Kufanya siasa hapa nchini hakujawahi kupungikiwa vitimbwi.
Haki, usawa na ustaarabu vimemilikishwa chama tawala. Mamlaka ikajikita kuhakikisha wengine hawafurukuti.
Yote haya yakifanikishwa kutokana na mapungufu makubwa ya makusudi kwenye katiba ya nchi isiyokidhi zama tulimo.
Pana sheria zinazo simamia uwepo na shughuli za vyama vya siasa zenye kujitosheleza kwa mujibu wa katiba.
Ajabu na kweli mamlaka imekuwa ikizikiuka sheria hizi kwa miaka yote. Kwa sababu hawawezi tena kuendelea kuzikiuka kama zilivyo, sasa kunakuja zinazoitwa kanuni ili kuhalalisha batili hii kuendelea.
Kufanikisha hili TCD ya Mwami Ruyagwa imekabidhiwa mikoba hiyo.
Katika TCD kuna vyama vya 5 (ACT, CCM, Chadema, CUF na NCCR). CCM na ACT vina agenda zilizo tofauti zaidi na vingine. Hawa ndiyo wanaoonekana kuwa waasisi wa mkakati mpya huu.
Lengo kuu likiwa kufifisha agenda ya madai ya katiba mpya.
Haihitajiki kuwa nabii kutambua kuwa msingi mkuu wa zinazosemekana kanuni za vyama siasa zitakuwa kuhakikisha hakuna katiba mpya hadi angalau baada ya 2025.
Panga pangua kwa mujibu wa kanuni za kina Mwami Ruyagwa na wenzake, kudai katiba mpya kabla ya 2025 itakuwa ni haramu kuliko kulima bange.