Uchaguzi 2020 Karata ya mwisho ya CCM ni kuahirisha uchaguzi na sio kuiba kura

Uchaguzi 2020 Karata ya mwisho ya CCM ni kuahirisha uchaguzi na sio kuiba kura

Nimejaribu kujifanya mimi ni ccm damu damu nikapita mitaa miwili mitatu kupiga story na "wanangu" kuhusu "mafanikio" ya John, nikawaambia tarehe28 tumpe mitano tena! Loh kilichonitokea najuta hata maigizo niliyofanya! Nilitimuliwa mbio kama mwizi, nimerudi baadae kuja kuwaambia wanangu enh mimi mwenzenu bhana, nilikuwa natest tu zali kama huku kijijini napo hamumuelewi "dikteta", wana wamekuwa wagumu kunielewa mpaka imebidi niwaoneshe magroup yote ya whatsapp niliyopo kwenye simu na uchangiaji wangu, na vile mimi ni "poti" basi bado wana mashaka namimi kama kweli naweza kusapoti haki na usawa ambao tumekuwa tukiwanyima wananchi kwa kutumikishwa na majizi ya ccm
Heee! Wewe poti??
Bado sikuamnini hata sasa.
Nyie mapoti hamueleweki, yawezekana unajaribu kutuchota akili hapa.
Nyie mapoti mnalipwa vizuri ndo maana mnaona sawa tu.
 
Haya kura wamepiga na zinahesabiwa vipi nabii na matokeo pia unabashiri au tukuache
 
CCM ilianza mapema kutafuta kura, ilianza na mbinu ya kuzuia vyama vingine na wagombea wao kujitangaza akabaki Magufuli peke yake, ikaja na mbinu ya kununua wapinzani waliyoshauriwa na Polepole na KM Bashiru, CCM ikautumia uchaguzi wa serikali za Mitaa kuwahujumu wapinzani.

CCM walijua wagombea threat kwao ni Lissu na Seif wala sio Membe, ndio maana waliposikia Lissu atarudi na atagombea wakaanza kumtisha kuwa akifika ataishia gerezani au atauawa na mahasimu wake, wakasema hata akiteuliwa na chama chake NEC itamuengua, mbinu zote hizo zimeshindwa.

Ili kuwapunguza nguvu wapinzani NEC/ZEC wakaja na mbinu ya kuwaengua baadhi ya wagombea sasa wameaanza kuwazuia wasifanye kampeni, najua hii nayo itashindwa kama ilivyoshindwa ya kuwazuia wapinzani kwa miaka 5.

Safari hii chochote wanachokianzisha kinaonekana kushindwa ikiwa ni pamoja na kutoa matamko mbalimbali kupitia vyombo vya serikali.

Mbinu ya mwisho ya CCM ya kizamani wanayoitegemea ni kuiba kura, lkn nawatahadharisha CCM na NEC, safari hii zoezi hilo litakuwa gumu sana, daftari liko wazi kwenye mitandao wanachoongeza kinaonekana wazi kwa wananchi.

Jumuiya za kimataifa zinafuatia kwa karibu sana uchaguzi huu, wasifanye kosa hilo linaweza kubadili kabisa historia ya Tanzania.

Nimeshiriki chaguzi zote tangu za kuchagua Nyumba na Trekita baadaye ule wa Picha na Kivuli, binafsi naona Mbinu ya mwisho kabisa ambayo angalau itakuwa salama kwa CCM ni kuahirisha uchaguzi na kujipanga upya.
Karibu tena 2025 Magufuli hayupo duniani lazima Chadema mchukue nchi.
 
Back
Top Bottom