Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
234
Reaction score
390
Kanuni mpya za usajili wa Laini za Simu za mwaka 2020 zimetangazwa kwenye Gazetti la Serikali la tarehe 7 February, 2020 kama Tangazo la Serikali No. 112 la 2020. Jina fupi (short title) la Kanuni hizo ni the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020.

Baadhi ya maswala kadhaa ambayo yamejitokeza katika Kanuni za Usajili wa Laini za Simu hizi mpya ni yafuatayo:

(1) Kwa sasa ni lazima kisheria kusajiri Laini ya Simu kwa alama za vidole.

(2) Usajili wa Laini ya Simu kwa alama za vidole utafanywa kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na NIDA pekee au Namba ya Kitambulisho cha Taifa na vitambulisho vingine kama vile kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva na passport havitatumika tena katika usajili wa laini za simu.

(3) Ni marufuku kwa mtu (binadamu) kusajili Laini ya Simu zaidi ya moja (1) kwenye mtandao mmoja wa simu kwa ajiri ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi (message), kuongea na data. Kwa mfano, ni marufuku kuwa na laini mbili au zaidi za Vodacom, unapaswa kuwa na laini moja tu ya Vodacom.

(4) Mtu anaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 4 kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na laini za simu nne (4) za Vodacom kwa ajili ya kutumia kwenye modem.

(5) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 30 kwa ajili ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi (message), kuongea na data.

(6) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 50 kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki.

(7) Mtu ambaye anamiliki laini za simu mbili au zaidi za mtandao mmoja wa simu amepewa muda mpaka tarehe 30 June, 2020 kuchagua laini moja tu atakayotumia.

(8) Mtandao wa Simu unawajibika kuzima laini ya simu ambayo haijasajiriwa kwa njia ya alama za vidole.

(9) Kila laini ya simu lazima iwe na PIN (Personal Identification Number) ambayo lazima iwekwe kwenye simu au kifaa cha kieletroniki kila wakati simu inapowashwa au inapobadilishwa.

(10) Laini ya Simu isipotumika kwa siku 90 mfululizo lazima ifungwe.

(11) Taarifa yoyote iliyowasilishwa kwenye mtandao wa simu ikibadilika lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa ndani ya siku 14 zikiesabika tokea siku ambayo mabadiliko hayo yametokea. Kwa mfano, mtu akibadilisha jina au majina yake amabyo alisajiria laini ya simu kutoka na kuolewa lazima atoe taarifa ya kubadilisha majina yake kwenye mtandao wa simu ndani ya siku 14 tokea siku alipobadili jina.

(12) Ukitokea wizi au upotevu wa laini ya simu lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa Polisi.

(13) Ili mtu apewa laini mpya kutokana na upotevu au wizi lazima apeleke kwenye mtandao wa simu Loss Report au taarifa ya uchunguzi wa awali kutoka Polisi.

(14) Mtu ambaye atakiuka masharti yoyote ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu, 2020 atakuwa ametenda kosa la jinai na adhabu zake ni kifungo cha kuanzia mwaka 1 mpaka miaka 10 au fine kati ya Tsh 300, 000 mpaka Tshs 30 Million kulinga na kosa husika au vyote kwa pamoja kifungo na faini.

(i) Angalizo la Kwanza
Kabla ya tarehe 7 February, 2020 kurudi nyuma, sheria au Kanuni za usajiri wa Laini za Simu, 2018 zilikuwa zilimruhusu mtu kusajiri laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia vitambulisho vitano (5) vifuatavyo;

(a) Kitambulisho cha Taifa

(b) Kitambulisho cha Mpiga kura
.

(c) Leseni ya Udereva

(d) Passport

(e) Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi


Kwa msingi huu basi, ilikuwa ni kinyume na sheria kwa TCRA kuwalazimisha watu kusajiri laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha Taifa pekee kabla ya tarehe 7 February, 2020 kwa kuwa Kanuni hizi mpya zilikuwa bado hazijaanza kufanya kazi na hapakuwepo na sheria yoyote inayoweka sharti hilo kwa sababu sheria na Kanuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaanza kufanya kazi au kutumika na kuwa na nguvu ya kisheria (force of law) baada ya kutangazwa kwenye Gazetti la Serikali, hili ni takwa la Kifungu cha 14 na 37 (1) (a) cha Sheria ya Tafsiri, Sura ya 1, Toleo la 2002. Hivyo basi Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu za mwaka 2018 yaani the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2018 (Tangazo la Serikali Na. 18 la 2018) zilifanyakazi kuanzia tarehe 2 February, 2018 mpaka tarehe 6 February, 2020. Maana yake ni kwamba raia wa nchi hii walikuwa na haki ya kusajiri Laini za Simu kwa alama za vidole kwa kutumia mojawapo ya vitambulisho vitano (5) vilivyoainishwa hapo juu ikiwemo kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva na passport mpaka tarehe 6 February, 2020.


