Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

..duh...Yani wabongo! Hii nchi jamani haina njaa ...ebu tuambie hizo kilo 25 za Mchele na kilo 10 za unga ndio utazitafuna Kwa maharage kilo 3 kweli?...na ebu fafanua ulaji wako WA chumvi!...maana Kwa mwezi unakula kilo ya chumvi na kilo ya sukari..hivi Kwa uhalisia hivi viwili kipi kinatumika Sana Kwa wakati mmoja? ...yaani we unatafuna chumvi Sawa na sukari kweli! ..maajabu ya bongo haya...
 
Hapana bwana usijitese hivyo,kama unapenda kula hivyo vitu,nyama kilo moja 9000,samaki badala ya kununua sato,unanunua sangala kilo moja 8500,ukikata kata vipande unapata vingi tu halafu sangala nyama yake inavimba tofauti na sato.
Wewe unaona elfu kumi ni ndogo 😃 huku sisi nyama huwa tunanunua nusu elfu mbili kwa wale wanaotembeza mitaani kwenye ndoo, unaweza ishi kwa miatano kwa siku hapo mboga ni tembele la miambili nyanya mia mbili kitunguu mia 😃
Unapika ugali wako safi siku inaisha
 
Kilo tatu za maharage means unakuwa unakula baadhi ya siku, unapima kikombe kimoja unanunua mkaa wa miatano unabandika yakiiva unayaunga unakula siku nzima na kesho yake asubuhi unayamalizia,

Mboga mboga ndio za kununua kidogo kidogo ili zisiharibike

Kuhusu chumvi hata huwa haitumiki sana pakti usishangae ikatoboa mwezi na siku kadhaa

Kuhusu sukari chai unakunywa mara moja moja
 
..we MTU Una akili njaa Sana...Yani unawezaje kuweza kununua Mchele kilo 25 na unga kilo 10 alafu unashindwa kunywa chai Kama kawaida?...plan yako ya mlo ni muflisi sana...we hata mboga za majani utakua unapika bila mafuta...hata huo Mchele..maana hata mafuta hujaweka bajeti .inaonyesha we MTU Kwa kichemsha vitu Tu....
 
Yote ni maisha tu mkuu,kikubwa uhai
 
Mafuta yapo ya alizeti lita tano.

Wewe itakuwa hauishi kwako au huenda huwa unapikiwa ndio maana huelewi vitu vingi
 

Maharage yanachemshwa kg Moja yanaliwa Mara 6
 
Swala la bajet ndani kwako linategemea na matumizi yako,KI bongo bongo vitu vya mwezi kwangu mimi naona sio Poa,kwanza vitu vya mwezi mzigo wake ni wa Kerry.

Ukiufunga huo mzigo stock yake utafkiri muha aanapeleka dukani kwake stoo.
Vitu vya mwezi utazalisha panya wengi na utawanenepesha.

Binafsi yangu bajet yangu ni ya wiki 1 Na siku tatu hiv...

Mchele hapa maskani tunakula kg 1 mpaka nusu
Maharage nusu
Mafuta robo
Ngano kg1
Mkaa kiroba kimoja cha 17000 kwa kipimo kila siku 2000

Kwa hiyo basi

Mchele kg35
Maharage kg5
Mafuta lit 3
Ngano kg15
Mkaa kiroba kimoja
Hamila mkanda mmoja
Chumvi pakt 5 za 200

Nikiwa na hivi vitu ndani,vitu hivyo vingine kuvikosa haviniumiz kichwa.
 
Acha umasikini wewe, piga kazi mpaka ukose muda wa kupika, baadala yake unakuwa na cash ya kutosha mfukoni unakula chochote, popote wakati wowote...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…