kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #21
Hebu niambie Mimi na wengine humu, Manara ameivunja kanuni gani ya TFF inayotoa adhabu ya vile? Yaani ukichunguza adhabu Ile ni cumulative. Imekusanya vionjo viingi ambavyo vimewekwa pamoja na kufunikwa shuka moja TU la Manara kazozana na Karia.Kuweni makini sana, unaweza jikuta unamsapoti mjinga bila kujua, malalamiko kuhusu Karia yote ni ujinga mtupu.
Adhabu Ile imelipia na wengine kama Barbara, mo, coastal Union na hata Simba yenyewe. Lakini Karia na Manara ni watu wadogo sana kuliko mpira wetu na Tanzania. Watanzania wanataka mpira wao uchezwe wafurahi na wengine wapate kipato. Utani wa Simba na Yanga ndio mpira wenyewe wa Tanzania, hivyo yeyote atakaeikosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya Simba na Yanga atakuwa amekusudia kuukosea mpira wa Tanzania. Atakuwa ameonheza maadui zake kila Kona hata uvunguni mwa kitanda chake.