Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Yaani, Katiba ya Tanzania itoe uhuru wa vyama vyote kushiriki uchaguzi, halafu miezi sita kabla ya uchaguzi tume ya uchaguzi ijifungie ndani na kuja na kanuni za kutakiwa kusainiwa kwanza na vyama vyote ili vyama hivyo vipate sifa ya kuja kushiriki uchaguzi miezi sita ijayo!
Tangu lini kusaini kanuni ndio kukawa msingi wa kuruhusiwa au kutokuruhusiwa kushiriki uchaguzi.
Chama chochote kwa wakati wowote kinapotaka kushiriki uchaguzi maana yake automatically kisheria kimeridhia kutekeleza masharti na kanuni zilizotengenezwa kuwezesha utekelekezaji wa sheria za uchaguzi.
Yaani vyama hata havijakaa kujadili na kupitisha kanuni zake za ndani za kushiriki uchaguzi, tume hata haijatangaza ratiba na taratibu za uchaguzi wa 2025, vyama vinaitwa kusaini maadili ya ushiriki wa uchaguzi na visivyofanya hivyo haziwezi kushiriki uchaguzi.
Nini kitatokea au kitapaswa kufanyika ikiwa Chama kilichosaini kanuni za maadili ya uchaguzi hapo baadaye kitagundua mapungufu ya hizo kanuni na kutokuzikubali?
Kanuni zinatengenezwa ili kurahisisha utekelezaji wa sheria za kikatiba na sio sharti la kulazimishwa kusainiwa kwanza ili kupata haki za kikatiba.