Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Heee heeee heeeee 🤣 🤣 🤣
Wasikuzingue hawa, hebu kula wimbo huu 👇

 
Kibisa katimba Raba raba mtoni ,jinsi kali karl kani ,alikuwa na fujo weekend ya sabato si mnakumbuka brother men? Ana shati la kitenge kifuani lina chapa kubwa ya kenge ya rangi ya udhurungi...ni kazeze ni kazeze.
 
Ila bro we bado ndezi.sana, umenunua mdosho unakuja kusfia hapa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kariakoo baba lao.

Nilikua nimeenda kununua Tende pale Msimbazi msikiti wa Idrisa kwa ajili ya iftar (kufuturisha Waislamu wenzangu nipate thawabu kwa Mola wangu. Yaani pamoja na kuwa na tabia chafu ya kutembea na wake za watu lakin najivunia kuwa Muislamu aisee. Inshallah mwaka huu nikioa nitatulia)

Sasa wakat naondoka nikapita mitaa ya katikati mule, nikaona meza moja Raba kali kinoma, zile wanaziiitaga Air Jordan, Nike, NBA snickers. Kuulizia bei zake akaanzia 20,000!

Daaah nikavikagua na kuanza kujisemea moyoni hivi si naonaga akina David Sportswear, Robyone, NjooKariakoo2020 wanauza kuanzia 65,000 mpaka 70, 0000!!!

Nikamwambia mshikaji mie nina 14,000 akanitolea nje. Nikasepa, akaniita akasema ongeza buku. Nikampa 15,000 nikabeba.

Wakuu, kumbe madukani huwa mnaibiwa. Vitu vya kijanja kwa bei za kijanja vyote vipo Kariakoo.

View attachment 1764016
Tofautisha Raba kali na Raba uliyoipenda

Mbona chongo unataka kutuamisha chongo kuwa ni kengeza we mjuba unavalisha nani hiyo raba sasa

Sent from my MI PLAY using JamiiForums mobile app
 
material yaliyotumika tengeneza itakuwa tofauti na ndio maana bei huwa tofauti
Hamna lolote ndo vile vile tu juzi nimekwenda kinunua yale mabeg ya plastic Yana kua pair 3 kwa 150000 wakati uko instagram uwa wana tangaza 250000 ata ivo nikagundua nimepigwa 10000....so dar kichwa kichwa watu uwa wanapiga sana faida aisee
 
Mkuu umeula, hapa bongo viatu OG vichache Sana , tunadanganyana Tu na brand , kiatu cha 20000 unauziwa 80000 , Bora uagize nje kwenye uhakika ..... Respect to Kariakoo , nishawah nunua mkanda 3000 pale wakat madukan ni 15000 , the same brand and quality
 
Hivi faida ya kuvaa viatu original iko wapi hasa?? Kwamba ufahari wa kuonekana umevaa maviatu ya gharama ndefu? Nani kwanza atajua kama umevaa OG au fake ikiwa kwa muonekano havina tofauti.
Fake ni fake tu mkuu huwez kuvaa famba kama hilo nyakati hizi madude kibao ya ukweli
 
Back
Top Bottom