Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Hivi Tanzania Kuna demokrasia au maneno tu?
Ukiwauliza Demokrasia ni nini? Wengi hawawezi kujibu.

Ila kimsingi demokrasia ni kutekelezwa kwa matakwa muhimu ya msingi ya wengi kwenye Taifa kama kupata huduma za afya, elimu, kusikilizwa na serikali, kuondoa rushwa, ufisadi, uwajibikaji.

Yote hayo yatatimia kama haki ya kuongea itakuja automatically. Raia wengi tayari watakuwa wasomi, wanajitambua ukiwapa huduma zao za msingi. Kuna vitu inabidi vije, vianze kwanza.
 
Baada ya mtafaruku wa Trump- Zelensky, siamini kama Afrika bado haijafunguka macho na kuelewa kuwa -UHURU MNAOFIKIRI MNAO, HAMNA. Huwezi ukazungumzia Demokrasia wakati bado mnatawaliwa. Kama Zelensky kakomaliwa kiasi hicho na ni mwenzao, vipi wewe wa bara la Afrika Mfano- Kongo DR. Ukadhani mkataba wa madini wa Kongo na Amerika utakuwa mzuri kuliko ule wa Ukraine na Amerika. Msijidanganye!
 
Hizo nchi zote ulizotaja hazina Marais zote zinaongozwa na wafalume ambao hawatoki madarakani !!! Chaguzi zinazofanywa ni Kwa nafasi ya mawaziri wakuu TU !!! Hapo kunademokrasia ??? Nchi chache saana ulaya zenye mkuu wa inchi ambaye ni president nyingi zinaongozwa na falume zao
Mfalme analindwa milele yeye na familia yake. Ndio kiongozi mkuu wa nchi. Waziri mkuu lazima aende kumuona kabla ya kupata idhini mamlaka ya kuongoza. Lazima akitutane na waziri mkuu kila wiki.

Waziri amwambie mipango yote ya serikali yake. Unafikiriki nani ana mamlaka?

Kumbuka huu mfumo ulianzishwa baada ya wananchi kudai haki zao UK, kabla ya hapo miaka 300 iliyopita wananchi wa kawaida hawakuwana haki yoyote hata ya uwakilishi popote.

Kulikuwa na mfalme na house of Lords, wamiliki wakubwa wa ardhi UK.


Baadaye sana Labour Party (chama cha wafanyakazi, walalahoi), house of commons zikaanzishwa kupigania maslahi ya watu wa kawaida walio wengi. Kwahiyo hata maskini wengi UK, France, USA wazungu, weusi, wanawake hawakuwa na haki, uwakilishi wowote kwa miaka mingi sana.
 
Demokraeia ni kupata kile unachokitaka even kwa Gharama za watu wengine.
Ni picha la uongo linalochorwa kwenye sura ya ukweli usiokuwepo.
Ni chai Kama chai zingine.
 
demokrasi....must prevail
Demokrasia ni greek word. Kiswahili ni haki ya wengi, nguvu ya wengi.

Hivi hapa Tanzania ukitaka kuzungumzia haki ya wengi unaanza na nini? kodi zetu zinavyotumika, huduma unazozipata, unasikilizwa na wanaotumia pesa yako kuishi.

Utamaduni wa Afrika kiasili uko kidemokrasia. Jamii, kabila, ukoo, Ufalme ulihakikisha kila mtu yupo vizuri kabla hata ya wakoloni.
 
Huyo ni jobless mmoja, anafikiri usomi ni kupinga kila kitu anachofanya Muuafrika, aki-qoute upuuzi wowote walioandika wazungu bila kutumia ubongo wake.

Ad hominem fallacy.

Thibitisha mimi ni jobless.
 
Kiranga unashambuliwa huku, kuna ukweli wowote juu ya haya yaliyoandikwa?
Ad hominem fallacy.

Nimemwambia athibitishe mimi ni jobless.

Halafu wabongo wanaona kuwa na kazi ndiyo kuukata, wakati huku kuna trust fund babies wana invest hela tu na kuishi kwa capital.

Ulimbukeni mtupu.
 
