Pole sana .Pole sana mkuu. Ni mtihani,kaza moyo.
Uliwahi ulizia kuhusu Butaro Cancer Center of Excellence? Ni kituo cha wamarekani,kipo Rwanda. Nimeonapo watu wengi wa nchi mbali mbali za Africa, sikufatilia kujua ila huenda wakawa na advanced technology kupunguza maumivu. Kupona sizungumzii.
Mgonjwa tuliewahi kuwa nae alitoboka shavu, ila mpaka anakufa, maumivu hayakuwa makali.
Labda ujaribu kufatilia uone kama watakuwa na la ziada
Huwezi kupona kwa KUBUGIA BUGIA TU madawa au TIBA, lazima akili yako isafishwe kwanza.Sawa umepasua ukweli ila mbona hujasema ni mmea upi huo atumie ila aimarike?, badala ya kusema leta kwanza ufumbuzi wa tatizo, akipona ndiyo tutarudi kupasua huo ukweli mkuu
Maji lita 5, na majani ndoo ya kilo 10Ahsante sana, ila sijaelewa maji lita 10
Maji nusu lita?
Naomba uniandikie vuzur kama hutojali
Kwenye shavu tu mkuu,kakidonda kadogo kalianzia mdomoni kwa ndani.Pole sana .
Alikua na kansa ya eneo gani mpaka anatoboka shavu?
Nikupe pole sana kwa kuuguliwa na mkeo... ila ningependa tu kuweka kitu kimoja sawa...Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa
Poleni sana kwa kipindi mnachopitia.Njoo tupeane moyo.
Nimeanza kumuuguza dada yangu cancer kuanzia mwaka 2019,
Tuliambiwa afanye Chemo baadae afanyiwe upasuaji....
Akaanza mizunguko minne akamaliza, ikaongezwa minne akamaliza. Akarudishwa Muhimbili Kwa ajili ya upasuaji, madaktari wakatuambia arudi ocean road uvimbe haujapungua.
Ikaongezwa mizunguko 8 Tena , akapewa transfer Muhimbili awamu hii mgonjwa akagoma kufanyiwa Op. Akakaa nyumbani mwaka bila matibabu ya hospital.
Ziwa likatoboka likawa linamwaga maji pamoja na usaha, tukarudi hospital,wakasema aanze chemo upya ikaenda mizunguko 6 na mionzi 16. Kamaliza mwez wa 10 mwaka huu Kwa Sasa kapewa mapumziko ya miezi mitatu na dawa anatumia.
Eneo la ziwa limefutika na wekundu kama kamwagiwa maji ya moto.
Cancer ni stage 4.
Ushauri wangu
Kama unaweza mpeleka ocean road mpelekee pale.
Pili kidonda kisafishwe Kila siku na maji ya drip wekeni na fragine ya vidonge mnatwanga mnapakaa eneo la kidonda kabla ya kukifunga
Kidonda usikifunge na khanga Wala kitenge funga na bandage.
Ajitahidi kunywa juisi ya stafeli angalau Kila siku glass Moja.
Majani yake pia chemsha anywee.
Mungu atutie nguvu katika Janga hili πππππ
Asante sana πππPoleni sana kwa kipindi mnachopitia.
Ameen mkuuPole Sana Kiongozi..... Nayahisi maumivu unayopitia....
Sina ujuzi kwenye hili ila Naomba Mungu amlinde na kumpa nguvu Mke wako.
Amuondolee kabisa maumivu yanayomsumbua, na kumponya kabisa hiyo saratani Kwa Jina la Yesu Kristo.
Damu ya Yesu imfunike na naalika ufalme wa Mungu utawale Nyumbani kwako.
Pia mpende sana mke wako Kwa moyo wako wote Katika kipindi hiki anachopitia na Mungu wa Mbinguni atawabariki.
Hakuna linaloshindikana mbele zake Kwa Imani.
Amina.
Pole san mkuuYapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.
Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.
Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.
Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.
Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.
KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.
KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.
Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu
Ushauri wowote pia napokea.
Aisee, pole sana mkuu! Mungu akupe moyo mkuu wa uvumilivu! Mungu aweke neema yake!Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.