SI KWELI Kanu ni Mnyama anayenukia harufu ya ubwabwa porini/vichakani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Kanu.jpg
 
Tunachokijua
Kanu ni wanyama wadogo, Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mpaka sasa kuna spishi 17 za kanu zilizoainishwa.

330px-Rusty-spotted_Genet_%28Genetta_maculata%29_%2832484079077%29.jpg
Kumekuwa na hoja inayodai kuwa mnyama Kanu hutoa ushuzi wenye harufu ya wali pale anapohisi adui kama njia ya kujilinda.

Je, ukweli wa hoja hiyo ukoje?
JamiiCheck imepitia makala na tafiti mbalimbali kuhusu maisha ya Kanu ili kupata uhalisia wa madai kuwa Kanu hutoa ushuzi ambao una harufu kama wali na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kanu wana tezi zinazozalisha harufu ambazo zipo kati ya mwanzo wa mikia yao na karibu na sehemu ya haja kubwa. Tezi hizo za harufu hutoa majimaji yenye harufu ya mkojo ambayo kanu hutumia kwa mawasiliano, kuashiria maeneo yao, na wakati mwingine kuwatisha wanyama au maadui wanaowawinda.

Kama wanyama wengine wengi, kanu hutegemea kuacha alama za harufu kama njia ya kutoa taarifa kuhusu uwepo wao, hali yao ya uzazi, na mipaka yao kwa wanyama wengine.

Aidha, Harufu inayotolewa na tezi za kanu hainuki kama wali kam inavyodaiwa bali Kanu hutoa harufu ya mkojo kutoka kwenye tezi zao, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kuwa kali na isiyopendeza, sawa na harufu ya wanyama wengine walao nyama.

Pia JamiiCheck imemtafuta na kuzungumza na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ambaye ameeleza kuwa harufu ya Ubwabwa au wali porini haihusiani na wanyama mbalimbali ambao wamekuwa wakihusishwa nayo, aidha amesema kuwa harufu hiyo hutolewa na aina fulani ya miti.

"Kuhusu harufu ya ubwabwa porini wengi huihusisha na wanyama mbalimbali. Lakini Kiuhalisia kuna aina fulani ya miti Mti kama Potato Bush (kiingereza) na Jina la kisayansi ni PHYLLANTHUS RETICULATUS ambayo hutoa harufu ya aina hiyo na sio Kanu wala Gamba la nyoka maana wengine wanahusisha na nyoka kujivua gamba".:-Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja
Mkuu hujaelimika, lkn pia wewe sio mstaarabu hata tone na huna akili. Ina maana hujui kwamba unafanya makosa?? Kwanini unamtoa uhai na unapost upuuzi wako. Endapo unasumbuliwa na Mnyama wa aina hiyo ulipaswa kutoa taarifa kwa TAWA mamlaka ya Wanyapori wao wangemwekea mtego na kumpeleka mahala sahihi akahifadhiwe lkn kwa Umbumbu wako umemuua mnyama huyo halafu unaposti ujinga wako. Mpumbavu sana umenikera sana mkuu, ID zetu Zingekuwa zinautambulisho ungefuatwa na mkono wa sheria pimbi wewe.
No thanks kwa video hizi
Mstaarabu anapotukana mitusi mfano wa hii unabaki unashangaa tu!
Ungepungukiwa na nini ungemuelekeza kwa utaratibu alitakiwa afanye jambo gani kuokoa kuku wake na maisha ya huyo mnyama?
 
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.
View attachment 3119620
Anaitwa serval cat kwa Kiingereza. Nilishamuona mara kadhaa, sikujua kwamba ndie anaetoa harufu ya namna hiyo
 
Mkuu hujaelimika, lkn pia wewe sio mstaarabu hata tone na huna akili. Ina maana hujui kwamba unafanya makosa?? Kwanini unamtoa uhai na unapost upuuzi wako. Endapo unasumbuliwa na Mnyama wa aina hiyo ulipaswa kutoa taarifa kwa TAWA mamlaka ya Wanyapori wao wangemwekea mtego na kumpeleka mahala sahihi akahifadhiwe lkn kwa Umbumbu wako umemuua mnyama huyo halafu unaposti ujinga wako. Mpumbavu sana umenikera sana mkuu, ID zetu Zingekuwa zinautambulisho ungefuatwa na mkono wa sheria pimbi wewe.
No thanks kwa video hizi
Alikuwa anakuletea nyama ya kuku nnn mkuu
 
Ni huyu anaachi ushuzi anapanda juu ya mti chini kama kuna mbwa hilo eneo watazu nguka kutwa nzima wakitafuta.
Hata ukimgusa huo mkono unanukia balaa hadi ufue nguo ndio harufu kutoka
Ukinawa kwa sabuni tuu na brush harufu haitoki
Huyu ndiye wa kuitwa fungo ?
 