(ii) Angalizo la Pili
Hizi kanuni hazina kitu kinaitwa Retrospective Operation or effect kwa maana ya kwamba hazifanyi kazi kwa kurudi nyuma bali zinafanya kazi kwa kwenda mbele kwa maana ya kuwa zitatumika kwenye Laini za Simu ambazo zitasajiriwa kuanzia tarehe 7 February, 2020 tu kwenda mbele yaani hizi kanuni zina fall kwenye category ya prospective operation. Kwa, maana hii, mtu ambaye alisajiri laini yake ya simu kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga Kura au Leseni Udereva au Passport kabla ya 7 February, 2020 haguswi na kanuni hizi katika sheria.

Hivyo, basi itakuwa kinyume na sheria na itakuwa uvunjifu wa sheria kwa TCRA au Mtandao wa Simu kama Vodacom, Tigo na Airtel kufunga laini ya mteja ambaye alisajiri laini yake kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni Udereva au Passport kabla ya tarehe 7 February, 2020. Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na ya Afrika Masharriki (Defunct) mara kadhaa katika kesi kadhaa iliweka msimamo thabiti kuwa sheria inayogusa haki za msingi (substantive law) haiwezi kufanya kazi kwa kurudi nyuma (it cannot operate retrospectively) isipokuwa pale ambapo imetamkwa bayana bila utata wowote kuwa itafanya kazi kwa kurudi nyuma na msimamo huu uliwekwa na mahakama tajwa katika kesi zifuatazo, among others;

(i) S.S Makorongo Vs Severino Consigilio [2005] EA 247

(ii) Municipality of Mombasa Vs Nyali Ltd (1963) E. A. 371

(iii) Bidco Oil and Soap Ltd Vs Commissioner General Tanzania Revenue Authority, Civil Appeal No. 89 of 2009

(iii) Gaspar Peter Vs Mtwara Urban Water Supply Authority (Mtuwasa) Civil Appeal No. 35 of 2017

Kanuni za Usajili wa Laini za Simu za mwaka 2020 zinagusa haki za msingi (substantive law) za raia kuhusu swala la kuwasiliana au haki ya kuwasiliana ambayo ni haki ya kikatiba na kisheria, hivyo basi, kanunu hizi haziwezi kufanya kazi kwa kurudi nyuma (it cannot operate retrospectively) kwa sababu katika kanuni hizi hakuna kanuni yoyote au masharti yoyote ambayo yametamka bayana bila utata wowote kuwa kanuni hizi za usajiri wa laini za simu za 2020 zitafanya kazi kwa kurudi nyuma. Hivyo basi, Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu za mwaka 2020 zitafanya kazi kwa kwenda mbele (prospectively) kuanzia tarehe 7 February, 2020.

Wenu Mwana JF Matojo M. Cosatta
 
Mi nadhani suala la line ni jukumu na dhamana ya mtumiaji ndiye anawajibika kwa kila kitu, labda wanataka kuwa wanatuwekea bundle.. Na kupunguza gharama za kutuhudumia..
 
Hizo lugha zenu za kisheria sijazielewa ngoja nihoji, Ina maana sisi tuliosajili kwa kitambulisho cha mpiga kura ama passport au leseni kabla ya tarehe 7 February, hiyo sheria ya kufungiwa laini Kama haujasajili kwa alama za vidole haituhusu?
 
Hizi sheria zenye macho baada ya muda zitabadilishwa tu. Kwahiyo ukiwa mgeni na una Business Visa hutoruhusiwa kutumia laini ya cm kwa sababu sio raia?

Hoja kwamba kitambulisho pekeee kinachotambulika ni NIDA .... maana yake vingine vyote havina maaana ?
 
Kwa nchi kama Tanzania haya tunayaita maendeleo. Hahaaaaa. Wenzetu wanapambana wakaishi sayari nyingine, sisi hata formula ya kutengeneza kiberiti hatuna tumebaki kufungiana ili kuonyeshana nani ni mwamba.

Sasa kama mimi nina line ya voda ya nyumbani, wanataka nani aje anisajilie?

Hopeless kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo lugha zenu za kisheria sijazielewa ngoja nihoji, Ina maana sisi tuliosajili kwa kitambulisho Cha mpiga kura ama passport au leseni kabla ya tarehe 7 February,hiyo sheria ya kufungiwa laini Kama haujasajili kwa alama za vidole haituhusu.....???
Jibu kwa kifupi, HAIWAHUSU.
Mko salama.
 
Jibu kwa kifupi, HAIWAHUSU.
Mko salama.
Tusome kuelewa tusisome tukijitafutia favor,pale juu imeandikwa.....waliosajili laini zao kwa kutumia vitambulisho ABCD kwa “ALAMA ZA VIDOLE” siyo ile ya kuandikwa kwenye makaratasi ila kwa finger print ndo wameokoka.

Mwenyewe nilipokuwa nasoma nikawa najiuliza hawa voda na Tigo wamenifungia nini line zangu ila nilivyorudia kuisoma ndo nikaelewa.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Hivi nani anajua kesho yake, kwani mtu akiwa na laini mbili au zaidi za mtandao mmoja zilizosajiliwa kwa alama za vidole, mamlaka husika zinapungukiwa nini, au ndo kusema kila mtu apate, "Ujamaalism" kwenye soko huria wa nini tena? Tunaimba kijamaa tunacheza kibepari, taabu tupu!
 
Back
Top Bottom