Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Asante sana Matojo, unastahili kuwa jaji sema basi tu
 
KUNA ULE MSEMO WA TUNA SAFARI NDEFU WALA SIONI KAMA TUNA SAFARI, AFRIKA HAIENDI POPOTE MAANA MUAFRIKA AKISHAKUWA KINGOZI ANAJIPA UMUNGU MTU.

WALIPOSEMA AFRIKA IS BLACK HAWAKULENGA RANGI ZETU WALIMAANISHA UBONGO MWEUSI.
 
Kwani mtukufu rais anasemaje? In tz it is one man's (de president) show that works. Hayo mengine mnayoyaita sijui sheria sijui katiba ni viini macho hata mkiandika kitabu chenye kurasa millions ya hayo mnayo yahubiri kuwa ni sheria kamwe hayatakuja kuwa na mashiko hapa kwetu bongolala!!
 
Africa bana...tunasafari ndefu sana, lengo lenu ni lipi hasa kuhakikikisha usalama wa mtumiaji wa simu au kupunguza idadi ya simu cards ambazo raia wanaweza kutumia kwa utashi wao?

Kwa nini kama issue ni usalama msiache mtu atumie laini zozote kwa idadi yoyote cha msingi isajiliwe..shida ni nini hapa?? Teknologia hamna au ni nini? Na kama basi kitu kama hicho kinatushinda tutawezafanya nini sasa?

Hao Maprof na Madotka wa falsafa katika masuala hayo wameshindwa kuwashauri cha kufanya.

AFRICA tuna safari ndefu sana na hatufiki leo wala kesho.

Nilipokua mdogo Miaka ya 90 nilifikiri kuwa Watu wakubwa wote wanaupeo, uelewa na akili sana kuhusu kila kitu.

Siku hizi nimegundua sio kabisa, Mtu anaweza kuwa mzee lakini ni mjinga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Meko anaogopa mitandao sana hadi Mwanae na yeye anataka kupambana na "JAMUHURI" ya Twitter .
 
Na Kama nilisajili laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja mfano Vodacom Tanzania kabla ya hio February 7, sihusiki kuchagua moja au nahusika.?

Msaada please.

Stay tuned [emoji6], Everything would be alright.
Naomba ufafanuzi kwenye hili swali maana tangazo halisemi chochote.
 
Hivi nani anajua kesho yake, kwani mtu akiwa na laini mbili au zaidi za mtandao mmoja zilizosajiliwa kwa alama za vidole, mamlaka husika zinapungukiwa nini, au ndo kusema kila mtu apate, "Ujamaalism" kwenye soko huria wa nini tena? Tunaimba kijamaa tunacheza kibepari, taabu tupu!
Kama mimi nilisajili laini mbili moja ni kwajili ya simu ya mkononi ya nyumbani kwajili ya mawasiliano na familia tunapokuwa kazini. Sijui hizi amri zinakaaje kaaje.
 
Jibu kwa kifupi, HAIWAHUSU.
Mko salama.
mimi nimesitishiwa huduma kwa line yangu moja ambayo sijaisajili kwa alama za vidole,na niliinunua na kuisajili kwa mujibu wa sheria ambazo zilikuepo kabla ya sheria tajwa ya feb 7
 
daah hii nchi yetu sometimes viongozi wanafanya maamuziua kif@ler sana, yaani tunarudishwa nyuma sana kwenye mambo ya teknolojia na hii awamu ya Mh. sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni mpya za usajili wa Laini za Simu za mwaka 2020 zimetangazwa kwenye Gazetti la Serikali la tarehe 7 February, 2020 kama Tangazo la Serikali No. 112 la 2020. Jina fupi (short title) la Kanuni hizo ni the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020.

Baadhi ya maswala kadhaa ambayo yamejitokeza katika Kanuni za Usajili wa Laini za Simu hizi mpya ni yafuatayo:

(1) Kwa sasa ni lazima kisheria kusajiri Laini ya Simu kwa alama za vidole.

(2) Usajili wa Laini ya Simu kwa alama za vidole utafanywa kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na NIDA pekee au Namba ya Kitambulisho cha Taifa na vitambulisho vingine kama vile kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva na passport havitatumika tena katika usajili wa laini za simu.