Jiandae kuilipa faini serikali kupitia Wanyamapori act na TAWA
 
Binadamu tuna kaukatili fulani, ilikua kwenye harakati zake za kutafuta riziki ili aweze kuendelea kuishi kwenye ardhi hii ya dunia kama vile tulivyo sisi ama hao kuku, ila ndio hivyo tena kakutana na binadsmuy mwenye ubinasfi .
Binaadamu wanauwa binaadamu wenzao, seuze mnyama
 
Mkuu hujaelimika, lkn pia wewe sio mstaarabu hata tone na huna akili. Ina maana hujui kwamba unafanya makosa?? Kwanini unamtoa uhai na unapost upuuzi wako. Endapo unasumbuliwa na Mnyama wa aina hiyo ulipaswa kutoa taarifa kwa TAWA mamlaka ya Wanyapori wao wangemwekea mtego na kumpeleka mahala sahihi akahifadhiwe lkn kwa Umbumbu wako umemuua mnyama huyo halafu unaposti ujinga wako. Mpumbavu sana umenikera sana mkuu, ID zetu Zingekuwa zinautambulisho ungefuatwa na mkono wa sheria pimbi wewe.
No thanks kwa video hizi
Punguza mihemko.
 
Aisee tumekula sana huyu mdudu anaitwa mtoro
 
Mkuu Kuna yule anaweza enda kwenye shimo akaingia mwili mzima akaacha mkunduh nje, huo mkunduh wake umejaa mavi mavi na mafunza yaliyoozeana... Ndege, kuku au mnyama yoyote akienda kula na kulamba huo mkunduh huyo mwamba atambana kichwa huyu mnyama mpaka afe....

Huyo kwa huku dar hawapo
 
Mkuu hujaelimika, lkn pia wewe sio mstaarabu hata tone na huna akili. Ina maana hujui kwamba unafanya makosa?? Kwanini unamtoa uhai na unapost upuuzi wako. Endapo unasumbuliwa na Mnyama wa aina hiyo ulipaswa kutoa taarifa kwa TAWA mamlaka ya Wanyapori wao wangemwekea mtego na kumpeleka mahala sahihi akahifadhiwe lkn kwa Umbumbu wako umemuua mnyama huyo halafu unaposti ujinga wako. Mpumbavu sana umenikera sana mkuu, ID zetu Zingekuwa zinautambulisho ungefuatwa na mkono wa sheria pimbi wewe.
No thanks kwa video hizi
Kwamba wewe ndie umeelimika? Ungekuwa mstarabu na umeelimika ungetumia lugha hizi? Hapo ulipo una kadegree kutoka SUA hata njiwa hujawahi kufuga na hata hujui uchungu wa kupoteza mifugo. Hovyo kabisa
 
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka.

Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake.

Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani.

Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine).

Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue.

Huyu nimetega baada ya kula kuku wangu sana.

Mdiyo wamemuua ili wamle ubwabwa?
Hivi ile harufu ya wale si huwa ni nyoka akiwa anajivua ametoka kujivua gamba?
Ingawa wengine walikuwa wanaamini ni majini yapo kupika. Bongo ya zamani ilikuwa tamu sana aisee, sijui siku hizi hata mnawezaji kuishi.
 
Kwa uelewa wangu najua chatu ndo halafu kadhaa kulingana na kitoweo alichoona

Mfano akiona nyani atatoka harufu ya ndizi na akiona mbwa ama jamii ya bweha atatoka harufu ya mzoga ulio oza/haribika ana harufu nyingi tu kulingana na windo alilo ona.
 
Mkuu umefanya kosa sana kumuua. Hao viumbe wapo hatarini kutoweka.
Mara ya mwisho kumuona Kanu vichaka makumbuka ilikuwa 1994.

Next time pigia simu Afisa wanyapori TANAPA watakuja kumkamata sio kuwaua.
 
Mkuu umefanya kosa sana kumuua. Hao viumbe wapo hatarini kutoweka.
Mara ya mwisho kumuona Kanu vichaka makumbuka ilikuwa 1994.

Next time pigia simu Afisa wanyaporiTANAPA watakuja kumkamata sio kuwaua.
 
Back
Top Bottom