Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Huyo Thomas Sankara angekuwa msanii Ufaransa wasingehangaika kumtoa madarakani. Wangemuacha akae mwenyewe achoke kama walivyomuacha Paul Biya wa Cameroon. Lakini kwa sababu alikuwa kiongozi mzuri mzalendo ndio maana walihakikisha wanapatikana wasaliti wa kushirikiana nao ili Sankara aangamizwe. Na hata huyo Gaddafi angekuwa msanii NATO wasingejihangaisha kwenda kumuua.
Hao akina Sankara na dikteta Muamar Gadaffi waliuwawa na wananchi wao na ushahidi upo kabisa ila nyie waafrika hamkosi kutafuta visingizio kwa matatizo yenu mnayojiletea wenyewe.
 
Huyo Nyerere mwenyewe hakuwa mwanademokrasia kwakuwa kulikuwa na chama kimoja kipindi cha uongozi wake na alitawala kwa miaka 24.
Mbona una jibu tena zuri kabisa na ndio aliacha nchi ikiwa maskini wa kutupwa sasa na udikteta huo wa miaka 24 mbona hatukuendelea.

Ongezea na udikteta mwingine wa miaka 40 baada ya yeye kuondoka na Tanzania ndio kabisa imekua shithole country sasa ni udikteta gani huo wenye kuleta maendeleo. Bure kabisa.
 
Sasa wewe ulitaka nchi iendelee ndani ya miaka 24?
Halafu udikteta upi unaouzungumzia ndani ya hiyo miaka 40? Kungekuwa na udikteta hata Chadema wasingekuwepo bungeni.
 
Kwahiyo unataka utuambie Nyerere ndo kaanzisha mfumo wa elimu bure? Kweli story za vijiweni sio nzuri.
Bila Magufuli unafikiri leo tungekuwa na viwanda vya kusafisha dhahabu na Tanzanite au vile viwanda vya kuchakata samaki?
Hakuna haja ya kubishana na wewe, hakuna unachojua tofauti na ushabiki maandazi.
 
Sawa baki na demokrasia yako.
Ila kaa ukijua nchi nyingi zilizoendelea hazikufuata demokrasia kipindi cha maendeleo yake.
Waziri mkuu wa India kaingia madarakani toka 2014 na hana dalili ya kutoka leo India imepiga hatua.
Hiyo Marekani yenyewe Rais anajiamulia tarrifs atakavyo hakuna cha demokrasia hapo.
 
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.

Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo Jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia "Mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.

Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika "mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno "demokrasia"

Je, wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?

CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Yuko sahihi 100%. Demokrasia na maendeleo haviendani. Wajinga wanaweza kuwa wengi wakaamua upuuzi kwa sababu kwenye demokrasia ni WENGI WAPE. Kuna wapuuzi wengine husema SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU bila kujali hao wengi wanaweza kuwa wamekubaliana ujinga.
 
stupid as africans are... mpuuzi huyu anataka kutawala milele. WHY NOT DEMOKRASI? MBONA WESTERN WORLD AMBAO WANA DEMOKRASIA BY 100% WAMEEDNDELEA? see Denmark, Norway, and Sweden Finland ni democratic by 100% but highly developed first world! JINGA KUMBE NALO! lakini, ni mitulinga mingi akili kidogo...... NA YEYE ATAPINDULIWA
USA wana demokrasia gani wakati mshindi wa urais huchaguliwa na kundi dogo la watu wanaojiita Electoral College? UK nchi ya kifalme ina demokrasia gani? Nchi za Middle East na China hazina demokrasia, tumewazidi nini?
 
Hao akina Sankara na dikteta Muamar Gadaffi waliuwawa na wananchi wao na ushahidi upo kabisa ila nyie waafrika hamkosi kutafuta visingizio kwa matatizo yenu mnayojiletea wenyewe.
Waliuwawa na wananchi wake kwa ufadhili wa nani? Marco Rubio mwenyewe kwenye YouTube Channel yake hadi leo kuna video aliyoiweka siku Gaddafi alivyokufa anawapongeza Uingereza na Ufaransa kwa kufanikisha mauaji ya Gaddafi. Zile silaha waasi wa Libya walipewa na nani? Wenyewe NATO wanapongezana hadharani kwa kuhusika na mauaji ya Gaddafi halafu wewe unabisha unasema hawahusiki. Poleee
 
Mbona una jibu tena zuri kabisa na ndio aliacha nchi ikiwa maskini wa kutupwa sasa na udikteta huo wa miaka 24 mbona hatukuendelea.

Ongezea na udikteta mwingine wa miaka 40 baada ya yeye kuondoka na Tanzania ndio kabisa imekua shithole country sasa ni udikteta gani huo wenye kuleta maendeleo. Bure kabisa.
Vipi kuhusu udikteta wa Mao Zedong unavyowafaidisha China hadi leo hii? Udikteta wa mtawala wa Dubai? Qatar? Na we
 
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.

Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo Jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.

Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia "Mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.

Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika "mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno "demokrasia"

Je, wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?

CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)
Anachosema ni kweli kabisa; ila tatizo la kutokuwa na Democracy ni hulka ya wanadamu ya kutaka Uungu Mtu. Endapo Binadamu wangefuata kwa Ukamilifu Mafundisho ya YESU, ni kweli kabisa hayo anayoyasema. Tatizo la pili ni ubinafsi na kijicho cha wanadamu kwa wenzao walioko madarakani. Hili tatizo la pili ndilo ambalo naona litambadilisha FIKRA CAPT TRAORE. wale wasiomadarakani wataleta chokochoko hadi huyu bwana atajenga himaya ya kutaka aogopewe. Na hapo ndipo atakaporudi kule kule kwenye Uungu Mtu.
Mliisha sikia Yesu kukubali kuwa yeye atasimamisha Ufalme wa Mbinguni. Ila akakataa kuwa Ufalme wake siyo wa Ulimwengu huu. Utawala pekee utakaokidhi falsafa ya Traore ni Utawala wa Yesu, HIVI KARIBUNI- WEWE SHANGAA TU
 
Vipi kuhusu udikteta wa Mao Zedong unavyowafaidisha China hadi leo hii? Udikteta wa mtawala wa Dubai? Qatar? Na we
Tunaongelea Afrika, udikteta wetu ni wa enzi na enzi lakini kila uchao tunaendelea kuwa maskini.
 
Sawa baki na demokrasia yako.
Ila kaa ukijua nchi nyingi zilizoendelea hazikufuata demokrasia kipindi cha maendeleo yake.
Waziri mkuu wa India kaingia madarakani toka 2014 na hana dalili ya kutoka leo India imepiga hatua.
Hiyo Marekani yenyewe Rais anajiamulia tarrifs atakavyo hakuna cha demokrasia hapo.
Hivi wewe hoja yako ni nini haswa. Afrika ndilo bara linaloongoza kwa udikteta duniani kwa maana ya toka enzi za machifu hadi leo na ndio maendeleo yamegoma, sasa wewe unataka udikteta wa aina gani tofauti na huu ambao umekuwepo tangu enzi na enzi..😛😛😛😛
 
USA wana demokrasia gani wakati mshindi wa urais huchaguliwa na kundi dogo la watu wanaojiita Electoral College? UK nchi ya kifalme ina demokrasia gani? Nchi za Middle East na China hazina demokrasia, tumewazidi nini?
Wewe ndio kabisa hakuna unachojua na inaonekana hauna elimu nzuri ya kuweza kutambua mambo, nyie ndio wale wa kukariri vitabu vya imani.

You're a believer in dogmas.
 
Sasa wewe ulitaka nchi iendelee ndani ya miaka 24?
Halafu udikteta upi unaouzungumzia ndani ya hiyo miaka 40? Kungekuwa na udikteta hata Chadema wasingekuwepo bungeni.
Kwa hiyo kwa akili zako wewe demokrasia ni Chadema kuwa bungeni..!!

Kwa huo udikteta mnaoutamani mimi ningekuwa rais ningepiga marufuku hizo elimu feki za kukariri imani za kale ili watu mfanye kazi mkiwa na akili za kujitambua na muda mwingi ungekuwa ni wa kufanya kazi na kama ni kusali ni usiku tu kabla ya kulala.

Mambo mengine hayo ya kijinga hamna na kwa njia hiyo naweza ninakubaliana nanyi kwamba udikteta unahitajika ili watu wafanye kazi na kuzingatia utamaduni wao na kuachana na tamaduni za kigeni.
 
Hivi wewe hoja yako ni nini haswa. Afrika ndilo bara linaloongoza kwa udikteta duniani kwa maana ya toka enzi za machifu hadi leo na ndio maendeleo yamegoma, sasa wewe unataka udikteta wa aina gani tofauti na huu ambao umekuwepo tangu enzi na enzi..😛😛😛😛
Hivi wewe unajua hata maana ya udikteta?
Bara linaloongoza kwa uditekta duniani ni Asia kwakuwa nchi nyingi za Asia zinaongozwa na wafalme ukienda uarabuni, Japan , Thailand hizo zote zinaongozwa na wafalme. Ongeza na China yenye chama kimoja na India iliyompa mamlaka waziri mkuu wake kutawala kipindi atakacho.

Halafu kuhusu bara la Afrika kuongozwa na machifu zamani hata Ulaya enzi hizo ilikuwa inaongozwa na wafalme. Enzi hizo uditekta ulikuwepo kila sehemu sio tu Afrika.
 
Sasa wewe unafikiri kungekuwa na uditekta nchi hii kungekuwa na vyama vingi?
Unajua hata Ujerumani ya Hitler ilikuwa na vyama vingi kama wewe kwa akili zako unafikiri kuwa na vyama vingi ndio demokrasia na hata Rwanda kuna vyama vingi.

Tatizo linalosumbua wengi humu ni kwamba hawaelewi nini maana ya demokrasia ila wame karirishwa tu maana kwamba ni kuwepo kwa vyama vingi na uchaguzi.

Hawajui kwamba uwepo wa vyama vingi sio hoja kwani vinaweza vikawa ni vyama 30 lakini vilivyoundwa na mtawala na uchaguzi ni yeye ndiye anayeamua wagombea halali na wasio halali na ni yeye ndiye anayehesabu kura na kutangaza mshindi.

Lakini kwa wajinga utasikia wanasema hiyo nchi ina demokrasia kisa wana utitiri wa vyama feki vinavyo ruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi feki. Bure kabisa.
 
Hivi wewe unajua hata maana ya udikteta?
Bara linaloongoza kwa uditekta duniani ni Asia kwakuwa nchi nyingi za Asia zinaongozwa na wafalme ukienda uarabuni, Japan , Thailand hizo zote zinaongozwa na wafalme. Ongeza na China yenye chama kimoja na India iliyompa mamlaka waziri mkuu wake kutawala kipindi atakacho.

Halafu kuhusu bara la Afrika kuongozwa na machifu zamani hata Ulaya enzi hizo ilikuwa inaongozwa na wafalme. Enzi hizo uditekta ulikuwepo kila sehemu sio tu Afrika.
Huna hoja ni kelele tu.
 
Back
Top Bottom