Kariakoo inakuwaje duka Moja la simu Kuna wauzaji zaidi ya 20

Inaumiza hasa ukitaka kufunga mzigo wa biashara ... Sasa hivi nikiwa na mzigo mkubwa naona bora niagize tu Alibaba nivumilie kusubiri Kuliko shida ya kariakoo....
 
Binafsi siingii duka la aina hiyo,huwa napenda bei moja elekezi,kidogo inapunguza changamoto ie. kupigwa na usumbufu,
Simu moja unapewa bei zaidi ya nne na kuna kauli moja inanikera sana,unaenda kununua maybe pixel 9,anakutaka wewe mteja utaje bei, huwa naondoka bila kuzungumza

Kibaya zaidi,nunua bidhaa kwa winga alafu ukapate changamoto, refund inakua kama unakemea maiti iamke
 
Kariakoo imejaza matapeli wengi sana ambao kimsingi wanaharibu biashara. Serikali ikitaka kuweka hadhi nzuri ya hili soko, ikiwa ni pamoja na kuvutia nchi wateja wa nchi jirani kufuata mizigo hapo, ibane hawa mawinga wakanye mambo mengine ya maana.
 
Kariakoo imejaza matapeli wengi sana ambao kimsingi wanaharibu biashara. Serikali ikitaka kuweka hadhi nzuri ya hili soko, ikiwa ni pamoja na kuvutia nchi wateja wa nchi jirani kufuata mizigo hapo, ibane hawa mawinga wakanye mambo mengine ya maana.
Kweli kabisa mkuu
 
Duka moja kutokana na issue ya kodi wafanyabiashara 5 , 6 au hata 7 hushare . Lakini pia wenye duka rasmi inaweza kuisha siku nzima wasiguse Kariakoo.
Wale ni madalali ndio maana Kariakoo simu ziko juu kuliko Chanika, Mgagara kwakuwa kando ya mji hakuna madalali
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisaa kiongozi.
 
HII TABIA IPO PIA FOROZANI KULE ZANZIBAR
Madalali wamejaa kama wapiga debe wa standi; Unaweza jikuta unaondoka bila kupata huduma.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…