Deinstein 01
JF-Expert Member
- May 12, 2024
- 2,090
- 3,928
We unauhakika gani yale maghorofa ni ya Magufuli? Wewe mke wake au mtoto wake? Hayo magorofa hayana majina?Demokrasia ipi unayoiongelea Tanzania...!!??
Toka nchi hii ipate uhuru hadi leo demokrasia umeiona wapi wakati ccm ndio inatawala kwa mkono wa chuma na tena wenyewe wanakiri wazi kwamba haiwezi ikaondolewa madarakani kwa vipande vya makaratasi.
Afrika hakujawahi kuwepo demokrasia na ndilo bara linaloongoza kwa umaskini uliokithiri duniani.
Magufuli mnayemsema kuna magorofa anayo pale Mwanza na aliyapataje kwa kipato chake halali..!!?? Yaani ufisadi mtupu.
Tangu Magufuli aondoke mashirika ya serikali na bandari wanapewa wachina na waarabu. Hivi unafikiri Magufuli angekuwepo vijana wetu wangeambiwa wakasome Veta? Yule mzee alikuwa anaanzisha viwanda kila kukicha.
Unafikiri asingeanzisha elimu bure tungekuwa na wasomi wengi?
Nyie mnachokiona ni fisadi na ditekta mengine mnayafumbia macho mtafikiri hamuoni AIR TANZANIA na miundombinu aliyoiweka.