Salamu Tanzania na Kote Duniani..!
Ile patashika ya Ligi Kuu ya Tanzania Vodacom Premier League VPL, iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu inapigwa leo January 4, 2020 kati ya Simba SC na Yanga SC kunako Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na maandalizi kwa timu zote mbili na vilevile ni kwa kuwa ni mchezo wa kwanza kukutana kwa msimu huu wa VPL 2019/2020.
Simba SC ambao ndo wenyeji wa mchezo, wakiwa na ndo vinara wa VPL kwa alama 34 kwa michezo 12, Kocha wake Sven Vanderbroeck amesema kikosi kimefanya maandalizi ya kutosha na kipo tayari kwa mchezo wa leo.
Yanga SC, kwa upande wao wakiwa wameshika nafasi ya tano kwa alama 24 kwa michezo 11, kupitia Kocha Charles Mkwasa amesema, anaamini game haitakuwa rahisi kama inavyodhaniwa lakini kikosi chake kimejiandaa kwa mapambano.
Wadau wapenda kandanda nani kuibuka na Ushindi hii leo, hayo ndani ya dakika 90 za mchezo wa VPL kuanzia saa 11: 00 jioni Alasiri.
...Usikose Ukaambiwa.