(3) Ni marufuku kwa mtu (binadamu) kusajili Laini ya Simu zaidi ya moja (1) kwenye mtandao mmoja wa simu kwa ajiri ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi (message), kuongea na data. Kwa mfano, ni marufuku kuwa na laini mbili au zaidi za Vodacom, unapaswa kuwa na laini moja tu ya Vodacom.

(4) Mtu anaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 4 kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na laini za simu nne (4) za Vodacom kwa ajili ya kutumia kwenye modem.

(5) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 30 kwa ajili ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi (message), kuongea na data.

(6) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi 50 kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki.

(7) Mtu ambaye anamiliki laini za simu mbili au zaidi za mtandao mmoja wa simu amepewa muda mpaka tarehe 30 June, 2020 kuchagua laini moja tu atakayotumia.

(8) Mtandao wa Simu unawajibika kuzima laini ya simu ambayo haijasajiriwa kwa njia ya alama za vidole.

(9) Kila laini ya simu lazima iwe na PIN (Personal Identification Number) ambayo lazima iwekwe kwenye simu au kifaa cha kieletroniki kila wakati simu inapowashwa au inapobadilishwa.

(10) Laini ya Simu isipotumika kwa siku 90 mfululizo lazima ifungwe.

(11) Taarifa yoyote iliyowasilishwa kwenye mtandao wa simu ikibadilika lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa ndani ya siku 14 zikiesabika tokea siku ambayo mabadiliko hayo yametokea. Kwa mfano, mtu akibadilisha jina au majina yake amabyo alisajiria laini ya simu kutoka na kuolewa lazima atoe taarifa ya kubadilisha majina yake kwenye mtandao wa simu ndani ya siku 14 tokea siku alipobadili jina.

(12) Ukitokea wizi au upotevu wa laini ya simu lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa Polisi.

(13) Ili mtu apewa laini mpya kutokana na upotevu au wizi lazima apeleke kwenye mtandao wa simu Loss Report au taarifa ya uchunguzi wa awali kutoka Polisi.

(14) Mtu ambaye atakiuka masharti yoyote ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu, 2020 atakuwa ametenda kosa la jinai na adhabu zake ni kifungo cha kuanzia mwaka 1 mpaka miaka 10 au fine kati ya Tsh 300, 000 mpaka Tshs 30 Million kulinga na kosa husika au vyote kwa pamoja kifungo na faini.

(i) Angalizo la Kwanza
Kabla ya tarehe 7 February, 2020 kurudi nyuma, sheria au Kanuni za usajiri wa Laini za Simu, 2018 zilikuwa zilimruhusu mtu kusajiri laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia vitambulisho vitano (5) vifuatavyo;

(a) Kitambulisho cha Taifa

(b) Kitambulisho cha Mpiga kura
.

(c) Leseni ya Udereva

(d) Passport

(e) Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi


Kwa msingi huu basi, ilikuwa ni kinyume na sheria kwa TCRA kuwalazimisha watu kusajiri laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha Taifa pekee kabla ya tarehe 7 February, 2020 kwa kuwa Kanuni hizi mpya zilikuwa bado hazijaanza kufanya kazi na hapakuwepo na sheria yoyote inayoweka sharti hilo kwa sababu sheria na Kanuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaanza kufanya kazi au kutumika na kuwa na nguvu ya kisheria (force of law) baada ya kutangazwa kwenye Gazetti la Serikali, ili nitakwa la Kifungu cha 14 na 37 (1) (a) cha Sheria ya Tafsiri, Sura ya 1, Toleo la 2002. Hivyo basi Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu za mwaka 2018 yaani the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2018 (Tangazo la Serikali Na. 18 la 2018) zilifanyakazi kuanzia tarehe 2 February, 2018 mpaka tarehe 6 February, 2020. Maana yake ni kwamba raia wa nchi hii walikuwa na haki ya kusajiri Laini za Simu kwa alama za vidole kwa kutumia mojawapo ya vitambulisho vitano (5) vilivyoainishwa hapo juu ikiwemo kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva na passport mpaka tarehe 6 February, 2020.


