Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kuna bodaboda mbili zilipita speed kwenda uelekeo wa mtaa wa Lindi na Livingstone, kumbe bwana walikuwa wanamkimbiza mhindi aliyekuwa kwenye bodaboda nyingine ya mbele akiwa na begi mgongoni, inasemekena ni mauzo ya dukani.

Basi nikasikia puuu, kugeuka nikaona ile bodaboda ya Mhindi ipo chini, na zile bodaboda zilizomgonga mmoja wao akashuka na kuanza kukata mikono ya begi kwa kisu, mhindi akang’ang’ani begi, maumivu ya kisu yalipozidi Mhindi akaachia begi, jamaa akapanda kwenye pikipiki wakaamsha, halafu eti watu wanaangalia tu.

Mi nilitaka kwenda ila nikaona wale jamaa ile mibisu yao sio ya kitoto, wameanza kuondoka watu ndio wanajidai kuwakimbiza, wakatokomea kupitia pale kona ya Azam, Livingstone pale.

Hadi sasa hali ni tete, polisi wawahi hapo kuchukua maelelezo.

======================

Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New Tahery Stores’.
 
62B58CDC-8E79-4339-9DC1-C4F3D96E38DE.jpeg
 
Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.

Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana, akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana.
 
Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New tahery stores’.
 
Walikata vipi muhindi mikono kwan muhinndi begi si liko mgomgoni au alijifungia nalo
 
Walikata vipi muhindi mikono kwan muhinndi begi si liko mgomgoni au alijifungia nalo
Kwanza nilipoangalia nilihisi ni msamaria mwema anajaribu kumuinua, ila sekunde zilivyosogea ndio ikaanza kuonekana kwamba jamaa anajaribu kupora begi kwani mhindi alibana vikwapa begi lisitoke, ndiopo jamaa akatoa bisu kukata begi, mhindi alipozidi kugoma ndio akalmbwa kisu, na kuachia mzigo. Anyway polosi wakaangalie CCTV cameras za pale waone wenyewe
 
Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.
Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana ...akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana
Ulikuwa na gloves?
 
Back
Top Bottom