Kanuni mpya za TFF ni za ovyo kupindukia; wanaendesha mpira kishamba sana!

Ondoa neno kanuni za tff ni za ligi ni za ligi kuu zimepitishwa na wenye viti na viongozi wa juu wa vilabu
Mkuu TFF ndio wasimamizi wa ligi na kamati zote hizo. Hatuwezi kuwaondoa kwenye lawama hata siku moja.
 
Mkuu sasa mbona unalalamika badala ya kutoa mapendekezo? Mimi nimetolea mifano mataifa yaliyoendelea kimpira ili tuige kutoka kwao. Wewe hupendi vitu vizuri? Unataka wachezaji wazuiliwe kuwa na wadhamini wafe njaa au wakaibe?
 
Na bodi ya ligi ipo chini ya nani?
Hujui kuwa TPBL ni entity Huru.

Wajumbe wa bodi ya ligi ni viongozi wa club zetu au hujui Hilo. Kanuni zote za ligi hupitishwa na viongozi wa timu zote waliomo kwenye bodi ya ligi.


Wewe umeona Kuna club hata Moja imepinga hiki ulichoandika?
 
Mkuu sasa mbona unalalamika badala ya kutoa mapendekezo? Mimi nimetolea mifano mataifa yaliyoendelea kimpira ili tuige kutoka kwao. Wewe hupendi vitu vizuri? Unataka wachezaji wazuiliwe kuwa na wadhamini wafe njaa au wakaibe?
Ronaldo alisign na Nike kama brand ambassador kabla adidas hajasign na Madrid. Barclays alikua ni mfadhili wa League,standard chartered ni mfadhili wa club mfano NBC anadhamini league yetu lakini sio vilabu vyetu so kila timu inaouwezo wa kutafuta mdhamini na ndio maana tuna akina sportpesa n.k.
Wachezaji wetu wanataka kuwa brand ambassadors wa crdb wakati tayari NBC ametoa dau la kudhamini ligi....yaani NBC amsaidie crdb kutangaza biashara? Not ease.
 
Basi kama shida ni hii NBC wawe wanawalipa wachezaji wanaokosa pesa ili kufidia hasara wanayopata. Vinginevyo utakuwa ushuzi tu, hakuna jipya. Hatuwezi kuruhusi wachezaji wafe njaa eti kwa sababu ya hii mikataba ya kipuuzi. Ni afadhali ligi ikose wadhamini kuliko kuruhusu huu upuuzi wa ajabu ajabu.
 
Ni kweli mkuu, udhamini wa ligi ungekuwa baina ya bodi ya ligi,tff na mdhamini. Ni muhimu kanuni zetu zikatoa nafasi hiyo japo najua ikija kampuni nyingne kwa lengo Hilo hamna shida. Tatizo ni crdb same business na kama ujuavyo nongwa za kibongo kwenye biashara mfanano
 
Wamezuia kutangaza biashara ya mshindani wa mdhamini mkuu tu
 
Barclays haidhamini EPL
 
Kile ni kikundi cha wahuni waliojificha kwwnye mgongo wa chama twawala
 
Kile ni kikundi cha wahuni waliojificha kwwnye mgongo wa chama twawala
Kweli kabisa mkuu. Kuna namna wanavyoshirikiana kuiba fedha zinazotokana na mpira na kuziingiza kwenye chama kuisadia CCM kuiba kura na kulaghai wananchi kila kukicha.
 
Reactions: ita
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…