Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Mchele,unga wa ugali ,ngano ,mafuta ,sukari ,maharagwe ,samaki ,dagaa ,njegele,karoti ,hoho,nyanya maji,vitunguu saumu,vitunguu maji,matunda,viazi mviringo,tambi,mayai,viungo vya mboga,pilau na chai e.t.c
Nyama na maini huwa nanunua fresh
Unanunua kiasi gani ?
 
Unga kg 25, Mchele 10 kg, Dagaa Kg kadhaa( huwa naongeza baada ya muda), vitunguu kg 2, Mafuta lt 5, Sukari Kg 5, Gesi full, Luku 10k, maharage kg 5, Siagi nusu Kg, maziwa. ya unga kg 2. vitu kama nyanya na mboga huwa nabadili mara njegere mara dagaa mchele na mambo yanakuwa fresh

hapo mwezi natoboa japo ni jeshi la mtu mmoja ila wanangu huwa wananiibukia weekend so tunatoa kitu kama kawa.
Nice Mzee, so damage huwa ni kama shilling ngapi kwa mwezi?
 
Unatengenezaje hizo paste

#MaendeleoHayanaChama
Paste ya nyanya inabidi ukoshe kata kuondoa mbegu iwapo una blender saga zipike vema ukiziweka kitunguu maji na swaumu na chumvi kidogo pika ziive vizuri eoua acha zipoe vema Kisha jaza katika vikopo Kama vile vya peanut butter kila kikopo kiwe kwa matumizi ya siku 3 Hadi 4

Paste ya kitunguu maji na swaumu pamoja na giligilani saga TU ujaze katika chombo chenye mfuniko haiharibiki kwa muda wote wa matumizi labda uchote na chombo au kijiko chenye maji
 
Single kwa sasa.
Mkuu hawa wanakuletea habari za nyama na sato utafikili una ajira TRA,

Uzoefu wangu
  1. Mchele kilo 45 (unatoboa miezi minne)
  2. Unga kilo 10 (usiongeze utaharibika)
  3. Maharage ya njano kilo 3 (nunua mapya huwa yanatumia mkaa kidogo kuiva)
  4. Sukari kilo 1
  5. Chumvi pakti mbili za 500
  6. Hakikisha gas iko full
  7. Mkaa nunua kidogo kidogo
Jifunze kupika matembele, mboga ya mayai, viazi mviringo mixa na nyanya, nyama nunua kwa wanao zungusha mtaani in case ukijisikia lakini

Utatoboa zaidi ya mwezi
NB: Epuka mademu wale wanaotaka pesa kupitiliza tongoza wengi wengi utampata mmoja asiye tumia pesa sana
 
Nyanya nanunua sado moja naweka kwenye friji

Carrot nanunua 2kg naweka kwenye mfuko natia kijiko naweka hata chini

Vitunguu 2kg naweka kwenye kitenga

Hoho mixer 3kg

Brocoli 2kg

Fresh beans 1kg

Zucchin 2kg nafunga kwenye mfuko kisha frijini

Tangawizi 1/2 nasaga naweka kwenye kopo natia kwenye friji

Viazi debe moja naweka sakafuni
😄😄😄😄
Wewe utakuwa una ajira mkuu
 
Mkuu hawa wanakuletea habari za nyama na sato utafikili una ajira TRA,

Uzoefu wangu
  1. Mchele kilo 45 (unatoboa miezi minne)
  2. Unga kilo 10 (usiongeze utaharibika)
  3. Maharage ya njano kilo 3 (nunua mapya huwa yanatumia mkaa kidogo kuiva)
  4. Sukari kilo 1
  5. Chumvi pakti mbili za 500
  6. Hakikisha gas iko full
  7. Mkaa nunua kidogo kidogo
Jifunze kupika matembele, mboga ya mayai, viazi mviringo mixa na nyanya, nyama nunua kwa wanao zungusha mtaani in case ukijisikia lakini

Utatoboa zaidi ya mwezi
NB: Epuka mademu wale wanaotaka pesa kupitiliza tongoza wengi wengi utampata mmoja asiye tumia pesa sana
Kwani nyama na sato ni kwaajili ya wenye nazo tu mkuu?
 
Paste ya nyanya inabidi ukoshe kata kuondoa mbegu iwapo una blender saga zipike vema ukiziweka kitunguu maji na swaumu na chumvi kidogo pika ziive vizuri eoua acha zipoe vema Kisha jaza katika vikopo Kama vile vya peanut butter kila kikopo kiwe kwa matumizi ya siku 3 Hadi 4

Paste ya kitunguu maji na swaumu pamoja na giligilani saga TU ujaze katika chombo chenye mfuniko haiharibiki kwa muda wote wa matumizi labda uchote na chombo au kijiko chenye maji

This is brilliant idea
Copied
 
Kwakweli hii elimu ya kununuwa chakula kwa mwezi ni pana sana, kuna mkuu moja hapo kauliza swali la msingi sana idadi ya wana familia ikoje?
Mini naongezea pia na wageni kwako wanakujaje? Huwa naamini kabisa ktk uhifadhi wa chakula husaidia hata mpangilio bora wamatumizi yako mengine, kwamfano sisi wafugaji naweza chinja Mbuzi 1 au kondoo halafu nimpangilie yakuwa ni wa mwezi mzima na utakapo changanya na vitu vingine ndipo utaona sasa pesa ingine uipangilie ifanye kitu gani kwa maendeleo ya familia. ila idadi ya wanafamilia inahusika sana ktk mpangilio huu.
 
Tunaotegemea kazi za kijungujiko huwa hatuli nyama wala sato hata miezi miwili mfululizo,

Ila unasurvive kibishi mpaka majirani wanashangaa wanajua una pesa nyingi
Hapana bwana usijitese hivyo,kama unapenda kula hivyo vitu,nyama kilo moja 9000,samaki badala ya kununua sato,unanunua sangala kilo moja 8500,ukikata kata vipande unapata vingi tu halafu sangala nyama yake inavimba tofauti na sato.
 
Mkuu hawa wanakuletea habari za nyama na sato utafikili una ajira TRA,

Uzoefu wangu
  1. Mchele kilo 45 (unatoboa miezi minne)
  2. Unga kilo 10 (usiongeze utaharibika)
  3. Maharage ya njano kilo 3 (nunua mapya huwa yanatumia mkaa kidogo kuiva)
  4. Sukari kilo 1
  5. Chumvi pakti mbili za 500
  6. Hakikisha gas iko full
  7. Mkaa nunua kidogo kidogo
Jifunze kupika matembele, mboga ya mayai, viazi mviringo mixa na nyanya, nyama nunua kwa wanao zungusha mtaani in case ukijisikia lakini

Utatoboa zaidi ya mwezi
NB: Epuka mademu wale wanaotaka pesa kupitiliza tongoza wengi wengi utampata mmoja asiye tumia pesa sana
Asante kwa ushauri Mkuu.
 
mchele kilo 10, unga muogo kilo 3, sembe kilo 6, samaki sato kg 4, nyama kg 10, mayai trei 1, sukari kg2 , chumv paket 3 . Vitu vingine bora uwe unanunua kwa wiki ili visioze kama nyanya , vitunguu maj/saumu, limao, matunda, mbogamboga, tangawz list kubwa sana..
Samaki kg 4 na nyama kg 10?

Mkuu hii familia ya watu wangapi?
 
Back
Top Bottom