TANZIA Kardinali Pengo afariki Dunia akiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

TANZIA Kardinali Pengo afariki Dunia akiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Huyu ni mmoja ya nguzo za Ccm kuendelea kuwatawala kupitia dini imeondoka, kwa upande wa Roman Catholic Ccm kwa sasa haina pandikizi, waongeze nguvu zao Bakwata.

Tec ya sasa siyo ya Pengo, inakabia juu kabisa.

Ni wakati sasa wa Vatican kuachana na urasimu papa The holy see atoke Vatican aje kumzika Kadinali wake Tanzania.

Nina imani Papa leo bado ana nguvu kusafiri siyo issue kwake.
Sio rahisi sana pope kuja kumzika kadinali , hata pale Vatican makadinali wengi wanazikwa bila papa kuhudhuria sembuse kusafiri umbali mrefu namna hii.
 
Tunamshukuru Mungu kwa uhai wake. Kumbukumbu yake ikawe faraja kwa wote wenye kuhuzunika na msiba huu.
Tunaomba Mwenyezi Mungu aampe pumziko la milele na kumjalia furaha pamoja na watakatifu wake katika ufalme wake
 
Pumzika kwa amani mwadhama Kardinali Pengo. Tuonane mbinguni asubuhi iliyo njema.

=====

YAH: TANGAZO LA KIFO​

Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazieni kwamba leo tarehe 19/02/2026 saa 04:00 usiku huu mpendwa baba yetu Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Taarifa za mazishi zitawajia mara baada ya mipango kukamilika. Tumwombee apumzike kwa amani.

Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani; Amina.

Katika Kristo,

Thaddaeus S. Ruwa'ichi OFM Cap
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam

Raha ya milele umpe eeh Bwana. Na Mwanga wa Milele umwangazie. Apumzike kwa amani. Amina.
 
Back
Top Bottom