He! Bado unajilinganisha na western world?
Traora yupo sahihi. Demokrasia ndani ya Afrika na nchi nyingine masikini ni njia mpya ya western world na rafiki zake kuipangia nchi husika uongozi wanaoutaka wao, sio wananchi. Kumbuka uchaguzi katika demokrasia unahitaji pesa. Western world ndio sponsor wakubwa wa chaguzi hizo na kuwapa pesa vile vyama wanavyotaka vishinde. Na wakishindwa, watakuja na silaha mpaka wamuweke wanaomhitaji.

Mfano wa nchi ambazo Demokrasia imeshindwa na wanaungwa mkono na western world: Rwanda (Uchaguzi Rais hushinda kwa 97%- bomu), Uganda, Libya, Misri, Kameroun .............

Hitimisho: Urusi na China sio wajinga kutupilia mbali mpango wa kidemokrasia wa western.
Afrika: Hata baada ya miaka 100 mbele, demokrasia hii ya western haitatutoa katika umasikini, ujinga na vita. Kama demokrasia, iwe na muundo mwingine wa Kiafrika na sio kuiga huu wa western.
ACT wamepokea mapesa ya Ford Foundation kupitia taasisi ya Twaweza . Baada ya kupokea hayo mabilioni wameanza kampeni ya linda demokrasia. Jiulize, ACT wamewaahidi nini Ford Foundation hadi wakapewa hayo mahela maana hapa duniani hakuna cha bure? Kingine mfano ACT ndo wanashinda uchaguzi unadhani Rais atakuwa na ubavu wa kuwakatalia mabosi wa FORD Foundation chochote watakachotaka kwenye nchi yetu? Ndio yanayotokea kwa Ruto sasahivi analipia pesa za waarabu kwa kuwahifadhi RSF ( Janjaweeed) kutoka Sudan nchini kwake. Janjaweeed wanaobaka na kuua watu weusi . Yaani Ruto anawahifadhi magaidi ambao mapepo yao yakipanda wanaweza kuua wakenya maana wenyewe wanachukia watu weusi balaa. Hiyo ndo demokrasia??
 
ACT wamepokea mapesa ya Ford Fondation kupitia taasisi ya Twaweza . Baada ya kupokea hayo mabilioni wameanza kampeni ya linda demokrasia. Jiulize, ACT wamewaahidi nini Ford Fondation hadi wakapewa hayo mahela maana hapa duniani hakuna cha bure? Kingine mfano ACT ndo wanashinda uchaguzi unadhani Rais atakuwa na ubavu wa kuwakatalia mabosi wa FORD Foundation chochote watakachotaka kwenye nchi yetu? Ndio yanayotokea kwa Ruto sasahivi analipia pesa za waarabu kwa kuwahifadhi RSF ( Janjaweeed) kutoka Sudan nchini kwake. Janjaweeed wanaobaka na kuua watu weusi . Yaani Ruto anawahifadhi magaidi ambao mapepo yao yakipanda wanaweza kuua wakenya maana wenyewe wanachukia watu weusi balaa. Hiyo ndo demokrasia??
Ruto amenishangaza sana kuwakumbatia RSF kuwalinda na kuwapa makao makuu Nairobi. Ni kama hataki mgogoro dishes Sudan.

Wengi wametekwa akiwa rais wapinzani wa Nigeria, Uganda. Oman, ncbi nyingi kuliko wakati wa uhuru. Alikuja akisema anatasaidia vijana wasio na ajira kupinga ufisadi. Yeye amekuwa fisadi mkuu.

ACT ni wahuni, wachumia matumbo yao, ruzuku. Report ya CAG kimya, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kimya. Linganisha kelele zao 2015 - 2020 na 2021 - 2025.
 
Ruto amenishangaza sana kuwakumbatia RSF kuwalind na kuwapa makao makuu Nairobi.

Wengi wametekwa akiwa rais wapinzani wa Nigeria, Uganda. Oman, ncbi nyingi kuliko wakati wa uhuru. Alikuja akisema anatasaidia vijana wasio na ajira kupinga ufisadi. Yeye amekuwa fisadi mkuu.

