Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Kanuni mpya za usajili wa laini za simu: Masuala muhimu ya kujua

Kama mimi nilisajiri laini mbili moja ni kwajili ya simu ya mkononi ya nyumbani kwajili ya mawasiliano na familia tunapokuwa kazini. Sijui hizi amri zinakaaje kaaje.
Amri hizi mwisho wake ni mbaya kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kufikiri. Huu ni ulimwengu wa teknolojia ya hali ya juu lakini mtu fulani kwa sababu zake zisizo na mashiko ana amua umma uishi katika ujima (zama za mawe za kale) vile apendavyo bila kujali ni wangapi unaathiriwa na amri hizo.
 
mirisho pm,
Mbona walishalitolea ufafanuzi, kama ni mgeni ambaye, amekuja kwa muda na kupewa visa ya siku 90,ataweza kutumia passport yake kujisajiri, ili kupata line ya simu, ila kwa yule ambaye ana zaidi ya siku 90,labda yupo kimakazi, atatakiwa atumie passport na kibali cha kufanyia kazi kwenye usajiri
 
Kuzuia Uhalifu kila Raia anatakiwa awe na namba 1 tu ya mtandao 1 milele hata akifa iendelee kuwepo kama TIN ilivyo au namba za magari

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo wala sio hoja!! Kama ametumia usajiri wa alama za vidole hofu inatoka wapi? Nani alikuambia kuwa TIN haifi endapo mlipa kodi akifa?!!! Kama TIN, haipo active tu, inakufa sembuse mlipa kodi akifa?!! Vitu vingine jamani kabla hujaandika fikiria kwanza, hapa ni jf, sio fb
 
Mbona hakuna sehemu walizoongea kuhusu privacyy za mtumiaji?
Hawa wapumbavu wanajiangalia wao tu jinsi ya kuwabana wananchi waishi kama mshetani
 
Matojo Cosatta,
Kama hujaewa serikali inataka nini soma hapa:

Kwa miaka kadhaa serikal imekuwa ikipata shida sms mtandaoni facebook, instagram, twitter na hasa humu jamii forum ilikuwa ni shida sana kuwashika watuhumiwa hii ni kwa sababu usajili ulikuwa shaghalabagala.

Wakaona hapa ngoja tuikuze na tuipe nguvu TCRA wakaja na vidole finger print na hairuhisiwi mtu kutumia ID ya mwingine na picha si muda watawaforce mpige lengo lao ni kuwashughulimia akina mshana jr na CHADEMA maana huku mtandaoni kumekuwa kunazua chachu na hisia mara kadhaa Serikali inahofia hivi vitu vikiachwa tu kuna siku vitatoa effect
 
Matojo Cosatta, Nchi haiongizwi kwa sheria tu, ndugu kuna mila, tamaduni na miiko hivyo kuna mengine uache ubishi tu ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi wajibu wangu ni kuwambia sheria inasema na sio zaidi ya hapo, sasa nyinyi mkitaka kuongoza nchi kwa mila, tamaduni, miiko, utashi na hisia zenu bila kufuata sheria hilo liko mikononi mwenu.

Je, kuna mahali nimekosea kutoa elimu ya sheria kwa wana JF na Watanzania kwa ujumla kupitia Jamiiforums? bigmind
 
Mbona walishalitolea ufafanuzi, kama ni mgeni ambaye, amekuja kwa muda na kupewa visa ya siku 90,ataweza kutumia passport yake kujisajiri, ili kupata line ya simu, ila kwa yule ambaye ana zaidi ya siku 90,labda yupo kimakazi, atatakiwa atumie passport na kibali cha kufanyia kazi kwenye usajiri
Imeelezwa kwenye hiyo kanuni?
 
Kipengele cha tatu na cha nne naona kama vinakinzana, tushike lipi kati ya hayo mawili, au vifaa vya electronic na hizo Mashine haviwezi kutumia muda wa maongezi, data na sms Kwa pamoja?
There is no consistence
Mkuu, hata mie tangazo hili limenichanganya. Ilibidi niwapigie TTCL kupata ufafanuzi kwamba mie nina "lines" zao tatu, moja kwa 'smartphone', nyingine kwa 'wireless' na ya tatu ni 'data'.
Mdada akanithibitishia hiyo haina tatizo japo bado nina mashaka na hawa TCRA.
 
