Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Binafsi siingii duka la aina hiyo,huwa napenda bei moja elekezi,kidogo inapunguza changamoto ie. kupigwa na usumbufu,
Simu moja unapewa bei zaidi ya nne na kuna kauli moja inanikera sana,unaenda kununua maybe pixel 9,anakutaka wewe mteja utaje bei, huwa naondoka bila kuzungumza

Kibaya zaidi,nunua bidhaa kwa winga alafu ukapate changamoto, refund inakua kama unakemea maiti iamke
 
Ahaa! Kumbe ipo hivyo. Nilishangaa bei ya electronics Kariakoo inataka kufanana na ya mikoani. Labda Kariakoo brands ni nyingi kuliko maduka ya mikoani. Pia, nilienda Karume kutafuta kiatu cha mpira cha mtumba almaarufu Six, bei ya chini walikomaa elfu 90. Nikaja mkoani nikapata kwa elfu 45 tena kikali kuliko vya Karume
Kariakoo imejaza matapeli wengi sana ambao kimsingi wanaharibu biashara. Serikali ikitaka kuweka hadhi nzuri ya hili soko, ikiwa ni pamoja na kuvutia nchi wateja wa nchi jirani kufuata mizigo hapo, ibane hawa mawinga wakanye mambo mengine ya maana.
 
Kariakoo imejaza matapeli wengi sana ambao kimsingi wanaharibu biashara. Serikali ikitaka kuweka hadhi nzuri ya hili soko, ikiwa ni pamoja na kuvutia nchi wateja wa nchi jirani kufuata mizigo hapo, ibane hawa mawinga wakanye mambo mengine ya maana.
Kweli kabisa mkuu
 
Ka frem kadogo wamejaa madalali zaidi ya 20 wanazidi hadi wateja
1727841655382.png
 
Duka moja kutokana na issue ya kodi wafanyabiashara 5 , 6 au hata 7 hushare . Lakini pia wenye duka rasmi inaweza kuisha siku nzima wasiguse Kariakoo.
Wale ni madalali ndio maana Kariakoo simu ziko juu kuliko Chanika, Mgagara kwakuwa kando ya mji hakuna madalali
 
Aisee nachukia sana matapeli.

Wenye maduka yao Kariakoo muwe na utaratibu mzuri. Sio nafika dukani nakuta madalali kibao utafkiri wasanii wapo kupakwa mafuta kwa Dee.

Mimi nikikuta dukani kuna watu zaidi ya wawili sinunui kitu alafu naenda kupublish mtandaoni, duka fulani wamenitapeli
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisaa kiongozi.
 
HII TABIA IPO PIA FOROZANI KULE ZANZIBAR
Madalali wamejaa kama wapiga debe wa standi; Unaweza jikuta unaondoka bila kupata huduma.....
 
Back
Top Bottom