Kanizidi umri lakini ana sifa hizi. Je, nijilipue nimuoe?

Kanizidi umri lakini ana sifa hizi. Je, nijilipue nimuoe?

Habari zenu,

Niko kwenye mahusiano na mwanamke ambaye kwa sasa ana miaka 30 kanzidi mwaka mmoja. mahusiano yana zaid ya miaka 6. (haya mahusiano hayakua straight mana kuna muda nlikua nahama mkoa hata miaka mi2, tena narudi tunaendeleza mahusiano). Kimuonekano mm sio handsome. Nina sura ya kawaida tu.

mwanamke huyu ana sifa zifuatazo
Yeye ni multiskilled, ni mpish mzuri sana yan akipika utajiramba, afu ni msusi afu ana ujuzi wa kushona kiufupi yy ni asset sio liability.

Miaka yote hyo hajawahi kuniomba pesa.(kuna watu mtasema eti kuna mwanaume ananisaidia majukumu). NO, huyu mwanamke n mpambanaji anafanya vibarua na sasa anafanya kibarua anacholipwa laki na nusu lakn hajawahi niomba hata 500 ya vocha.

Ni mwanamke mtiifu&anaenijali sana, nkiwa sina hela ya kula naenda kwake nakula nalala na asbuhi ananiogesha na nikiondoka siachi hata 100 na hajawahi nidai

Ni mwanamke mpambanaji na mwenye focus ya maisha yaan analipwa lak na nusu lakn kajibana mpaka kanunua vitu vyote vya ndani mfano kabati la nguo, la vyombo, kitanda, na vngine kwa pesa zake. sometimes hua ananipigia kakosa hela ya mboga anakula ugali na asali🥺

Kazn kwao wanatoka saa11 jion, akitoka kazn anaingia barabaran kwny zile folen anauza mataulo, chaja n. k kwa wale madriver.

LAKINI SASA:
Sikua na mpango wa kuoa kwa sasa lakn leo kanipigia smu anaongea huku akitoa sauti ya uchungu huku analia, anambia yeye anaona umri wake unaenda kwa hyo kama sina mpango wa KUMUOA n bora tuachane tu (naogopa nikimkosa je ntapata wapi mwngne kama yeye?)

Sura yake sio nzuri sana (simaanishi ni mbaya NO) ana sura ya kawaida tu yaan haivutii wala haikeri. mm pia sura yangu sio handsome nawaza watoto wetu si watakua na sura ambazo sio nzuri

Mimi bado nabangaiza na shughuli za ujasiriamali wa bidhaa ndogo ndogo, nikiingia kwny ndoa saiz hayo majukumu ya ndoa ntayaweza kwl?

Kanizid mwaka mmoja.

Nawaza sku nikikutana na mwanamke mwenye sura na muonekano naoutaka afu akanikubali je si ndo chanzo cha kuona nlikosea kuoa?

NB:sijamzalisha wala kumpa mimba.
Najua humu kuna watu wenye ujuzi na uzoefu wa haya mambo naombeni mnishauri jaman nimuoe au niachane nae??
Yaani mwanaume unakaa unaandika unajisifu u marioooo hata aibu huna? Mjinga sana mwanamke siyo lazima akuombe hela mwehu wewe. Kama mwanaume jukumu mojawapo ni kujua mahitaji ya mwanamke na kuyatimiza kabla hujasaidiwa
Mario wa hovyo kabisa.
 
Maisha ni zaidi ya tendo na sura; chukulia mfano, umepata ajali na ukashindwa kutembea, ni nani atakuwa tayari kukusafisha kama mtoto mdogo pale kitandani?
huyu mwanamke anaweza kufanya yote haya bila tabu
 
Hata Trump alishawahi kusema ndoa nyingi sana zinakufa mostly because ya matatizo ya kipesa.

Sisemi unatakiwa kua kama Mo ndo uoe.

Mtoa mada amesema ANABANGAIZA anafuata nini kwenye ndoa?

Yaani hapo hajaoa ameshaanza kuomba ushauri, akioa si atajaza server huyu na nyuzi za kuomba ushauri?
Kwa hiyo trump mpaka kufikia mke wa tatu, kulikuwa na changamoto ya kifedha?
 
Yaani mwanaume unakaa unaandika unajisifu u marioooo hata aibu huna? Mjinga sana mwanamke siyo lazima akuombe hela mwehu wewe. Kama mwanaume jukumu mojawapo ni kujua mahitaji ya mwanamke na kuyatimiza kabla hujasaidiwa
Mario wa hovyo kabisa.
nadhan hujaelewa vzuri thread yangu
 
Jaman smu yangu inaisha chaji na hapa mtaani umeme umekata mkiona kmya msishangae
 
Kwa hiyo trump mpaka kufikia mke wa tatu, kulikuwa na changamoto ya kifedha?

Elewa mada. Hakusema it was THE ONLY thing.

Ila alisema nyingi zinavunjika kwa sababu hiyo.

Hujaelewa wapi pengine nikuelekeze?
 
Elewa mada. Hakusema it was THE ONLY thing.

Ila alisema nyingi zinavunjika kwa sababu hiyo.

Hujaelewa wapi pengine nikuelekeze?
Ilikuwa ni mtazamo wake, bado kuthibitika kisayansi
 
Kaangalie stats za what causes most divorces in the US alagu rudi hapa
Sababu ya kwanza ni wanawake kuwa na tamaa ya pesa na kutaka mgao wao, wanatumia mahusiano kama sehemu ya kupata mtaji; rejea kwa matajiri ambao ndoa zao zimevunjika.​
 
mbona ishu ya sura umeikazia sana? Kwamba wote ni wa kawaida,,, ! Dah.,,, !

ni kama unamuonea huruma ama hujiamini kama unaweza pata mwingine akakupenda! Sikia man, unaonekana bado ni mtu una-hustle mambo bado hayajajipa ! Muambie kwa sasa hujajipanga kuoa, mambo yako hayajakaa sawa, akilusubiri it's OK, akikataa wacha aende !! Umesema upo na 29, atleast una miaka 3 ya kukomaa ndo uoe walau na 32,,,! Huyo huenda kapata bwana, sasa anakupima! Usioe kumfurahisha mtu ukateseke bure, dunia imevaa bukta haina huruma !
Umemaliza mkuu...Napigia na lamination Hapo kwenye Sura ,usimpende Mtu sababu ya kitu kimoja Tu maana kile kitu kikiondoka utateseka mno
 
Back
Top Bottom