Hiyo wala sio hoja!! Kama ametumia usajiri wa alama za vidole hofu inatoka wapi? Nani alikuambia kuwa TIN haifi endapo mlipa kodi akifa?!!! Kama TIN, haipo active tu, inakufa sembuse mlipa kodi akifa?!! Vitu vingine jamani kabla hujaandika fikiria kwanza, hapa ni jf, sio fb
TIN haifi hata siku moja isipokuwa unaweza kwenda kuisimamisha...hata ukikaa miaka mingapi siku ya kwenda TRA itasoma palepale.
 
Mbona walishalitolea ufafanuzi, kama ni mgeni ambaye, amekuja kwa muda na kupewa visa ya siku 90,ataweza kutumia passport yake kujisajiri, ili kupata line ya simu, ila kwa yule ambaye ana zaidi ya siku 90,labda yupo kimakazi, atatakiwa atumie passport na kibali cha kufanyia kazi kwenye usajiri
So what is the point...
Kama Vitambulisho vingine vina we za kuwa na umuhim kwa mgeni kwanini sisi iwe lazima NID?
DL,Passport, havina umuhim wowote sio.

Na hoja ni kwamba kama tunatumia Finger prints kuna haja gani ya kuforce ID moja pekee....
 
hili tangazo mimi sijaliona. hata hivyo acha wafungie kwani wanamkomoa nani? kuna mambo mengi sana ya kufanya lakini serikali imekalia kufuatilia mawasiliano ya watu... hopeless kabisa.
 
Hamna namna zaidi ya kuwa raia wema
Naona tunaelekea zama zile ambazo uhalifu kupitia simu utakwisha ama kupungua kwa kiasi kikubwa sana
 
RENATUS GODIAN,
Kwahiyo njia rahisi ya kuwakamata wakosoaji na watukanaji wa mtandaoni ni kusajili kwa alama za vidole kweli,ina maana kwenye social network watu wanasajisajili kwa namba za simu peke yake
 
So what is the point...
Kama Vitambulisho vingine vina we za kuwa na umuhim kwa mgeni kwanini sisi iwe lazima NID?
DL,Passport, havina umuhim wowote sio....
Na hoja ni kwamba kama tunatumia Finger prints kuna haja gani ya kuforce ID moja pekee....
Mambo mengine ni utaratibu wa serikali, ulivyoweka, mfano mgeni, passport ndio id, inayoaminika sana, hadi kufika hapa, kwa sisi, inawezekana kuna vitambulisho vingi, tulishajisajiri kwa alama za vidole, mfano cha mpiga kura, lakini uratibu wake haukuwa mzuri sana, ndio maana wameona kitambulisho pekee ni cha NIDA,
 
Kwahiyo njia rahisi ya kuwakamata wakosoaji na watukanaji wa mtandaoni ni kusajili kwa alama za vidole kweli,ina maana kwenye social network watu wanasajisajili kwa namba za simu peke yake
Ata ukitumia email kujisajili io email huwezpata bila phone number ndugu take care database zinalink wjatever ni gmail with jamii forum au so zitalink tu mpaka wakudake na km ulimuomba mjomba sim wataanza na uyo uyo mjomba wako
 
Sasa ina maana hizo database za Facebook,twitter nk zitakuwa zinafikiwa na tcra ,kwa mtazamo wangu aliyeshauri kupambana na wakosoaji/watukanaji wa mtandaoni kwa kusajili line kwa alama za vidole hayuko vizuri kwenye mambo ya lT, labda kama anataka kuwakamata wale matapeli wa ile pesa tuma kwenye hii namba hapo sawa
 
(3) Ni marufuku kwa mtu (binadamu) kusajili Laini ya Simu zaidi ya moja (1) kwenye mtandao mmoja wa simu kwa ajiri ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi (message), kuongea na data. Kwa mfano, ni marufuku kuwa na laini mbili au zaidi za Vodacom, unapaswa kuwa na laini moja tu ya Vodacom.
Je hii ni busara? Mfano: Nachukua router ya Voda, kwa ajili ya intaneti ya familia kwangu nyumbani. Router inahitaji simcard. Sasa siruhusiwi kuwa na simcard ya Voda kwa ajili ya simu yangu??
 
Back
Top Bottom