residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Mungu akubariki sana ndugu.Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.
Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.
Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana, akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.
Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana.
Kuna mtu mmoja miaka ya 1980's aliwahi kusema kuwa DSM ndio mlango wa kuzimu.
Kwa miongo yangu minne (4) ya kuishi DSM,hakika naamini hilo.
Watu wa DSM tu wa ajabu sana.