Karate ndio mchezo unaoweza kukuhakikishia safe self defense kwa zaidi ya 90%

Karate hamna kitu , wanaojua karate ni wachina tuuu , wabongo miili yenyewe ipo irregular shaped....mtu yupo kama pipa anatembea kama kono kono.....ukutane na vibaka wenye njaa Wana mapanga, visu na bisibisi wapo serious na kazi Yao ..aiseee labda ukutane na vibaka wa Dar sio Mura wa Tarime
 
Mkuu karate ni mazoezi na uzoefu ,unaweza kuwa mkanda wa juu na ukapigwa kizembe, mazoezi ,mazoezi ,practise ,practise ,practise mwanafunzi ni bora a practise ndio anakuwa na defense ,la sivyo unaweza pigwa tu kama kawa
 
Mkuu karate ni mazoezi na uzoefu ,unaweza kuwa mkanda wa juu na ukapigwa kizembe......mazoezi ,mazoezi ,practise ,practise ,practise.........mwanafunzi ni bora a practise ndio anakuwa na defense ,la sivyo unaweza pigwa tu kama kawa
Sasa mcheza karate gani asiye practise mazoez na kumite..? Kama yupo wa hivo ni mzembe tu
 
W
We tutu China hawachezi karate.....ao wakina Mura inategemea wanakutana na Nani....uku kwenu nyinyi waunga mboga lazima muwaogope
 
Wee jidanganye tuu, martial arts ( karate) hai furukuti mbele ya modern arts ( silaha), yaani mwisho wa siku mtu wa martial arts ni mbio tuu ndizo zita mwokoa toka kwa mtu wa modern arts!!
 
Sasa mcheza karate gani asiye practise mazoez na kumite..? Kama yupo wa hivo ni mzembe tu
Mimi nimekaa madogo zaid ya 2, kuna watu wanakuja siku ya mafunzo tu ,siku ya mazoezi na kumite hatuwaoni......na akifanya mazoez ni kidogo lakini wanatumia fedha au ushawishi fulani kupanda daraja.

Wengine wanataka mkanda tu ili wakaanzishe club zao chini ya wasaidizi ambao ndo wanafanya mafunzo.....


Kumite na mazoezi ,practise muhimu sana.

Ngoja nirudi kwenye fani ,nisimama hadi nimeanza kuwa na nyama uzembe.majukumu
 
Karate tamu japo sijajifunza effectively ni maeneo flani nami nikasema nijiunge but sio official

Sasa kwa zile Basic na kata mbili nilizo jifunza kiukweli naweza mkabili mzembe mzembe na nikamuweka chini vizuri.

Kuna teke moja ilo nalijubali Sana nafikiri linaitwa Yoko Geri kikome yaani unampiga MTU chuma wakati umeangalia mbele kwa kugeuka haraka.

Nilimtwika moja tu maeneo itovu jamaa akasema Basi baba pale ndy nikasema alaaaaa kumbe mzigo unapiga kazi
 
Daaah hayo sikuwahi kuyajua mkuu...maana mi sijafundishiwa dojo....kwakweli kareti bila mazoezi na kumite...unajitafutia kudhalilika siku ukikutwa na balaa mtaaani
 
Sasa iyo teke ukitaka imuingie mtu Inabidi ucheze nae alafu unavizia Kama unaangalia pembeni ivi ndo unaipiga....alafu Kuna moja iko kwenye taikwondo inaitwa bolley kick...aisee ina mvuto wa kimapenzi hatari...Yani ukiwa mbele ya demu wako afu Kuna fala kajipitisha ukiipiga ile lazima ukawekewe maji ya kuoga yaliyoungwa
 
Maigizo ya video yanawadanganya.
 
Mkuu juma mpemba kumite ni nini?
Ni rehearsal ya mapigano ya ukweli kwa wacheza Sanaa ya mapigano....yaani kupimana uwezo kwa Yale mliyojifunza...mnapigana kweli ila hakuna uadui ndani yake. ...faida ya kumite ni kuondoa uoga na kuleta confidence,,,kuweza kukamata vema uliyojifunza...na kushusha hasira na pressure pindi ukikutana na visanga vya kupigana mtaani
 
Ikoje hiyo mkuu...au ile ya kuswipe mtama wa kuzunguka...?
Hapana, katika Ong bak 1 wakati Tony jaa ana anacheza kata aliipiga pia ni moja ya kick inayotumika sana kwao ukiongeza na round horse + push kick ukitazama hata jeshini kwao katika sanaa yao huo mchanganyiko haukosekani.

Ukikuta kweli mtu ana mazoezi hizo teke ikipigwa kweli usogei.
 
Unajua Muay Thai imejaribu kuondoa techniques nyingi sana za hatari za Muay Boran yenyewe pure kwa ajili ya mashindano mpaka imekuja kutumiwa kama kick boxer.

Ila ile MuayBoran halisi kabisa (traditional) iliyotumiwa na jamaa kama sanaa ya kujihami vitani wakati wakipambania Uhuru imegawanyika ki kanda kwendana style zake.

Muay Chaiya, Muay Korat, Muay Lopburi na Muay Thasao ni style tofauti sasa wapo waliochanganya hizo sasa ukute huyo mtu anapractice na tae kwondo au krav maga HAFAII.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…