivu makali ya kuzuiwa kuabudu.

ZABURI 50:15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
Wakristo ni wakati sasa wa kushikamana mkadai haki yenu ya kuabudu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Soma hapo 👉Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) lililopo Ubungo Kibo Jijini Dar es salaam ambalo kwa Wiki tatu limetumiwa na Waumini wa KKAM na Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima kufanya Ibada, limevunjwa na kubomolewa kabisa ambapo Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amefika katika eneo hilo asubuhi hii leo July 13,2025 na kujionea pakiwa pamevunjwa kabisa na hakuna Muumini yoyote huku Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi.

Itakumbukwa Jumapili iliyopita Jeshi la Polisi liliimairisha ulinzi pia katika eneo kubwa la Ubungo ikiwemo kuzingira Kanisa hilo wakati Waumini wakifanya Ibada hatua ambayo ilijiri baada ya Jeshi hilo kuta onyo kwa kundi la Watu ambao walikuwa wakitokea KKAM na mabango baada ya ibada wakidai haki yao ya kuabudu kufuatia kufungwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima hivyo kupelekea Waumini kutawanywa kwa mabomu kwa Wiki mbili mfululizo huku Waumini wengine wakikamatwa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la KKAM.

Waumini kwa Kanisa la Gwajima kwa zaidi ya Wiki mbili walijumuika na Waumini wa KKAM Usharika wa Ubungo Kibo ambalo ni Kanisa rafiki na lililo jirani na Kanisa lao lililofungwa ambapo kwenye Ibada ya ya Jumapili iliyopita miongoni mwa waliohudhuria ni Naibu Katibu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima Akofu Maximilian Machumu Kadutu maarufu Askofu Mwanamapinduzi ambaye aliwasihi Waumini kutobeba mabango wala kufanya vurugu huku akiwaomba Polisi kutorusha mabovu kauli ambayo ilizaa matunda na Ibada ikakamilika kukiwa na usalama Waumini wakarejea makwao bila kupigwa na Polisi.

Bado haijajulikana sababu ya Kanisa kuvunjwa na aliyevunja lakini Majirani wa eneo hilo wanasema limevunjwa juzi Ijumaa.. tunaendelea kufuatilia kujua wanapofanyia Ibada Waumini wa Gwajima na wa KKM na tutakujuza >> youtu.be/PhTgm6FGIbg?si…View attachment 3404279
Hongereni sana wakuu kwa kuvunja makanisa.. Mungu awabariki kwa uhodari huo.
 
Wangeachana na Gwajima wafanye mambo yao huko wanakokwenda wanakosea sana kanisa huwa halivunjwi au msikiti ni kutafuta laana za bure tu..
Laana imeshatafutwa na kupatikana na sasa anasubiriwa ajaye kuja kuomba msamaha tena huku akisagia kunguni aliyepo. Yaani ni kuomba msamaha kanisa katoliki kwa kutaka kumuua Padre. Ila inasikitisha sana hakika huu ujinga ni mimba
 
Wakristo ni wakati sasa wa kushikamana mkadai haki yenu ya kuabudu
hakuna wakati wakristo walishatakiwa kushikamana kama wakati huu. wakati ambao watanganyika wanatawaliwa na mzanzibari, wakati ambao watanganyika wanafungiwa makanisa na muislam, wakishirikiana na kamanda wa polisi muislam. sisemi ili kuhamasisha udini, ila ukweli upo ndio maana serikali hii tangu mama yenu aingie madarakani macho yake yamekuwa uarabuni na kila kitu anawapa waarabu, sasa na ukristo anataka kuufuta ili wawepo watu wa dini yake au nini?
 
huyu mdogo wake na heche ana akili na busara nyingi, naamini uwezo alio nao hata kaka yake hamfikii, nilikuwa sijawahi kumsikia.
 
Jeshi letu lipo busy kutaka amani ipotee nchini, ila Mungu alivyo mwema halitawezekana. Amewajaza maarifa ya mbinguni wake wake ili waishi na mwovu kwa ujinga wake ila mwisho ataonekana kuwa yeye ni Mungu wa namna gani
 
Uhuru wa kuabudu hapa Nchini ni wakutosha kabisa. Ndio maana makanisa na misikiti inafunguliwa kila leo.
Hatusemi uhuru wa kuabudu hakuna kutokana na kufunguliwa makanisa na misikiti. Tunasema uhuru wa kuabudu hakuna kutokana na kufungwa kwa kanisa moja nchi nzima hivyo kuwazuia waumini wake wasisali popote nchini hata kama sio kwenye kanisa lao. Haijawahi kutokea tangu kupata uhuru.
 
Kanisa la Askofu Gwajima limekuwa mobile - kwa sasa wanakodi kumbi wanapiga neno na maombi vilivyo. Sasa kazi ya Police ni kuzuia kumbi zote nchi nzima kutumika kama ibada.

Chezea chochote Duniani ila si Imani ya mtu.
 
Kanisa la Askofu Gwajima limekuwa mobile - kwa sasa wanakodi kumbi wanapiga neno na maombi vilivyo. Sasa kazi ya Police ni kuzuia kumbi zote nchi nzima kutumika kama ibada.

Chezea chochote Duniani ila si Imani ya mtu.
kwahiyo watu pia wasifanye biashara kwa sababu ya kosa la gwajima (kama lipo).
 
hakuna wakati wakristo walishatakiwa kushikamana kama wakati huu. wakati ambao watanganyika wanatawaliwa na mzanzibari, wakati ambao watanganyika wanafungiwa makanisa na muislam, wakishirikiana na kamanda wa polisi muislam. sisemi ili kuhamasisha udini, ila ukweli upo ndio maana serikali hii tangu mama yenu aingie madarakani macho yake yamekuwa uarabuni na kila kitu anawapa waarabu, sasa na ukristo anataka kuufuta ili wawepo watu wa dini yake au nini?
Ndio analeta swaga za wa aarabu wazee wa kutesa na kuua mtu yeyote mwenye mawazo tofauti na yeye. Sema kila jambo lina mwanzo na mwisho ila mwisho wa bibi chura kiziwi ni gerezani akaungane na Pdidy
 
Back
Top Bottom