Kanuni Mpya vyama vya Siasa zinazotaka kupenyezwa

Kufanya siasa hapa nchini hakujawahi kupungikiwa vitimbwi.

Haki, usawa na ustaarabu vimemilikishwa chama tawala. Mamlaka ikajikita kuhakikisha wengine hawafurukuti.

Yote haya yakifanikishwa kutokana na mapungufu makubwa ya makusudi kwenye katiba ya nchi isiyokidhi zama tulimo.

Pana sheria zinazo simamia uwepo na shughuli za vyama vya siasa zenye kujitosheleza kwa mujibu wa katiba.

Ajabu na kweli mamlaka imekuwa ikizikiuka sheria hizi kwa miaka yote. Kwa sababu hawawezi tena kuendelea kuzikiuka kama zilivyo, sasa kunakuja zinazoitwa kanuni ili kuhalalisha batili hii kuendelea.

Kufanikisha hili TCD ya Mwami Ruyagwa imekabidhiwa mikoba hiyo.

Katika TCD kuna vyama vya 5 (ACT, CCM, Chadema, CUF na NCCR). CCM na ACT vina agenda zilizo tofauti zaidi na vingine. Hawa ndiyo wanaoonekana kuwa waasisi wa mkakati mpya huu.

Lengo kuu likiwa kufifisha agenda ya madai ya katiba mpya.

Haihitajiki kuwa nabii kutambua kuwa msingi mkuu wa zinazosemekana kanuni za vyama siasa zitakuwa kuhakikisha hakuna katiba mpya hadi angalau baada ya 2025.

Panga pangua kwa mujibu wa kanuni za kina Mwami Ruyagwa na wenzake, kudai katiba mpya kabla ya 2025 itakuwa ni haramu kuliko kulima bange.
Watafeli tu
 
Mwami Ruyagwa kwa kutokujua au kwa kujua, ni mzigo mkubwa kwa taifa hili
Alivyokuwa anawaomba wazungu wasiikopeshe pesa serikali mnamchekea mlidhani unafiki ule ungeishia kwenye serikali ya awamu ya tano tu?
 
Kwa hiyo wewe mkuu ulipo sasa unamchekea?
 
Inawezekana Zitto ameshakata tamaa na maisha katika Ulimwengu wa siasa, anatafuta mitaji ya biashara tu au uwekezaji mkubwa.
Hili ni wazo jipya ninaloliunga mkono.
Au pengine kaona njia pekee ya yeye kuendelea kuwa 'relevant' ndani ya siasa ni kujisalimisha kwa CCM. Sasa anasubiri tu uteuzi na maisha yaendelee.
 
Kutokana na usaliti wa Zitto na ACT yake, maisha ya ACT, hakika yatategemea uharamia wa CCM. Siku uharamia wa CCM umekomeshwa, itakuwa pia mwisho wa ACT.
Zitto si ameshahakikishiwa ajira kwa miaka 9?
 
Hili ni wazo jipya ninaloliunga mkono.
Au pengine kaona njia pekee ya yeye kuendelea kuwa 'relevant' ndani ya siasa ni kujisalimisha kwa CCM. Sasa anasubiri tu uteuzi na maisha yaendelee.
Zitto ilikuwa ateuliwa muda tu kabla ya Zuhura Yunus ila vetting imemkataa.
 
Hivi kweli kuna kitu kama "vetting" katika nchi yetu, au hii inafanya kazi kwa baadhi ya wateuliwa na haifanyi kazi kwa wengine?

Maana naona kuna baadhi ya wanaoteuliwa rekodi zao zinatisha zaidi pengine hata zaidi ya huyo Zitto.

Mteuaji hana uwezo wa ku'overide' 'vetiting' zisizokuwa rafiki kwa watu anaowateua? Maanake huyu mtu ana madaraka makubwa sana.
 
Kufanya siasa hapa nchini hakujawahi kupungikiwa vitimbwi.

Haki, usawa na ustaarabu vimemilikishwa chama tawala. Mamlaka ikajikita kuhakikisha wengine hawafurukuti.

Yote haya yakifanikishwa kutokana na mapungufu makubwa ya makusudi kwenye katiba ya nchi isiyokidhi zama tulimo.

Pana sheria zinazo simamia uwepo na shughuli za vyama vya siasa zenye kujitosheleza kwa mujibu wa katiba.

Ajabu na kweli mamlaka imekuwa ikizikiuka sheria hizi kwa miaka yote. Kwa sababu hawawezi tena kuendelea kuzikiuka kama zilivyo, sasa kunakuja zinazoitwa kanuni ili kuhalalisha batili hii kuendelea.

Kufanikisha hili TCD ya Mwami Ruyagwa imekabidhiwa mikoba hiyo.

Katika TCD kuna vyama vya 5 (ACT, CCM, Chadema, CUF na NCCR). CCM na ACT vina agenda zilizo tofauti zaidi na vingine. Hawa ndiyo wanaoonekana kuwa waasisi wa mkakati mpya huu.

Lengo kuu likiwa kufifisha agenda ya madai ya katiba mpya.

Haihitajiki kuwa nabii kutambua kuwa msingi mkuu wa zinazosemekana kanuni za vyama siasa zitakuwa kuhakikisha hakuna katiba mpya hadi angalau baada ya 2025.

Panga pangua kwa mujibu wa kanuni za kina Mwami Ruyagwa na wenzake, kudai katiba mpya kabla ya 2025 itakuwa ni haramu kuliko kulima bange.
Na mimi naunga mkono Katiba mpya baada ya 2025 kwa sababu ya Bunge hili kutawaliwa na wana ccm.
 
Wanasema "if you can't beat it you join it."

Kwa kiswahili kisebu sebu na kiroho papo.

Kwani tukiamua kusubiria dodo kwenye mnazi kunakuwa kuna option nyingine tena mkuu?

Au wananchi wakitaka katiba yao kwa namna wanavyotaka nini kinachozuia?
 
Back
Top Bottom