Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Kariakoo haihamisishi ukuaji wa viwanda vya ndani, Kariakoo ni Dumping site ambako asilimia 100 ya products zinazo uzwa pale ni Made in nje.

Ni wajinga pekee ndio wanaoweza kuamini kwamba soko lenye asilimia 100 ya bidhaa za nje ya nchi lina umuhimu sana kwa uchumi wa nchi kuliko, Kilimo, kuliko Madini, kuliko Uvuvi na kulilo utalii.

Kariakiakoo ni makao makuu ya kituo uapnde wa Tanzania cha kupromote products za nje hasa kupromote viwanda vya China na kupelekea China kutoa ajira zaidi kwa wachina.

Huwa nashangaa sana tunapo aminishwa kwamba kariakoo ndio roho ya uchumi wa nchi, yaani sehemu inayo promote viwanda vya China inaweza vipi kuwa roho ya uchumi wa nchi?

Kariakoo ni Dumping site ya products low qualities kutoka nje ya nchi.

Kama angalau asilimia 40 ya bidhaa za kariakoo ni made in Tanzania hapo kungekuwa na logic ila asilimia 100 then wajinga sisi tunaaminishwa kwamba pale ndio uchumi wa nchi ulipo?

Vipi huko wanako enda kuchukua bishaa?

Kariakoo ni kituo moja wapo cha kuua viwanda vya ndani.

Nchi inamalizwa na siasa za kijinga sana.
 
Wachina wanazidi kula mema ya nchi na muda sio mrefu watafungua soko lao lengine.

Kweli Made In China 2025 imewanufaisha sana.

Hapa ndipo kuna umuhimu wa kuwa na mipango endelevu na target kama taifa nini tua achieve.

Kariakoo ni soko la industrial products za wachina.
 
Dunia nzima nchi zinapigana kuwa nchi za viwanda, na wanajua nguvu ta nchi yoyoe iko kwenye viwanda na si kuwa Dumping site.

Su bure meli za mizigo zinageuza tupu kurudi ziliko toka then tunashangilia, yaanu tunashangilia meli kubwa za mizigo kutua nanga kuleta products na kuondoka tupu?

Magari ya mizigo huwa yanarudi tupu Dar es salaam mengine yanaamua kubebana kwa sababu sisi ni Dumping site ya products za nje ya nchi.

Sijui SGR itabeba mizigo gani kupeleka Dar es salaam Bandarini
 
Wachina wanazidi kula mema ya nchi na muda sio mrefu watafungua soko lao lengine.

Kweli Made In China 2025 imewanufaisha sana.

Hapa ndipo kuna umuhimu wa kuwa na mipango endelevu na target kama taifa nini tua archive.

Kariakoo ni soko la industrial products za wachina.
Bongo ni siasa mkuu, ni aibu kituo cha Biashara kuwa na asilimia 100 ya bishaa. za nje na tunashangilia mno, ni ujinga mkubwa sana.
 
Wewe ni jinga kabisa.unataka kariakoo ikanunue wapi bidhaa.Nchini mwako kunakiwanda Gani Cha ngua,vifaa vya kilimo n.k.kinachotengeneza?Ni kichaa pekee anayeweza kuamini kuwa kariakoo haina umuhimu
Hujaelewa jamaa anazungumza Nini. Anataka tuwe na viwanda vinavozalisha products za kutunza hapo kariakooo.
 
Wewe unaiita Kariakoo dampo una akili kweli? Hivi unajua thamani ya mitaji ya biashara waliyoiweka watu pale?

Acha dharau mdogo wangu, pale pana mzunguko sana wa fedha na hata wateja kutoka nje ya nchi kama Congo huenda kununua bidhaa Kariakoo. Bidhaa zinatoka Kariakoo zinaenda mikoani

Mpaka Kariakoo iitwe mkoa wa kikodi unafikiri TRA walikurupuka
 
Wewe ni jinga kabisa.unataka kariakoo ikanunue wapi bidhaa.Nchini mwako kunakiwanda Gani Cha ngua,vifaa vya kilimo n.k.kinachotengeneza?Ni kichaa pekee anayeweza kuamini kuwa kariakoo haina umuhimu
Una una uelewa mdogo Sana!, kma umeshindwa kuelewa alichomaanisha mleta mada..... Kariakoo haiwezi kuwa kitovu Cha uchumi wa Nchi labda bidhaa ziwe zinadhalishwa hapa ndani!.
 
Back
Top Bottom