Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Watukodishie aiseee..!!
Hata nyuzi za kichawa humu zitapungua..!

Kabisa, kodi itatumika vizuri huduma zote za serikali zitatolewa, mafisadi watanyongwa, huduma za serikali zitaboreshwa kama elimu, afya, ardhi, mazingira ya biashara.
 
Umenichekesha sana.
England, France, Holland ,Russia, Spain na Italy hizi zote zilitawaliwa na wafalme huko nyuma na bado England, Spain na Holland zinatawaliwa na wafalme hadi sasa bila kusahau UAE nchi zake hazifuati demokrasia na zimeendelea tukienda Canada, New Zealand na Australia hizi ni dominion za King Charles na zimepiga hatua.

Naungana na Rais wa Burkinafaso.

Pole sana mkuu
 
Huyu jamaa ni dikteta. Ila wabongo wanaojifanya wanapinga udikteta wanamshangiria.
Nani huyo? Kwanini unafikiri ni dikteta, udikteta ni nini? Baba yako ni dikteta kwenye familia yenu? Kiongozi wa ukoo wako? chief wa ukoo? Kwanini unakubali amri za baba yako kwa sababu unajua deep down ana nia njema na wewe. Anataka ufanikiwe. Benevolent dictator. Sio madikteta wote ni wabaya.

Ila wengine ni wabaya kama huyu tuliyenaye sasa, anaowapendelea mafisadi na kutokemea rushwa, ufisafi, wizi, report ya madudu ya CAG. Hana any idea, clue, vision, seriousness kwanini anataka kubaki kuwa rais zaidi ya kutanua.

Benevolence dictatorship ni mfumo Waafrika, binadamu na Mungu wameutumia toka dunia iumbwe. Jamii imebaki salama hadi leo. Neno moja tumeletewa Afrika miaka demokrasia linatuchanganya hadi leo.
 
Hao ni wasanii tu hawana lolote. Populist leaders.
Kama Gaddafi alikuwa msanii unafikiri wangemuua?
Hao leaders ni popular kwasababu walikuwa wanafanya mazuri kwenye nchi yao ndo maana hadi leo waaimbwa.
Leo ukiachana na Gaddafi rais yupi mwingine wa Libya unayemjua?( Bila kusearch mtandaoni)
 
We unauhakika gani yale maghorofa ni ya Magufuli? Wewe mke wake au mtoto wake? Hayo magorofa hayana majina?

Tangu Magufuli aondoke mashirika ya serikali na bandari wanapewa wachina na waarabu. Hivi unafikiri Magufuli angekuwepo vijana wetu wangeambiwa wakasome Veta? Yule mzee alikuwa anaanzisha viwanda kila kukicha.
Unafikiri asingeanzisha elimu bure tungekuwa na wasomi wengi?

Nyie mnachokiona ni fisadi na ditekta mengine mnayafumbia macho mtafikiri hamuoni AIR TANZANIA na miundombinu aliyoiweka.
Wewe kama uchawa wako kwake unakufanya usifamu ufisadi alioufanya basi hiyo ni shauri yako na wakati wake ndipo ilipoanzishwa "Control Number" feki zinazotumika kuiba fedha za umma hadi leo.

Hivyo viwanda alivyoanzisha kila uchao viko wapi labda wengine tumepigwa changa la macho hatuvioni.

Mimi nafahamu wakati wa Nyerere ndio watu walisoma bure na labda wewe hukuwepo wakati huo lakini sio wakati wa dikteta Magufuli.
 
Kama Gaddafi alikuwa msanii unafikiri wangemuua?
Hao leaders ni popular kwasababu walikuwa wanafanya mazuri kwenye nchi yao ndo maana hadi leo waaimbwa.
Leo ukiachana na Gaddafi rais yupi mwingine wa Libya unayemjua?( Bila kusearch mtandaoni)
Gaddafi huyo mambo mengi amepakaziwa tu na wala hakuyafanya hayo na wajinga ndio wanadanganywa lakini pia alichukua mabinti za watu akawafanya walinzi wake huku akiwala kingono japo hilo magaidi hamtaki kabisa kuliongelea. Wanafiki wakubwa.
 
Wazo, asirudie tena kualika wachezaji wa zamani waliocheza ulaya kucheza nao mpira pamoja, asirudie...... Itamcost anawindwa sn kaweka mchanga kwenye kitumbua cha western countries
 
Wewe kama uchawa wako kwake unakufanya usifamu ufisadi alioufanya basi hiyo ni shauri yako na wakati wake ndipo ilipoanzishwa "Control Number" feki zinazotumika kuiba fedha za umma hadi leo.

Hivyo viwanda alivyoanzisha kila uchao viko wapi labda wengine tumepigwa changa la macho hatuvioni.

Mimi nafahamu wakati wa Nyerere ndio watu walisoma bure na labda wewe hukuwepo wakati huo lakini sio wakati wa dikteta Magufuli.
Kwahiyo unataka utuambie Nyerere ndo kaanzisha mfumo wa elimu bure? Kweli story za vijiweni sio nzuri.
Bila Magufuli unafikiri leo tungekuwa na viwanda vya kusafisha dhahabu na Tanzanite au vile viwanda vya kuchakata samaki?
 
Gaddafi huyo mambo mengi amepakaziwa tu na wala hakuyafanya hayo na wajinga ndio wanadanganywa lakini pia alichukua mabinti za watu akawafanya walinzi wake huku akiwala kingono japo hilo magaidi hamtaki kabisa kuliongelea. Wanafiki wakubwa.
Hebu niambie hayo mambo ambayo Gaddafi amepakaziwa halafu una uhakika gani Gaddafi aliwala mabodyguard wake au ulikuwa mmoja wao?
 
Mimi nafahamu wakati wa Nyerere ndio watu walisoma bure na labda wewe hukuwepo wakati huo lakini sio wakati wa dikteta Magufuli.
Huyo Nyerere mwenyewe hakuwa mwanademokrasia kwakuwa kulikuwa na chama kimoja kipindi cha uongozi wake na alitawala kwa miaka 24.
 
Hao ni wasanii tu hawana lolote. Populist leaders.
Huyo Thomas Sankara angekuwa msanii Ufaransa wasingehangaika kumtoa madarakani. Wangemuacha akae mwenyewe achoke kama walivyomuacha Paul Biya wa Cameroon. Lakini kwa sababu alikuwa kiongozi mzuri mzalendo ndio maana walihakikisha wanapatikana wasaliti wa kushirikiana nao ili Sankara aangamizwe. Na hata huyo Gaddafi angekuwa msanii NATO wasingejihangaisha kwenda kumuua.
 
Yeye namuelewa wala s9mshangai kwa sababu ana tamaa ya madaraka ana kitu anatafuta.

Nisiowaelewa ni hawa misukuke wa Afrika wanaomshangilia.

They are cheering for a tyrant.

Mkuu africa kuna watu wapumbavu sana
 
Ameanza kuutaman Ufalme dogo janja, Atarambishwa asali kwa kisu anyonge awashe kisha avute.
 
stupid as africans are... mpuuzi huyu anataka kutawala milele. WHY NOT DEMOKRASI? MBONA WESTERN WORLD AMBAO WANA DEMOKRASIA BY 100% WAMEEDNDELEA? see Denmark, Norway, and Sweden Finland ni democratic by 100% but highly developed first world! JINGA KUMBE NALO! lakini, ni mitulinga mingi akili kidogo...... NA YEYE ATAPINDULIWA
Walianza kuendelea kabla ya democracy
 
Back
Top Bottom