Karibu tukujengee hii nyumba ya chumba kimoja kwa mkopo

Karibu tukujengee hii nyumba ya chumba kimoja kwa mkopo

MKOPO MKOPO wa ujenzi,
Nyumba hii inasifa zifuatazo.

Chumba kimoja kikubwa chenye washroom, sitting room kubwa,kitchen na public washroom.

Nyumba hii ni maalum kwa vijana wanaoanza maisha au kwa wanaojenga nyumba zakupangisha ni nzuri sana na haina gharama kubwa.

Gharama yake ni kiasi cha shiling million 28,000,000 tu mpaka finishing,Nyumba inakua na kila kitu kinachoitajika,maji,umeme,rangi ndani na nje,tiles,madirisha ya aluminum nk.

Namna ya malipo kwa Nyumba hii nikama ifuatavyo.

📍Malipo ya awali huanza na 30%=8,400,000

📍Deni 19,600,000

📍Mrabaha ni 10%=1,960,000

📍Jumla ya deni litakuwa 21,560,000

📍Muda wa marejesho ni miaka 4 Sawa na miezi 48.

📍Rejesho kwa mwezi litakuwa ni 449,000

Muda wakukabidhi Nyumba ni miezi sita tu.

VIGEZO;-
Uwe Mtanzania
Uwe na kiwanja chenye hati au nyaraka ya mauziano.

Kwa maelezo zaidi tembelelea office zetu zilizopo kitunda
0743257669
Nitafute whatsappView attachment 3226242

Wezi nyinyi
 
Hii nyumba kwa million 6 unahamia.
Hio 28 unajenga guest kabisa ya vyumba kumi.
Maana chumba kimoja kwa kila kitu Ina gharimu million moja na nusu.
 
Ukishakuwa na kiwanja ujenzi ni rahisi sana kuliko kununua bodaboda ya milioni 2.8 au bajaji ya Milioni 12.

Kwa DSM Ujenzi.
Tofali 70 zinajengewa namfuko 1 wa cement.(hapa ndipo wanapopigwa vijana/ wajenzi wapya)
Chumba kimoja kinatumia Tofali 450 hadi 650.
Bei ya Tofali 1,100 limeshafika site.
Mfuko wa Cement 17,000 umeshafika site
Nondo 26,000
Dirisha la Chuma 160,000
Mlango wa Chuma mzuri 210,000
Wavu wa Mbu 5,400 per meter
Misumari 1kg ,4500
Conduit pipes za umeme 1,200 per pc
Choo cha Asian type 15,000 cha kukaa 120,000
Bomba la choo 4"PVC 15,000
Bati gauge 30, ni 23,000 -30,000
Unaanza ujenzi kwakuchimba Shimo la Maji taka, kisha unalijengea kwa vitofali bila cement 300,000.
Mchanga wa hilo Shimo ndio unaanzia ujenzi. Na ujenzi unaanza site kukiwa na choo tayari cha kuanzia maisha.

Nyumbanyingi sana za kuanzia maisha Dar zimejengwa kwa style hii.
Nyumbainakamilika ukishaanza kuishi na kuanza kupikia ndani.
Finishing zingine unafanyia ukiwa unaishi humo. Faida yake hakutakuwa na uongo uongo wa mafundi/vibarua au wizi na upotevu wa vifaa .
 
Hii nyumba kwa million 6 unahamia.
Hio 28 unajenga guest kabisa ya vyumba kumi.
Maana chumba kimoja kwa kila kitu Ina gharimu million moja na nusu.
Millions 6
Mkuu Hapo Nimenunua Grill 3 Za 5 X 6
Dirusha La Aluminium 5 X 6
Mlango Wa Grill

Ukubwa Wa Vyumba Futi 10 Kwa 10
Vifaa Vya Umeme, Na Hapo Unawaka
Maisha Yanaendelea
 
Back
Top Bottom