ACT ni wahuni, wachumia matumbo yao, ruzuku. Report ya CAG kimya, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kimya. Linganisha kelele zao 2015 - 2020 na 2021 - 2025.
Ruto analipia pesa za waarabu. Na sio yeye tu, mwanasiasa yoyote lazima alipie fedha za wanaomfadhili wakati wa kampeni na uchaguzi. Kwahiyo tunavyohubiri demokrasia tusisahau kuwa mabosi wa viongozi tunaowachagua sio sisi bali ni wafadhili wanaowapa pesa za kampeni
 
Mkuu, kwa hilo juu kuhusu kusalitiwa na viongozi wenzake ninalitilia mashaka,

Viongozi wepi hao?


Haki☝🏿Sidhani hilo juu lina ukweli wowote ule.

...hulka za Mwafrika sio za kuishi na vinyongo- kuwashinda wazungu, they are more vengeful, than us bana, ni makatili pyu.

...naafiki, Waafrika wanajitambua kitambo sana, na sio kwamba tunawatizama/ hatuwatizami wazungu kama ni maadui.
Ni kiongozi gani wa Afrika
asiye mwanajeshi aliyethubutu kufanya aliyofanya Traole na majirani zake wa Mali,na Niger,
kwa muda mfupi ikiwemo kufuta madeni yote,kujenga viwanda,kufunga military bases,kuanzisha mashamba,nk??

Manabii/mitume wa Afrika huwa hawakubaliki nyumbani kwao
!!
 
Kabisa unafikiri ukimpa Tanzania huyu kijana miaka mitano, kumi nchi hii itakuwa wapi, atacheke na mwijaku, babalevo na wahuni wengine kama hawa.

Atakuwa kazini.kupiga kazi kuhakikisha kuna umeme, maji, huduma zote muhimu kama afya, elimu, ajira, kazi makazi, mazingira rafiki ya biashara kwa wote, nidhamu serikalini, kuondoa rushwa, ufisadi.

Pesa ya nchi haitatumika kwenye matamasha, ufisadi, machawa.
Watukodishie aiseee..!!
Hata nyuzi za kichawa humu zitapungua..!
 
Unafikiri Ufaransa kama ufaransa ilianzishwa kwa demokrasia. Napoleon Bonapatre alipindua serikali na ufalme na kumuua mfalme, Uingereza walikuwa na civil wars, Spain, Portugal, USA. Sweden, Norway, Denmark zamani walikuwa majambazi wamejikita kwenye uporaji. Baadaye wakapata empires, mwisho miaka kama 200 hivi iliyopita ndio wamestaraabika.

USA, UK. France, Spain, Portugal, Germany wote wanahubiri demokrasia ila vyote wameanz a uvifanya 1960's.

Lazima mtu ajenge misingi imara kwa muda wa kutosha.
Kama mnataka kupita njia waliyopita hao ina maana mnataka na sisi tupinduane, na kuuana ili tuje kufika huko kwenye hiyo demokrasia!? Ni nini hasa unachojaribu kusema hapa!?
 
Kama mnataka kupita njia waliyopita hao ina maana mnataka na sisi tupinduane, na kuuana ili tuje kufika huko kwenye hiyo demokrasia!? Ni nini hasa unachojaribu kusema hapa!?

Sio lazima kuuana mapinduzi ina maana unaondoa utawala uliopita mbovu uliokuwa kwa maslahi ya wachache , unakuja na utawala mpya in theory utakaotenda haki kwa wote.

Mapinduzi ya Zanzibar yaliondoa serikali ya Wachache na kusimamia maslahi wengi. Kuna watu walikufa ili wengi waishi, keki igawanywe kwa wengi, Taifa.

Bara tuna kitu kinaitwa chama cha mapinduzi (CCM). Hakijawahi kupindua serikali yoyote. Walizungumzia mtazamo mpya, dira mpya, haki kwa wote, kuinua maisha ya watanzania wote. Katiba yao ni nzuri sana na waanzilishi walikuwa na nia njema sana. Ila kimegeuka chama cha wakandamizaji, chama cha wachache, chama kisichojali hata misingi yake.

Waanzilishi wanapiga kelele hawasikilizwi kama Warioba.
 
Huyu jamaa ni dikteta. Ila wabongo wanaojifanya wanapinga udikteta wanamshangiria.
 
Back
Top Bottom