Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.

Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana, akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana.
Mungu akubariki sana ndugu.
Kuna mtu mmoja miaka ya 1980's aliwahi kusema kuwa DSM ndio mlango wa kuzimu.
Kwa miongo yangu minne (4) ya kuishi DSM,hakika naamini hilo.
Watu wa DSM tu wa ajabu sana.
 
Police police! Juzi wale panya rod walivyopigwa vyuma ndg zenu chadema wakaanza kuwatukana police nakutaka tume iundwe, mhindi kapigwa tunahoji police wako wapi! Waambieni chadema na bagonza wawahi sasa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asilimia 90 ya watu unaowaona karikakoo ni vibaka, waporaji, wezi wa mifukoni, na matapeli......katika hali kama hiyo ni ngumu sana kusaidia uhalifu......ukiona wanakusaidia ujue kuna fursa ya wao kuiba......ndio maana wanaweza kukutetea ukiibiwa simu alafu unajikuta mwisho huna pochi.........

Asilimia kubwa watu wanawajua wezi wote.....Kwa kifupi karikakoo ni jamhuri ya vibaka, wezi na majambazi..........

Unaweza ukajitoa kusaidia kumbe waliokuzunguka ni wezi wenzie ukazurika..........

Niliwahi kusaidia Binti mmoja aliyekuwa anaibiwa pochi lake...... katika watu waliokuja kunisaidia kukabiliana na wale vibaka na mimi wakaniibia simu yangu......mpaka leo sithubutu kusaidia...

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daah juz juz apa karume kuna mwiz kakimbia hakuna anae fata
 
Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.

Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana, akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana.
Nyerere katupa uwoga sana nchi hii.nina waswas na ile fimbo

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Kuna bodaboda mbili zilipita speed kwenda uelekeo wa mtaa wa Lindi na Livingstone, kumbe bwana walikuwa wanamkimbiza mhindi aliyekuwa kwenye bodaboda nyingine ya mbele akiwa na begi mgongoni, inasemekena ni mauzo ya dukani.

Basi nikasikia puuu, kugeuka nikaona ile bodaboda ya Mhindi ipo chini, na zile bodaboda zilizomgonga mmoja wao akashuka na kuanza kukata mikono ya begi kwa kisu, mhindi akang’ang’ani begi, maumivu ya kisu yalipozidi Mhindi akaachia begi, jamaa akapanda kwenye pikipiki wakaamsha, halafu eti watu wanaangalia tu.

Mi nilitaka kwenda ila nikaona wale jamaa ile mibisu yao sio ya kitoto, wameanza kuondoka watu ndio wanajidai kuwakimbiza, wakatokomea kupitia pale kona ya Azam, Livingstone pale.

Hadi sasa hali ni tete, polisi wawahi hapo kuchukua maelelezo.

======================

Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New Tahery Stores’.
Watu wa Dar huwajui wewe, unategemea nini kwa mdar anayelala chumbani hata hana bisibisi!
 
Mwanamme wa Dar, hata mende huwezi kuua, basi sawa!
 
Ujambazi wa aina ule ule umetokea tena pale pale.
Mtu kaporwa begi na watu wenye pikipiki, wamempiga visu vya kutosha. damu ni nyingi. Mtaa wa Lindi na Livingstone. Polisi wahini hapo haraka.

Mtu anapigwa visu raia wanaangalia tu, watu wa Dar tumekuwaje?! Mtu anapigwa visu namna ile mnaangalia tu...

Nasikia alikuwa wakala mkuu anasambaza pesa kwa mawakala, alishamaliza kusambaza zote, hivyo hawajapata kitu. Ila wamemuumiza vibaya sana.., ambulance iwahi hapo
 
Kariakoo kulivyo jaa police plus pikipiki za voda fasta,wao kazi yao kuvizia mizigo madukani na jangwani kwenye mafuso.....kariakoo ukiona uwizi police wanajua
 
Inashangaza sana, polisi tigo wamejaa kila kona, ila wao wanavizia mizigo badala ya kulinda raia
 
Back
Top Bottom