(ii) Angalizo la Pili
Hizi kanuni hazina kitu kinaitwa Retrospective Operation or effect kwa maana ya kwamba hazifanyi kazi kwa kurudi nyuma bali zinafanya kazi kwa kwenda mbele kwa maana ya kuwa zitatumika kwenye Laini za Simu ambazo zitasajiriwa kuanzia tarehe 7 February, 2020 tu kwenda mbele yaani hizi kanuni zina fall kwenye category ya prospective operation. Kwa, maana hii, mtu ambaye alisajiri laini yake ya simu kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga Kura au Leseni Udereva au Passport kabla ya 7 February, 2020 haguswi na kanuni hizi katika sheria.

Hivyo, basi itakuwa kinyume na sheria na itakuwa uvunjifu wa sheria kwa TCRA au Mtandao wa Simu kama Vodacom, Tigo na Airtel kufunga laini ya mteja ambaye alisajiri laini yake kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni Udereva au Passport kabla ya tarehe 7 February, 2020. Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na ya Afrika Masharriki (Defunct) mara kadhaa katika kesi kadhaa iliweka msimamo thabiti kuwa sheria inayogusa haki za msingi (substantive law) haiwezi kufanya kazi kwa kurudi nyuma (it cannot operate retrospectively) isipokuwa pale ambapo imetamkwa bayana bila utata wowote kuwa itafanya kazi kwa kurudi nyuma na msimamo huu uliwekwa na mahakama tajwa katika kesi zifuatazo, among others;

(i) S.S Makorongo Vs Severino Consigilio [2005] EA 247

(ii) Municipality of Mombasa Vs Nyali Ltd (1963) E. A. 371

(iii) Bidco Oil and Soap Ltd Vs Commissioner General Tanzania Revenue Authority, Civil Appeal No. 89 of 2009

(iii) Gaspar Peter Vs Mtwara Urban Water Supply Authority (Mtuwasa) Civil Appeal No. 35 of 2017

Kanuni za Usajili wa Laini za Simu za mwaka 2020 zinagusa haki za msingi (substantive law) za raia kuhusu swala la kuwasiliana au haki ya kuwasiliana ambayo ni haki ya kikatiba na kisheria, hivyo basi, kanunu hizi haziwezi kufanya kazi kwa kurudi nyuma (it cannot operate retrospectively) kwa sababu katika kanuni hizi hakuna kanuni yoyote au masharti yoyote ambayo yametamka bayana bila utata wowote kuwa kanuni hizi za usajiri wa laini za simu za 2020 zitafanya kazi kwa kurudi nyuma. Hivyo basi, Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu za mwaka 2020 zitafanya kazi kwa kwenda mbele (prospectively) kuanzia tarehe 7 February, 2020.

Wenu Mwana JF Matojo M. Cosatta


Duuu, Mambo kibao.
 
Gazetti la Serikali, ili nitakwa la Kifungu cha 14 na 37 (1) (a) cha Sheria ya Tafsiri, Sura ya 1, Toleo la 2002. Hivyo basi Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu za mwaka 2018 yaani the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2018 (Tangazo la Serikali Na. 18 la 2018) zilifanyakazi kuanzia tarehe 2 February, 2018 mpaka tarehe 6 February, 2020.


Linauzwa wapi maana sisi wa vijijini halitufikii
 
Shukurani zimepokelewa kwa moyo mkunjufu.

Hii ya kumiliki line moja ya simu kwa mtandao mmoja tu, imekaa vibaya sana, yaani TCRA kweli you failed to know mtu mmoja kumiliki line zaidi ya moja kwa kampuni moja ya simu ni jambo la afya sana sanaa na mnazuia kweli?

Kwanza mtaua business za kampuni ya simu sana tu, pili mapato ya serikali yatashuka sana, na mbaya zaidi hamna sbb ya msingi kuzuia mtu kumiliki line zaidi ya moja kwa kampuni moja ya simu. Kama sbb ni uhalifu, hapo mmekosea, sbb uhalifu unaweza kudhibitiwa hata mtu akiwa na line zaidi ya moja ya kampuni moja ya simu.

Sioni sababu yoyote, mmepotea kabisa, nimesikitika sana kuona mmewaza poorly hivyo.
 
Back
Top Bottom