TANZIA Karatu: Padri Pamphilius Nada auawa na mtu anayedhaniwa kuwa na changamoto ya afya ya akili

TANZIA Karatu: Padri Pamphilius Nada auawa na mtu anayedhaniwa kuwa na changamoto ya afya ya akili

Padri ndie chanzo cha vifo vyote. Katoliki hawana maombi ya usiku wa saa hizo. Kufungua kwake mlango usiku ndio matokeo ya vifo.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Padre na Daktari lao moja!

Unaweza kuamshwa muda wowote kwa ajili ya kutoa Huduma kwa Wagonjwa!

Mpako wa Mwisho nk!!

Mungu ampe Nuru ya Milele!!
 
Kufungulia mtu usiemjua usiku ni Risk sana...bora umwambia akalale akutafute kukicha...
Siku ikifika hakuna ingekuwa!
Israel mtoa roho za watu alikuwa na rafiki yake!
Anapoenda kutoa roho za watu alikuwa anamuaga!
Siku hiyo alishinda nyumbani na kumueleza Rafikie kwamba leo haeñdi mbali!
Rafiki yake kutafakari akaona jirani na pale hakuna mtu mwingine ila yeye tu! Akajua kwa leo ni siku yake!
Akaenda kuinua chungu kikubwa akaingia ndani akajifunika nacho, ili kujificha israel ASIMUONE!
Kumbe siku yake Imefika!
Akakosa hewa akafa!
Simulizi tu mkuu!

R I P BABA![emoji120]
 
Karatu jana kuna jamaa saa saba usiku ameenda Kanisani kumgongea mlango Paroko amuombee, Paroko alivyofungua Kanisani jamaa aingie amuombee kumbe alikuwa na chuma akapiga sana. Paroko ameenda kufia Fame Medical.

Wananchi wenye hasira nao wamemuua Mtuhumiwa

----
Padri Pamphilius Nada wa Parokia ya Karatu amevamiwa na kuuwa na mtu ambaye anayedhaniwa kuwa hana akili timamu usiku wa kuamkia leo tarehe 19.7. 2023.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amina.

KAMANDA WA POLISI ARUSHA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema “Mtuhumiwa aliyemshambulia Padri kwa nyundo inadaiwa alikuwa na changamoto ya afya ya akili, naye alifariki baada ya kushambuliwa na Wananchi wenye hasira kali eneo la tukio.”
Mapadre sasa wawe wanafundishwa Karate.
 
chanzo cha kufahamu mtu mwenye matatizo ya akili alienda kwa paroko kutaka kuombewa saa 7 usiku ni kipi?? navyofahamu makazi ya paroko yanakuwa na walinzi kama siyo mlinzi napo hapa naomba kufahamishwa
Huyo jamaa alizuiwa na walinzi kuingia akarudi tena alfajiri ndio paroko baada ya kusikia mabishano akaja getini na kuamuru afunguliwe aingie ndio mbele ya safari padri akauawa.
 
Karatu jana kuna jamaa saa saba usiku ameenda Kanisani kumgongea mlango Paroko amuombee, Paroko alivyofungua Kanisani jamaa aingie amuombee kumbe alikuwa na chuma akapiga sana. Paroko ameenda kufia Fame Medical.

Wananchi wenye hasira nao wamemuua Mtuhumiwa

----
Padri Pamphilius Nada wa Parokia ya Karatu amevamiwa na kuuwa na mtu ambaye anayedhaniwa kuwa hana akili timamu usiku wa kuamkia leo tarehe 19.7. 2023.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amina.

KAMANDA WA POLISI ARUSHA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema “Mtuhumiwa aliyemshambulia Padri kwa nyundo inadaiwa alikuwa na changamoto ya afya ya akili, naye alifariki baada ya kushambuliwa na Wananchi wenye hasira kali eneo la tukio.”
Changamoto ya afya ya akili hapo imetumika kuficha tatizo
 
Back
Top Bottom